Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

November 2017

CHUO cha mchezo wa kareti  cha CHISHAKU kilichopo Gerezani Kariakoo Jijini Dar es Salaam, kimefungua rasmi shindano la 10  kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu cha Ardhi Mlimani leo.

Akizungumza na Raia Tanzania Online, Mkurugenzi na mkufunzi wa Chuo hicho Master Jimmy, amesema mchezo huo haupewi kipaumbele kama ilivyo michezo mingine hivyo kukosa Timu ya Taifa yenye ushindani.
Master Jimmy, amesema kuwa, lengo la kuwa na mashindano hayo ni pamoja na kutaka kufahamu uelewa wa wanafunzi hao  juu ya masomo yao.
Aidha, Master Jimmy, amesema kuwa shindano hilo sio  mara yake ya kwanza  kwani shindano hilo ni la kumi kufanyika na lilianza  mwaka 2007.
Hata hivyo, Master Jimmy , amesema kuwa mbali na kuwashindanisha wana lengo la kuwajengea uwezo na  ukakamavu pamoja na kujua mbinu za kujilinda katika kutenegeneza Vijana kuwa wazalendo wa  Taifa lao.
“Tumeamua kuwa na mashindano haya kila mwaka lengo ni kujua mafunzo kama yameeleweka vizuri pamoja na  kuwajengea uwezo binafsi wa kujilinda na kutengeneza furaha miongoni mwa Wazazi na watoto ili kuwafundisha jinsi ya kuishi pamoja na kujenge urafiki ulio na amani”. Amesema Master Jimmy

Naye Mgeni rasmi ambaye ni Mhariri Mkuu wa Habari Gazeti la Raia Tanzania kutoka TSN Media , Moris Lyimo, amesema ni zamu ya Serikali kupitia upya sheria ya JKT nakuwaingiza watoto hao katika mfumo rasmi utakao wapa fursa ya kuajiriwa na kujiajiri kuliko ilivyo sasa.
“Serikali inapaswa kuwaangalia watoto hawa, kama waliweza kuingiza uhamiaji kwenye sekta rasmi basi iwe na jukumu la kulinda vipaji hivi na sio kuvitumia kipindi cha matukio na kuwaacha kwani wakilelewa vizuri naamini tutapata Vijana safi wenye uzalendo wa kweli watao wakilisha Vyema Taifa letu kama michezo mingine “ Amesema Lyimo

Mbali na washindi wa medali , wapo walioibuka na ushindi wa jumla ambapo kundi C waliibuka kinara kwa kupata alama 1016, mshindi wa pili kundi G wakiambuilia alama 903 wakati mshindi wa tatu akitokea kundi E kwa alama 750

Chuo hicho  kipo kwenye mpango wa kuandaa tuzo za washindi wa  Belt mbali mbali kama Vile Yellow Belt, White Belt, Orange Belt, Green Belt, Blue Belt, shindano hilo  linatarajia kufanyika February mwaka 2018.

Picha Na 2Na Greyson Mwase, Dar es Salaam
Novemba 28, 2017
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amesema kuwa kata za Kigamboni, Vijibweni, Tungi zinatarajiwa kupata umeme wa uhakika  kufuatia kukamilika kwa mradi wa upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Kigamboni kilichopo jijini Dar es Salaam.
Waziri Mgalu aliyasema hayo  tarehe 27 Novemba, 2017 kwenye ziara yake katika kituo cha kupoza umeme Kigamboni na katika mikutano ya hadhara aliyoifanya katika kata za Kisiju na Mkamba zilizopo wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
Alisema kituo hicho kitakuwa na uwezo wa kuhudumia wateja kutoka 6,000 hadi 12,000 na kuongeza kuwa Serikali kupitia  Wizara ya Nishati  itahakikisha  vituo vingine vya kuboresha  hali ya umeme ndani ya jiji la  Dar es Salaam  vinakamilika mapema Desemba 15, 2017 na kuondoa  tatizo la  kukatika kwa umeme mara kwa mara lililokuwa linajitokeza.
Aidha, alilitaka  Shirika la Umeme  Tanzania (TANESCO) kukamilisha vituo  vingine  vilivyobaki vya Kurasini, Gongo la Mboto na Mbagala mapema ili wakazi wa jiji la Dar es Salaam waweze kuondokana na  tatizo la ukosefu wa umeme.
Katika hatua nyingine, Mgalu aliwataka wandarasi waliopewa kazi ya kujenga miundombinu ya kusambaza umeme vijijini kupitia Wakala wa Nishati  Vijijini (REA) kukamilisha miradi mapema na kuongeza kuwa  Serikali haitamvumilia mkandarasi atakayezembea ukamilishwaji  wa mradi wake.
“ Wananchi wanahitaji umeme wa uhakika na kwa gharama nafuu, umeme ndio uchumi wa nchi na kama Wizara ya Nishati  tupo kwa ajili ya kuhakikisha  uchumi  wa viwanda unakua kwa kuhakikisha nishati ya umeme ya uhakika inapatikana sehemu zote hasa vijijini,” alisisitiza  Mgalu
Vilevile, Mgalu aliitaka REA kuainisha vipaumbele katika usambazaji wa umeme vijijini, kipaumbele kikiwa ni vijiji  vyenye wakazi wengi na taasisi kama hospitali, makanisa na misikiti.
Akizungumzia suala la fidia kwa wakazi wanaopisha  ujenzi wa miundombiniu ya umeme unaosimamiwa na  REA, Naibu Waziri Mgalu alisema hakuna fidia kwa kuwa serikali imekwishagharamia gharama zote na kinachohitajika kwa wananchi ni kulipia gharama za Kodi (VAT) ambayo ni shilingi 27,000.
Aliwataka wakazi wa Kata za Kisiju na Mkamba wilayani Mkuranga kutandaza mifumo ya nyaya (wiring) kwenye nyumba zao au kununua kifaa maalum cha Umeme Tayari (UMETA) mapema kwa ajili ya kujiandaa na huduma ya umeme.
Akielezea mikakati ya Serikali katika kuhakikisha umeme unapatikana hususan katika wilaya ya Mkuranga yenye viwanda vingi, Naibu Waziri Mgalu alisema Serikali inatarajia kujenga  kituo cha kuzalisha umeme  kwa kutumia gesi Somanga Fungu na  kusambaza gesi nyingine kwenye viwanda vitakavyohitaji.
Aliongeza kuwa Serikali inatarajia kuanza ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji wa Stieglers Gorge utakaokuwa na uwezo wa kuzalisha Megawati 2,100 na kukamilisha miradi ya Kinyerezi II na Kinyerezi III
Alisema kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2020 Megawati 5,000 zinapatikana na nchi kuingia kwenye uchumi wa viwanda utakaozalisha ajira kwa vijana hususan kwa vijana waishio  vijijini.
“ Tunataka mazao  yasindikwe vijijini na kusafirishwa ndani na nje ya nchi yakiwa kama  bidhaa, tunataka mtumie  fursa ya umeme kwa ajili ya uchumi wa viwanda badala ya matumizi ya majumbani tu,” alisema Mgalu.
Naye Mbunge wa Mkuranga ambaye ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalah Ulega alimshukuru Naibu Waziri Mgalu kwa ziara yake katika wilaya ya Mkuranga na kuongeza kuwa wananchi wana matumaini makubwa ya umeme wa uhakika kwani wilaya  hiyo imekuwa na changamoto ya ukosefu wa umeme kwa muda mrefu.

Wanajeshi wakijiandaa kwa sherehe ya kuapishwa kwa rais Uhuru Kenyatta katika uwanja wa michezo wa Kasarani NairobiHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWanajeshi wakijiandaa kwa sherehe ya kuapishwa kwa rais Uhuru Kenyatta katika uwanja wa michezo wa Kasarani Nairobi
USALAMA umeimarishwa katika mji mkuu wa Kenya Nairobi wakati wa siku ambayo rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuapishwa kwa awamu ya pili ya urais.
Takriban viongozi 13 wa mataifa tofauti wanatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo.
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga ambaye alisusia marudio ya uchaguzi ameitisha kufanyika kwa mkutano wa upinzani licha ya mkutano huyo kupigwa marufuku.
Uchaguzi wa mwezi Agosti ulifutiliwa mbali na mahakama kutokana na kile kilitajwa kuwa uchaguzi usio huru na haki.
Marudio ya uchaguzi wa Oktoba 26 ulimpatia Uhuru Kenyatta asilimia 98 ya kura huku waliojitokeza kushiriki katika shughuli hiyo wakiwa asilimia 39.
Sherehe hiyo ya siku ya Jumanne inayofanyika katika uwanja wa michezo wa Kasarani jijini Nairobi inatarajiwa kuanza mwenzo wa saa nne.
Waandalizi wanatarajia watu 60,000 kujaza uwanja huo huku skrini kubwa zikiwa zimewekwa nje ya uwanja huo kwa wale watakaoshindwa kuingia.
Rais Kenyatta anakabiliwa na wakati mgumu wa kuliunganisha taifa hiloHaki miliki ya pichaEPA
Image captionRais Kenyatta anakabiliwa na wakati mgumu wa kuliunganisha taifa hilo
Baadhi ya watumbuizaji wanaotarajiwa kuhudhuria sherehe hiyoHaki miliki ya pichaAFP
Image captionBaadhi ya watumbuizaji wa kabila la Maasai wanaotarajiwa kuhudhuria sherehe hiyo
Naibu wa rais William Ruto, pia ataapishwa.
Miongoni mwa viongozi wa kigeni wanaotarajiwa ni waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, rais wa Uganda, Yoweri Museveni na rais wa Rwanda Paul Kagame.
Upinzani nchini humo umewataka wafuasi wake kususia sherehe hiyo na badala yake kukusanyika katika mkutano ili kuwakumbuka wafuasi waliouawa katika ghasia tangu uchaguzi wa mwezi Agosti.
Upinzani ulikabiliana na Polisi baada ya uchaguzi wa Agosti 8Haki miliki ya pichaEPA
Image captionUpinzani ulikabiliana na Polisi baada ya uchaguzi wa Agosti 8
Maafisa wapolisi wameonya upinzani huo dhidi ya kufanya mkutano huo.
CHANZO BBC NEWS


Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete amesikitika kutohudhuria kuapishwa kwa Rais mteule wa Kenya na kusema alipata mwaliko kuhudhuria sherehe za kuapishwa Kenyatta lakini ameshindwa kutokana na kuingiliana kwa majukumu.

Leo baadhi ya mitandao ya kijamii nchini Kenya alidai kuwa Rais mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete ni mmoja wa wageni ambao wamehudhuria sherehe za kuapishwa kwa Uhuru Kenyatta jambo ambalo Jakaya Kikwete amelipinga kwa kusema ameshindwa kwenda Kenya kutokana na majukumu kuingiliana.

Jakaya Kikwete ametumia mtandao wake wa Twitter kufikisha ujumbe wake wa pongezi kwa Kenyatta kuchaguliwa tena kuongoza nchi ya Kenya ambayo ni nchi rafiki na Tanzania kwa miaka mingi sasa.

"Nakupongeza Rais UKenyatta kwa kuchaguliwa tena kuongoza nchi rafiki ya Kenya. Nakushukuru kwa mwaliko wa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwako. Nasikitika sitaweza kuhudhuria kutokana na kuingiliana kwa majukumu. Nakutakia kila la kheri katika awamu yako ijayo" alindika Kikwete

Rais Uhuru Kenyatta alichaguliwa kuwa Rais kwa Kenