Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

October 2017

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (aliyenyoosha mkono), akimfafanulia jambo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (wa nne kulia) wakiwa kwenye eneo la abiria wanaowasili kutoka nje ya nchi.
Kaanankira Mbise, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhamiaji Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), akieleza namna abiria anavyopata huduma ya viza mbele ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (kushoto), huku Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (kulia) akisikiliza kwa makini
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) akiwaeleza jambo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (kulia) na Kaimu Mkurugenzi Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka katika eneo la kuchukua mizigo baada ya kuwasili.


Na Mwandishi Wetu

JENGO la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII) linalotarajiwa kukamilika Desemba 2018, litafungwa mfumo wa huduma ya viza kwa njia ya mtandao (e-visa), ambao utarahisha na kuharakisha upatikanaji wake.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhamiaji cha JNIA, Bw. Kaanankira Mbise amemwambia jana Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye alipotembelea eneo la uombeaji viza kwa abiria wa kimataifa wanaowasili, kuwa wanatarajia kutumia huduma hiyo ambayo ni rahisi na haraka.

“Tayari mkakati umeanza wa kuanzisha huduma hii ya e-visa hivyo tukifanikiwa utafungwa katika jengo hili jipya, ambapo itasaidia kwa abiria kuipata huduma hiyo kwa haraka kwani itatumia mtandao,”  amesema Bw. Mbise.

Hata hivyo, Bw. Mbise amesema kwa sasa wameboresha huduma hiyo kwa wasafiri wanaowasili katika jengo la pili la abiria (JNIA-TBII) , ambapo tayari wamepatiwa mashine nne za kisasa zinazosaidia kupunguza msongamano wa abiria wenye kuhitaji huduma hiyo, hususan kipindi cha mchana chenye ujio wa ndege nyingi za nje ya nchi.

“Hizi mashine zimeharakisha upatikanaji wa huduma kwani tumeweza kuhudumia abiria wengi kwa wakati mmoja, na msongamano umepungua kiasi tofauti na awali mashine zilikuwa chache.” amesema Mbise.

Naye Mhe. Mhandisi Nditiye amesema baada ya ziara yake amegundua mashine za viza ni za muda mrefu na zinahudumia abiria mmoja kwa mrefu, na tayari ameuagiza uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kuwasilisha kwa maandishi mapendekezo yao ya namna ya kuharakisha huduma hiyo, ili serikali iyafanyie kazi kwa kusaidia kuondoa kero hiyo.

“Nimegundua kuna baadhi ya mashine za viza zimeongezwa lakini pia zilizopo zimechoka kwani ni za muda mrefu na zinahudumia abiria mmoja kwa muda mrefu na hii inaharibu sifa ya kiwanja chetu kwa wageni wanaokuja hapa nchini,” amesema Mhandisi Nditiye.

Hata hivyo, amesema wanampango wa kuongeza madirisha ya benki yanayolipia viza hizo ili kuharakisha huduma hiyo, ambapo sasa ni machache kulinganisha na idadi kubwa ya abiria wanaowasili kwa ndege kubwa. Ndege hizo ni Emirates, Etihad, Oman Air, Qatar, South Africa Air na Ethiopia, ambazo zimekuwa zikipishana kwa muda mfupi.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa TAA, Richard Mayongela amesema tayari wanampango wa kuongeza upana wa eneo hilo la wasafiri wanaowasili wa kimataifa, ambapo sasa kumekuwa na msongamano kutokana na ufinyu wake.

“Hili jengo linazaidi ya miaka 30 na ukiangalia abiria waliokuwa wamekadiriwa wakati ule lilikuwa likikidhi mahitaji, lakini sasa abiria wameongezeka na eneo limekuwa dogo, hivyo tayari tumeanza kwa kuondoa baadhi ya ofisi ili kuongeza upana wake, ninaimani litapunguza msongamano uliopo sasa,” amesema Bw. Mayongela.   

Lakini pia Bw. Mayongela amesema sasa wapo katika mazungumzo na Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), ili kuangalia namna bora ya kuzipangia muda ndege zinazopishana muda mdogo kwa wakati wa mchana ili ziachiane muda mrefu, ambapo kutasaidia kupunguza msongamano


Awali eneo hilo linakumbwa na changamoto kubwa ya msongamano wa abiria wanaohitaji huduma ya viza baada ya uchache mashine zinazosimamiwa na Idara ya Uhamiaji zilizokuwepo na kufanya abiria wanaohitaji huduma hiyo kutumia muda mrefu kuipata.  

POLISI  Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imelaani vitendo vilivyofanywa na askari ambavyo havina maadili ya kazi.
 
Taarifa ya polisi ya jana Jumanne Oktoba 24, 2017 imesema jalada limeshafunguliwa na uchunguzi unaendelea ili kuwabaini  waliohusika kuwapiga wananchi.
 
Imeelezwa askari hao walijichukulia sheria mikononi baada ya mwenzao Charles Yanga kukutwa ameuawa na mwili wake kuachwa pembezoni mwa uzio wa kambi ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) iliyoko Ukonga.
 
Kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema Jumapili Oktoba 22,2017 walipokea malalamiko ya watu wanaosadikiwa kuwa askari kufanya msako na kuwapiga wananchi wanaoishi jirani na kambi ya FFU ambao hawana hatia.
 
“Jeshi la Polisi linalaani vitendo hivyo ambavyo havina maadili ya kazi za polisi. Jalada limefunguliwa na uchunguzi unaendelea ili kuwabaini watuhumiwa wa tukio hilo. Tunaomba wananchi watoe ushirikiano kutoa taarifa za wahusika waweze kuwachukulia hatua watu au askari waliohusika na matukio hayo,” alisema.
 
Kamanda Mambosasa amesema Oktoba 21,2017 saa sita usiku maeneo ya kambi hiyo askari wakiwa kazini walikuta mwili wa askari huyo, huku pikipiki aliyokuwa akiendesha ikiwaka taa za tahadhari.
 
Amesema mwili wa askari huyo ulikuwa na majeraha kwenye paji la uso na sikio moja likiwa limekatwa.
 
Kamanda Mambosasa amesema walipofuatilia wamebaini askari huyo aliuawa na watu wasiojulikana na kutelekezwa katika maeneo ya kambi ya polisi.
 
Amesema kupitia kikosi kazi cha polisi wanaendelea na msako kuhusu tukio hilo la kikatili li kuwabaini watuhumiwa waliohusika.

NA MWANDISHI WETU, DAR

MSANII ambaye hakauki vituko mitandaoni Harmorapa, amewajibu watu wanaomsema kuwa amepotea pamoja na kiki zake zote, na kusema kwamba hajapotea isipokuwa yuko busy na biashara.

Harmorapa ameyasema hayo kwenye eNewz ya East Africa Television, na kusema kwamba watu wanatakiwa wajue licha ya muziki Harmorapa ana maisha yake mengine ambapo pia ni mfanyabiashara, na sasa hivi yuko busy na kazi za biashara ikiwemo kusafiri, lakini mashabiki wake wakae mkao wa kula kwani muda si mrefu atawapa kazi mpya.

"Watu waelewe sipo kimya, sasa hivi nipo busy na biashara nasafiri sana, ile kuonanana tu ni bahati,  project zangu za muziki zinaendelea kama kawaida wiki ijayo naachia dude jipya, watu wajue tu mimi nipo, wamemzoea Harmorapa leo kafanya hiki mara hiki, sasa hivi niko busy na muziki wangu bado upo, kama kutrend kila siku natrend, naingia Instagram nakuta tu mtu amenipost bado machoni mwa watu naonekana, bado mimi nipo na nitakuwepo na vitu vitaendelea", amesema Harmorapa.

Hivi karibuni kumekuwa na tetesi kwamba msanii huyo ameshapotea kwenye game, kwani hawezi kufanya muziki na anachotegemea yeye ni kiki ambazo anazifanya na kuchekesha watu.


MAHAKAMA  ya Wilaya ya Arusha, imepanga  kuanza kusikiliza kwa siku tatu mfululizo kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), kwa upande wa Jamhuri kuanza kuleta mashahidi wao.

 Hatua hiyo inakuja baada ya jana upande wa Jamhuri kumsomea maelezo ya awali mshtakiwa huyo ambaye pia anakabiliwa na kesi nyingine ya uchochezi katika Mahakama ya Wilaya ya Arumeru.

 Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Devota Msoffe, alisema kutokana na kesi hiyo kuwa nje ya wakati, itasikilizwa siku tatu mfululizo kuanzia Novemba 27 hadi 29, mwaka huu.

 “Tutasikiliza kesi hii siku tatu mfululizo kwani iko nje ya wakati na natoa agizo kwa mashahidi wa Jamhuri kuitwa ambapo tunatarajia kufunga ushahidi wao Novemba 29,” alisema Hakimu huyo.

Wakili wa Serikali, Agness Hyera, akimsomea Lema maelezo ya awali katika kesi hiyo namba 440 ya mwaka 2016, alidai kuwa mshtakiwa huyo anakabiliwa na shtaka moja la uchochezi  ambapo anadaiwa kutenda kosa hilo Oktoba 22, mwaka jana katika eneo la Kambi ya Fisi, Kata ya Ngarenaro akiwa anahutubia mkutano wa hadhara.

Miongoni mwa maneno ya uchochezi anayodaiwa kuyatoa Lema ni pamoja na: “Rais Magufuli akiendelea na tabia ya kudhalilisha demokrasia na uongozi wa upinzani iko siku Taifa litaingia kwenye umwagaji wa damu,…. “Rais yeyote ambaye haheshimu mipaka ya sheria, mipaka ya Katiba, rais huyo ataliingiza Taifa katika majanga na umwagaji damu,watu watajaa vifua, wakiamua kulipuka polisi hawa wala jeshi halitaweza kudhibiti uhalifu utakaojitokeza.”

Baada ya kumsomea mashtaka hayo, Wakili Hyera aliiomba mahakama kupanga tarehe ya kuanza kusikiliza na kuwa hawakuwa tayari kuweka hadharani majina ya mashahidi wao wala vielelezo ambapo alisema wanatarajia kuwa na mashahidi wasiozidi 10.

Katibu Mkuu wa chadema Dk. Vincent Mashinji
KATIBU  Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Dk. Vincent Mashinji ametakiwa kuripoti ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), imeelezwa.

Dk Mashinji anakwenda kuripoti kipindi ambacho Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa chama hicho, Kigaila Benson anaendelea kushikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwananchi leo Oktoba 25,2017 mwanasheria wa Chadema, Fredrick Kihwelo amesema, “Katibu Mkuu ametakiwa kuripoti kwa DCI na sasa natoka hapa Central kwa Kigaila nakwenda huko."

Amesema suala la Kigaila kupata dhamana au kupelekwa mahakamani litajulikana mchana wa leo baada ya kutakiwa kurudi Kituo Kikuu cha Polisi.

Kihwelo alipoulizwa ni nini sababu ya Dk Mashinji kuitwa kwa DCI, amesema itakuwa ni mwendelezo wa mahojiano na Jeshi la Polisi kuhusu tuhuma za kutoa lugha za uchochezi alipozungumzia hali ya afya ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Kigaila ambaye ameshafikisha saa 72 akiwa rumande tangu alipojisalimisha kituoni hapo Jumatatu Oktoba 23,2017 na kuhojiwa kwa kutoa lugha za uchochezi katika mkutano na wanahabari Oktoba 12,2017 makao makuu ya Chadema wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam.

Hussein Mohammed Bashe
MBUNGE  wa Jimbo la Nzega kwa tiketi ya (CCM) Hussein Mohammed Bashe amefunguka na kusema zaidi ya asilimia 60 ya wakazi wa kijiji cha Undomo kilichopo Kata ya Uchama Nzega wamehama makazi yao kutokana na kamata kamata inayofanya na jeshi la polisi.

Bashe amesema hayo baada ya jana kufanikiwa kuzitembelea familia tano ambazo zimeathirika kutokana na imani za kishirikina ambapo kina mama watano walipigwa na kuchomwa moto na wanakijiji wakituhumiwa kuwa ni wachawi, kufuatia jambo hilo jeshi la polisi liliweza kukamata watu zaidi ya 60 na kuligeuza tukio hilo kama njia ya kujipatia kipato jambo ambalo Mbunge anasema halikubaliki.

"Kina mama watano walipigwa na kuchomwa moto kwa kuwa walituhumiwa kuwa ni wachawi, jeshi la polisi lilikamata watu zaidi ya 60 na uchunguzi unaendelea, jambo jingine ambalo limejitokeza wakazi zaidi ya asilimia 60 wamehama na kufunga nyumba zao kwakua jeshi la polisi limegeuza tukio hilo mradi na kila mtu ambae anakipato hukamatwa na kutakiwa atoe rushwa ama asipotoa anaunganishwa katika kesi jambo hili nimelifikisha kwa mamlaka husika" alisema Bashe.

Mbunge Hussein Bashe akiwa na familia ya Katekista ambae mke wake alichomwa moto na watu wasiokua na utu wala ubinadamu katika kijiji hicho.

Aidha Mbunge Bashe amesema kuwa ofisi yake itashirikiana na jeshi la polisi ili wale waliohusika kweli kwenye tukio hilo waadhibiwe ila wale ambao hawahusiki na wamekamatwa wasigeuzwe chanzo cha mapato kwa askari wa polisi na jeshi hilo.

Marehemu Steven Kanumba
MBELE  ya Jaji Sam Rumanyika leo Oktoba 25, 2017 katika mahakama kuu Kanda ya Dar es salaam, imemaliza kusikiliza ushahidi wa kesi namba 125/2012 inayomuhusu Msanii Elizabeth Michael maarufu kama 'Lulu' ya kumuua mpenzi wake Steven Kanumba bila kukusudia, ambapo kesho Oktoba 26 Mahakama hiyo itasikiliza maoni ya Baraza la wazee wa mahakama sambamba na kupanga tarehe ya hukumu.

Kwamujibu wa maelezo ya shahidi namba 2  na wa mwisho kwa upande wa mshitakiwa, aliyefahamika kama Josephine Mshumbus yaliyosomwa kwaniaba yake na Staff Sajenti wa polisi Detective E103 Aitwaye Nyangea, aliyotoa 23/04/2012, ameeleza kuwa yeye alimfahamu Marehemu Steven Kanumba Kama Mgonjwa wake katika kituo chake cha tiba mbadala cha Precious Clinic kilichokuwepo karibu na Jengo la Mawasiliano Jijini Dar es sala.

 "Steven Kanumba alikuwa ana matatizo ya sumu mwilini na alikuwa anakuja kwenye kituo changu cha Kliniki Ambapo alikuwa akifanya vipimo vya mwili mzima na aligundulika kuwa na tatizo la Mafuta (Cholestrol), tatizo la Moyo, Upungufu wa Hewa ya Oksijeni kwenye Ubongo ambayo yalimsababishia maumivu makali.

Hata hivyo niligundua kuwa wakati akiendelea na tiba alikuwa akifanya mazoezi ya kutanua misuli, nilimkataza mara moja kwakuwa angeweza kupoteza maisha au Kupooza baadhi ya sehemu za mwili wake.

Kuna siku alikuja kunilalamikia kuhusu maumivu makali anayopata kwenye Moyo, lakini kulingana na wingi wa wateja sikuweza kumuhudumia lakini tulipanga kuonana siku nyingine lakini haikuwezekana tena" Maelezo ya Shahidi yameeleza.

Upande wa Mstakiwa uliongozwa na Wakili msomi Peter Kibatala, Huku Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili Faraja George.

Upande wa Jamhuri uliwasilisha mashahidi Nne, na Upande wa Mstakiwa uliwasilisha mashahidi Wawili. 

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (katikati mstari wa mbele), akinyanyua mikono juu kuashiria mshikamano daima na baadhi ya viongozi wa matawi wa chama cha wafanyakazi mahala pa kazi (TUGHE) matawi ya Makao Makuu na Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), alipokutana nao leo.

Viongozi wa Chama cha Wafanyakazi mahala pa Kazi (TUGHE) matawi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Makao Makuu (TAA HQ) na Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), jana wakimsikiliza kwa makini Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Bw. Richard Mayongela (kushoto) alipokutana nao leo.



Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela leo akiongea na baadhi ya viongozi wa Matawi ya Chama cha Wafanyakazi mahala pa kazi (TUGHE), TAA Makao Makuu na Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).


Na Mwandishi Wetu

KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela amewataka viongozi wa wafanyakazi kupitia matawi mawili ya  Chama cha Wafanyakazi, TAA Makao Makuu na Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), kutenda haki kwa kusikiliza malalamiko ya wafanyakazi wote bila kubagua na kuwasilisha kwa mwajiri ili yaweze kufanyiwa kazi kwa wakati.

Bw. Mayongela ametoa kauli hiyo leo wakati viongozi wa matawi hayo walipokwenda kujitambulisha ofisi kwake TAA Makao Makuu, ambapo alisisitiza kuwa wafanyakazi wa chini ndio wenye matatizo makubwa lakini wamekuwa hawasikilizwi na kutatuliwa matatizo yao kwa wakati.

“Ninashukuru uongozi mmekuja kuonana nami, ninahitaji ushirikiano wenu kama chama cha wafanyakazi, muwatumikie wafanyakazi kwa kutenda haki mkisikiliza matatizo ya kila mmoja na kufikisha sehemu husika na ninawaahidi kuwa nanyi bega kwa bega kutatua matatizo ya wafanyakazi kwani wao ndio wanafanya TAA iwepo, endapo wakifanya kazi bila manung’uniko wala makundi, mamlaka yetu itasonga mbele kwa kuwa uongozi sio kupigana vita bali tunatakiwa kujenga na kuwa kitu kimoja.” amesema Bw. Mayongela.

Hatahivyo amesema, kwa sasa yupo mbioni kuangalia namna ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi  kwa kupitia makusanyo yatakayotokana na vyanzo mbalimbali vya mapato ili kuongeza tija na ufanisi wa kazi, kwa kuwa inaonekana wengi wamekata tamaa kutokana na kufanya kazi nyingi na wakati mwingine kupitiliza muda wa kazi wa kawaida bila kupata stahiki yeyote.

“Kwa msaada wa Mungu nina imani atanionyesha wapi fedha zilipo na jinsi ya kuzitumia ipasavyo kwa masuala ya msingi, na ninakusudia hadi kufika Desemba mwaka huu niweze kuboresha maslahi ya wafanyakazi. Watu wanafanya kazi sana lakini maslahi ni madogo, unaona kabisa jinsi mtu anavyoitumikia taasisi kwa moyo, lakini sura inaonesha jinsi alivyokata tamaa, ninaamini kwa kufanya hivi itaongeza tija na bidii ya kazi.” amesema Bw. Mayongela.

Halikadhalika, Bw. Mayongela amesema atahakikisha wafanyakazi wanapata vitendea kazi vya uhakika kulingana na kazi zao, zikiwemo bajaji, pikipiki na magari kwa ajili ya doria na kwa shughuli za uendeshaji ndani Viwanja vya Ndege.

Pia amewataka viongozi hao kuwa karibu na wafanyakazi ili kuhakikisha wanawahamasisha wanafanya kazi kwa bidii, uaminifu na uadilifu ili kuondoa mianya na tabia za upokeaji wa rushwa, kwa kuwa TUGHE ni daraja kati ya mwajiri na wafanyakazi.

Naye Mwenyekiti wa TUGHE tawi la TAA Makao Makuu, Bw. 
Nasib Elias mbali na kumshukuru Kaimu Mkurugenzi Mkuu kwa kuwapa fursa ya kukutana naye, lakini amemuomba kuendelea kudumisha mahusiano baina ya mwajiri na chama cha wafanyakazi (TUGHE), na pia kumuomba aitake menejimenti yake kuwa na utaratibu wa kuweka milango wazi kwa wafanyakazi kama yeye ili waweze kusikiliza na kutoa majibu sahihi kwa baadhi ya masuala ya kiofisi yanayowasilishwa na wafanyakazi kwao na sio kila jambo liwasilishwe kwake.

“Tunakuombea kwa Mungu akutie nguvu kwa haya unayotaka kufanya likiwemo la kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa kuwa litasaidia kuamsha morali ya kazi kwa wafanyakazi, lakini hii sera yako ya kuwacha milango wazi tunaomba nayo itekelezwe katika ngazi ya menejimenti yako kwani kuna mambo ambayo yanaweza kumalizwa na Wakurugenzi na Mameneja wenyewe na sio lazima yafike kwako, “ amesema Bw. Elias.

Katika kuboresha maslahi ya wafanyakazi ambacho kimeonekana ni kipaumbele cha Kaimu Mkurugenzi mkuu kwa wafanyakazi, Bw. Elias amemuomba kuangalia namna bora ya kusimamia maslahi hayo ikiwemo kuuasili mkataba wa hali bora (SBA) kama inavyotekelezwa na taasisi nyingine za serikali.

Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita (katikati) mwenye suti akiwa katika harambee ya kuchangia kwaya ya Bikira Maria Mama wa Mungu kigango cha Vijibweni wa kwanza kulia ni Padri Gerevas Lyimo wa parokia ya Kigamboni.


Wanakwaya wa kwaya ya Bikira Maria Mama wa Mungu kigango cha Vijibweni.

MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amesema waimbaji wa nyimbo mbalimbali za injili,  Wanakwaya wanapaswa kutangaza amani na upendo katika Taifa kupitia unjilishaji ili amani iliyopo  isiharibiwe na watu wachache.

Meya Mwita amesema kuwa waimbaji mbalimbali ikiwemo kwaya za makanisa wanayonafasi kubwa ya kuhubiri upendo na hivyo nchi ikaendelea kuwa na amani na hivyo kusababisha watu kufanya kaTanzania ikaendelea kusifiwa nakuwa mfano mzuri wa kuigwa.

Meya Mwita ametoa kauli hiyo jijini hapa leo wakati alipokuwa akiendesha harambee ya kuchangia kwaya ya Bikira Maria  Mama wa Mungu katika kigango Cha Vijibweni Parokia ya Kigamboni  jumla ya shilingi milioni Nne zilipatikana.

Amesema katika kuhubiri amani, Taifa linategemea waimbaji wa jimbo za dini, viongozi wa kiroho makanisani,mikitini  na kwamba kwa kufanya hivyo taifa litaendelea kusimama imara pasipokuwa na machafuko yoyote licha ya changamoto mbalimbali zilizopo.

Ameongeza kuwa mbali na kujenga amani lakini pia itawezesha kurudisha maadili kwa vijana, makundi mengine  kwakuwa ndio wanaotegemewa katika kutangaza maadili mema katika Nyanja mbalimbali katika jamii.

“Mnapoona  viongozi tunafanya mambo yasiyo mpendeza mungu hamna budi kutukemea kupitia njia hii ya unjilishaji kwasababu ujumbe unatufikia” amesema Meya Mwita.

“ Lakini kama mtakuwa mnaona halafu mkanyamaza, itakuwa hamja wasaidia waumini wetu, wananchi ambao wananunua na kusikiliza nyimbo zenu, kila mmoja anajukumu la kuhubiri na kulinda amani ya nchi yake” ameongeza.

Kwaupande wake Mwenyekiti wa Kwaya hiyo Faustine Kabaganya amemshukuru Meya Mwita kwa na kusema kuwa wanatambua mchango wake kwa kuwa ni kiongozi ambaye anajali makundi yote.

Ameeleza kuwa kwaya hiyo natarajia kuingia studio kwa ajili ya kurekodi albamu na kwamba wamemshukuru kwa mchango ,hamasa ambayo ameitoa katika harambee hiyo.


MsimamiziwashughulizamzaniwaTindekutokaWakalawaBarabara (TANROADS),mkoaniShinyanga, Bw. LugembeVicent (kushoto), akitoataarifayakiutendajiyamzanihuokwaNaibuWaziriwaUjenzi, UchukuzinaMawasiliano (SektayaUjenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa. Mzanihuounapimamagari 300 kwasiku.
NaibuWaziriwaUjenzi, UchukuzinaMawasiliano (SektayaUjenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa, akiangalianamnawatumishiwamzaniwaTinde, mkoaniShinyangawanavyopimanakurekoditaarifazamagariyanaoingiakupimauzitokwenyemzanihuo.

Magariyakiwakatikafolenikusubirihudumazaupimajiuzitoilikuendeleana safari kwenyemzaniwaTinde, mkoaniShinyanga.

MuonekanowabarabarayaUyovu- Bwanga (KM 45) kwakiwango cha lamiiliyopomkoaniGeita, ikiwaimekamilikakwaasilimia 98.

NaibuWaziriwaUjenzi, UchukuzinaMawasiliano (SektayaUjenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa (Mwenyesuti),kiangalianamnashughulizaupimajiwamagarizinavyoendeshwakatikamzaniwaTinde, mkoaniShinyanga. KushotokwakeniMenejawaWakalawaBarabara (TANROADS), wamkoahuo, MhandisiMibalaNdilindi.
Wafanyakaziwamizaninchiniwametakiwakufanyakazikwaweledi, uadilifunakuachananavitendovyarushwailikuletatijanaufanisiwakazizao
katikausimamiajinaulinziwabarabaraambazoSerikaliimekuwaikitumiagharamakubwakatikaujenzi wake.
HayoyamesemwanaNaibuWaziriwaUjenzi, UchukuzinaMawasiliano (SektayaUjenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa, leomkoaniShinyanga, alipokuwaakikagua  mzaniwaTinde(Shinyanga), naMwendakulima (Kahama),  ambapoamesisitizaushirikianokatiyawafanyakazihaonamaderevailikutatuachangamotozinazojitokezakatika  vituovyamizani.

"Watumishinamaderevashirikianenikutokomezavitendovyarushwa, kamwemsijihusishekutoawalakupokearushwailikupatahudumazaharaka, tukikubainitutakuchukuliahatua kali zakisheria", amesemaNaibuWaziriKwandikwa.
Aidha, ametoawitokwamaderevawamagariyamizigowanaotakiwakuwanastikamaalumzausafirishajiwamizigoyaokufuatautaratibuwakuchukuastikahizomahalihusikailikuepusha usumbufunamsongamanowamagarikatikavituovyamizani.

Akiwa katikaeneo la sehemuyamaegeshonakulazamagarimjiniKahamaNaibuWaziriKwandikwa, ametoawitokwaviongoziwaHalmashaurihiyokuchukuahatua kali kwamaderevawanaopakinjeyaeneohilo, ilikudhibitiuchafuziwamazingiraunaowezakufanywanabaadhiyamadereva hao.
AmeshaurikwauongoziwaHalmashaurihiyokuonanamnayakujengamaegeshomenginekamahayoilikupatachanzo cha mapatonakusaidia kuujengamjikuwanaTaswiranzuri.
Kwaupande wake, MenejawaWakalawaBarabara (TANROADS), mkoaniShinyanga, MhandisiMibalaNdilindi,amethibitishakuwepokwavitendovyarushwakwabaadhiyawafanyakaziwamizaninchiniambapoamefafanuakatikakupambananasualahilokwawatumishiwamkoa waketayarimweziuliopitaamewachukuliahatuazakinidhamuwatumishiwatatuwamzaniwaMwendakulima.
Naye, MsimamiziwashughulizamzaniwaMwendakulimakutoka TANROADS Shinyanga, Bi HeriethMonjesa,amesemakuwachangamotozamsongamanowamagarikatikamizanizinasabaishwanabaadhiyamaderevawamagariyamizigowanaotakiwakuwanastikamaalumzausafirishajiwamizigoyaokushindwakufuatautaratibu, hivyokupelekeausumbufukwawahudumunawatumiajiwenginewamizani.


Katikahatuanyingine, NaibuWaziriKwandikwa, amekaguabarabarayaUyovu-  Bwanga (KM 45), ambapoujenzi wake kwasasaumefikaasilimia 98 namkandarasiamebakishakazizaujenziwamiferejinauwekajiwaalamazabarabarani.

JUMLA ya shilingi milioni 202 zimetolewa kwa vikundi 89 na Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora ikiwa ni sehemu ya mikopo ya kuwezesha vijana , wanawake na walemavu.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri 

Fedha hizo zimekabidhiwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa sherehe fupi ya uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake na kukabidhi mkopo iliyofanyika mjini Kaliua na kuhudhuria  na wabunge wa majimbo yote mawili ya Wilaya hiyo.

Alisema mkopo huo ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya viongozi wa juu ya kutaka kila Halmashauri itenge asilimia kumi ya mapato ya ndani kwa ajili ya uwezeshaji wa vikundi vya wanawake asilimia nne, uwezeshaji vijana asilimia nne na uwezeshaji watu wenye ulemavu asilimia mbili.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora alitoa wito kwa vikundi vya wanawake vilivyofanikiwa kupata fedha hizo kuzitumia katika malengo waliyoweka ili waweze kuzirejesha kwa ajili ya kuwakopesha wengine.

Alisema kuwa ni vema fedha walizokopeshwa wakazitumia kwa ajili ya shughuli zao za maendeleo na kisha wazirudishe  ili kije kigezo cha siku nyingine kuweza kukopesheka.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama aliwakumbusha vikundi vilivyokeshwa kutambua kuwa fedha hizo sio hisani bali ni mkopo ambao wanapaswa kuufanyia kazi ili waweze kupiga hatua na kisha waurejeshe ili vijana na wanawake wenzao nao wapate fursa ya kukopa.

Alisema kuwa wanaimani kuwa kundi hilo likitumia vizuri mikopo hiyo jamii yote ya wilaya itakuwa na maendeleo na uchumi wa Wilaya hiyo utaimarika.

Kwa upande Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kaliua John Pima alisema kuwa wataendelea kuhakikisha kuwa kila mwezi wanatenga fedha kutokana na mapato ya ndani ili baadae wawakopeshe wanawake, vijana na walemavu kwa ajili ya kusaidia kuboresha maisha yao na jamii inayowazunguka.

Naye Mbunge Jimbo la Ulyankulu John Kadutu alitoa wito kwa wakazi wa Wilaya ya Kaliua kuungana katika shughuli za maendeleo bila kujali tofauti za itikadi zao za vyama.

Alisema kuwa yeye na mbunge wa Kaliua ambaye anatoka Chama cha waananchi CUF wamekuwa mstari wa mbele kupigania maslahi ya wananchi wote na kuwataka viongozi vingine waige mfano huo.

Wakati huo huo Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua imetoa pikipiki nane zenye thamani ya shilingi milioni 18.9 kwa ajili ya Maafisa Ugani wanne na Watendaji wa Kata wanne ili kuimarisha utoaji wa huduma kwa wakazi wa maneo yao.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Pima , pikipiki hizo zinalenga kuwaondolewa Maafisa Ugani uhaba wa usafiri ili waweze kuwahudumia vizuri wakulima na kuwasaidia ili waweze kupata mazao mengi na bora.

Alisema kuwa wakati mwingine ilikuwa vigumu kwa Maafisa Ugani kuwafikia wakulima kwa sababu ya kuwa mbali na hivyo vyombo hivyo wa usafiri vitasaidia kuondoa visingizio kwa watumishi hao.

Kuhusu watendaji wa Kata kupata usafiri huo alisema kuwa zitawasaidia kuimarisha shughuli za utawala ikiwemo kusikiliza kero na matatizo mbalimbali ya wananchi na kuwaondolea shida ya wananchi  kusafiri umbali mrefu ili kuwafuata viongozi.

Akiongea wakati wa kukabidhi pikipiki hizo kwa watumishi hao Mkuu wa Mkoa wa Tabora aliwaonya kutumia vyombo hivyo kuwasaidia wananchi na sio kwa maslahi binafsia kama vile kubeba mizigo na wakati mwingine kuzigeuza bodaboda.

Alisema kuwa atakayebainika atachukuliwa hatua kali ili ije iwe fundisho kwa wengine.

Watendaji walipata pikipiki wanatoka kata za Ilege, Igwisi, Usimba na Nhwande na kwa upande wa Maafisa Ugani watoka kata za Seleli, Zugumlole, Silambo na Ukimbisiganga.


WALIMU wilayani Sikonge wameiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kulipa madai ya muda mrefu kwani yamekuwa yakipunguza ari ya utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.


Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Walimu (CWT) wilayani Sikonge Perez Kuduhula katika mkutano uliowakutanisha walimu hao kwa lengo la kutathmini utendaji wao wa kazi pamoja na  kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili

Alisema kuwa baadhi ya walimu walishapandishwa madaraja lakini wamekuwa wakiendelea kupata mshahara ule ule wa kabla hajapandishwa.

Kuduhula aliongeza kuwa wapo wengine wamekuwa wakidai gharama za masomo , nauli na gharama za matibabu jambo ambalo linawatia hadi sasa hawajatimiziwa.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Simon Ngatunga aliwataka walimu hao kuwa wavumilivu kwani serikali inafanya jitihada za kulipa madai yao.

Alisema kuwa Halmashauri hiyo itaendelea kulipa madai hayo ya walimu kadiri itakavyokuwa ikipokea  fedha .

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alisema kuwa pamoja na changamoto hizo zinazowakabili walimu amewataka walimu kuendelea kujituma ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi.

Alisema kuwa Serikali inaendelea kushughulikia matatizo yao ya ya wale watumishi wengine ni vema wakawa na subira kwani ilikuwa katika zoezi zito la kuhakiki wafanyakazi hewa.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora Mwanri ametoa wiki mbili kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya, Mji na Manispaa pamoja na Maafisa elimu wilaya kukaa na Wazazi na Walezi kupanga mipango ya kutekeleza utoaji wachakula kwa wanafunzi kwa shule ambazo hazijaanza kutekeleza mpanga huo.

Alisema kuwa Kiongozi yoyote mwenye dhamana atakayeshindwa kutekeleza jukumu hilo hatasita kumwajibisha kwani ukosefu wa chakula shule hasa kwa wale wanafunzi wanaoishi mbalimbali na shule umekuwa ukisababisha utoro na ufaulu mbaya.


Mwanri alisema kuwa mwanafunzi hawezi kumsikiliza vizuri mwalimu kama anasumbuliwa na njaa na wakati mwingine anatoroka shule pindi anapokuwa na njaa.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa kampuni ya Yapi Merkezi Abdullah Kilic, anayejenge reli ya kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam-Morogoro  yenye urefu wa KM 205 eneo la Soga, mkoani Pwani. 

Meneja Mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Mhandisi Maizo Mgedzi, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, alipokagua ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam-Morogoro yenye urefu wa KM 205 eneo la Soga, mkoani Pwani, inayojengwa usiku na mchana.

Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Kampuni ya Yapi Merkezi Abdullah Kilic, akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), kutoka Dar es Salaam-Morogoro yenye urefu wa KM 205 kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, katika eneo la Soga, mkoani Pwani.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akimpongeza mwanamke anayeendesha mtambo wa kutengeneza tuta la reli ya kisasa (SGR), Bi Miriam Juma alipomkuta saa 4 za usiku akichapa kazi katika eneo la Soga, mkoani Pwani

Muonekano wa Mitambo ya kisasa inayojenga Reli ya Kisasa (SGR), kutoka Dar es Salaam-Morogoro yenye urefu wa KM 205 eneo la Soga mkoani Pwani, inayojengwa kwa saa 24.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amezungumzia umuhimu kwa wafanyakazi wote waliopata fursa ya kujenga reli ya kisasa (SGR) kufanya kazi kwa moyo na uzalendo mkubwa ili kuandika historia katika maendeleo ya Tanzania.

Profesa Mbarawa amesema hayo alipokagua ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), inayojengwa usiku na mchana kuanzia Dar es Salaam-Morogoro  yenye urefu wa KM 205 na kuzungumzia kuridhishwa na kasi ya ujenzi huo.
“Hii ni fursa kubwa ambayo mmeipata kujenga mradi mkubwa utakaocha historia katika nchi hii hivyo fanyeni kazi kwa bidii, weledi na uzalendo”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Amewataka viongozi wa Shirika Hodhi la Rasilimali za Reli (RAHCO), kuwa katika eneo la mradi wakati wote ili kuhakikisha mkandarasi anapata ushirikiano wa kutosha na hivyo kuwezesha mradi kukamilika kama ilivopangwa.
Aidha amemuagiza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO Mhandisi Edward Malima, kuhakikisha wanafunzi wa uhandisi wanapata nafasi ya kutosha ya kushiriki kwa vitendo katika ujenzi huo ili kuiwezesha nchi kuwa na wataalamu wa kutosha wenye uzoefu kwenye ujenzi na usimamizi wa miradi ya reli.
“Ongezeni wahandisi wanafunzi katika mradi huu, nia yetu ni kupata reli lakini pia na wataalamu wengi katika ujenzi na uendeshaji wa reli”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Naye  Mhandisi Edward Malima, amempongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa kufanya ziara ya kustukiza usiku ambayo imechochea hamasa kwa wafanyakazi na mkandarasi na kuahidi  kumsimamia mkandarasi kikamilifu ili mradi huo ukamilike kwa wakati na uwiane na thamani ya fedha.

Takribani shilingi trilioni 2.8 zinatarajiwa kutumika kujenga reli ya kisasa (SGR), awamu ya kwaza kati ya Dar es Salaam na Morogoro yenye urefu wa KM 205 itakayowezesha treni ya umeme yenye kasi ya KM 160 kwa saa kupita na hivyo kuhuisha mfumo wa usafiri wa reli hapa nchini.

NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI DAR

MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amewataka vijana kuacha tabia ya kuchagua kazi za kufanya,  kutegemea ajira serikalini badala yake wawe wabunifu na kuwa tayari kufanya shughuli yoyote isipokuwa ya kiuhalifu.

Meya Mwita ametoa kauli hiyo jijini hapa leo wakati akizungumza na wanafunzi wanaohitimu elimu ya kidato cha nne katika shule ya Sekondari Minazini iliyopo Kata ya Vijibweni ,Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni .

Meya Mwita ameeleza kuwa vijana wengi wanachagua kazi kwa malengo ya kusubiri ajira kutoka serikalini jambo ambalo alisema sio sawa na kwamba wanapaswa kufanya shughuli yoyote ambayo itawaingizia kipato na kuweza kuendesha maisha yao.

“ Vijana wangu tufanyeni kazi, tuache habari za kuchagua kazi ipi unataka kuifanya, kazi ni kazi tu ilimradi inakuingizia kipato cha kuendesha maisha yako, lakini msifanye zile ambazo mnajua sio halali mana vyombo vya dola vitawashugulikia” amesema Meya Mwita.

Mbali na hilo ,Meya Mwita amewapongeza walimu kutokana na kujitoa kwao kuwafundisha wanafunzi licha ya changamoto mbalimbali wanazokutana nazo.

Amesema walimu wamekuwa na changamoto kadha wa kadha lakini bado wamekuwa wavumilivu ikiwemo  kuhakikisha  wanafunzi wanafanya vizuri katika masomo yao ambapo alitumia nafasi hiyo kuwataka wazazi, kamati za shule kutoa ushirikiano wa kutosha ili waweze kutimiza majukumu yao.

“ Naelewa kwamba zipo changamoto nyingi zinazo wakabili, lakini bado mnafanya kazi kwa moyo mmoja, kutokana na juhudi hizo nawapongeza sana, zile changamoto ambazo ninauwezo wakuzitatua tutashirikiana” amesema.

Katika hatua nyingine Meya Mwita ameahidi kuwachimbia kisima cha maji shuleni hapo ili kuondokana na changamoto ya kutumia gharama kubwa ya kununua maji jambo ambalo alielezwa wakati wa risala iliyosomwa na wanafunzi washule hilo.

Hata hivyo Mkuu wa shule hiyo Maria Abihudi amesema kuwa shule hiyo inachangamoto ya Umeme ambapo kwasasa upo katika jingo moja la walimu hivyo bado kusambazwa kwenye madarasa mengine ambapo Meya Mwita aliahidi kulishughulikia jambo hilo.

MBUNGE  wa Jimbo la Iringa Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mchungaji Peter Msigwa amefunguka na kusema kuwa katika Bunge ambalo linatarajiwa kuanza Novemba 7, 2017 anakusudia kupeleka hoja ya kumuondoa Spika wa Bunge, Job Ndugai

Msigwa amesema hayo leo kupitia moja ya mtandao wake wa kijamii na kusema kuwa kwa kuzingatia kanuni ya 137 ya kanuni za kudumu za Bunge atapeleka hoja yake hiyo ya kumuondoa Spika wa Bungue.

"Ninakusudia kupeleka hoja ya kumuondoa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Job Ndungai, kwa kuzingatia Kanuni ya 137 ya kanuni za kudumu za bunge ina complement ibara ya 84 (7) (d) ya Katiba" alisema Msigwa

Mbunge Peter Msigwa ni kati ya wabunge ambao wamekuwa wakilalamika kuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai amekuwa akiendesha bunge kwa shinikizo na upendeleo na kudai kuwa hastahili kuendelea kuongoza kiti hicho.

Chanzo .EATV

JIMBO  Katoliki la Tunduru Masasi limempoteza askofu wake, Castory Msemwa aliyefariki jana Alhamisi Oktoba 19,2017 saa saba mchana nchini Oman.

Kwa mujibu wa Makamu wa Askofu wa Jimbo Katoliki Tunduru Masasi, Padri Jordan Liviga, Askofu Msemwa amefariki dunia mjini Muscat akiwa safarini kwenda nchini India kwa matibabu.

Taarifa ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) imesema Askofu Msemwa alikuwa na tatizo la kiafya kwa kipindi cha miaka miwili na amekuwa akipata tiba na kuendelea na utume kama kawaida.

TEC imesema Askofu Msemwa aliondoka nchini Jumatano Oktoba 18,2017 kuelekea nchini India kwa matibabu kabla hajafariki dunia.

Padri Liviga amebainisha kuwa utaratibu wa kuuleta nchini mwili wa marehemu Askofu Msemwa Jumapili Oktoba 22,2017 unafanyika. Amesema taarifa zaidi za utaratibu wa mazishi zitatolewa baadaye.

Askofu Msemwa amezaliwa mwaka 1955 katika Kijiji cha Kitulira, Parokia ya Matola Jimbo Katoliki Njombe.

Alipata elimu ya msingi katika shule ya Motola, kisha sekondari katika Seminari Kuu ya Peramiho ambako alisomea Falsafa na Teolojia kati ya mwaka 1981 na 1987. Alipata daraja ya upadri Juni 7,1987. Amekuwa Paroko Msaidizi, kiongozi wa vijana parokiani jimboni Njombe, mwalimu na amesoma katika Chuo cha Teresianum Pontifical College for Spirituality huko Roma na kuhitimu mwaka 1996.

Alipata Daraja ya Uaskofu Januari 30,2005 kisha kusimikwa kuliongoza Jimbo Katoliki Tunduru Masasi Agosti 25,2005.

OFISA  mkuu mtendaji wa Tume ya Uchaguzi Nchini Kenya Ezra Chiloba anatarajiwa kuchukuwa likizo ya wiki tatu na hatoshiriki katika uchaguzi wa marejeo wa Alhamisi.

Kulingana na duru katika tume hiyo ya IEBC bwana Chiloba alifanya uamuzi huo wa kibinafsi wa kutoshiriki ili kujenga upya imani ya washikadau ambao wamelalamika kuhusu maafisa wa tume hiyo.

Afisa huyo amekuwa chini ya shinikizo kubwa kutoka muungano wa upinzani Nasa kujiuzulu, huku mgombea wa urais wa muungano huo Raila Odinga akiitisha maandamano ya kumlazimisha kuondoka pamoja na maafisa wengine ikiwatuhumu kwa kusimamia vibaya uchaguzi wa Agosti 8 ambapo rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi.

Matokeo ya uchaguzi huo hatahivyo yalifutiliwa mbali na mahakama ya juu ambayo iliamua kwamba haukufanyika kulingana na sheria.

Bwana Chiloba anachukua likizo baada ya mwenyekiti wa tume hiyo wafula Chebukati kutaka maafisa waliotajwa baada ya uchaguzi huo kufutiliwa mbali kung'atuka.

Mahakama ya juu ilisema kuwa haikupata ushahidi kuhusu makosa yaliofanywa na maafisa lakini wanasiasa wamelalamika na kuishutumu tume hiyo kwa kujaribu kufanya udanganyifu katika uchaguzi huo mbali na wizi wa kura.

Uamuzi huo wa kuchukua likizo ulijadiliwa na mwenyekiti na bwana Chiloba anaamini kwamba kutokuwepo kwake hakutaathiri maandalizi ya tume hiyo kusimamia uchaguzi ulio huru na haki .

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget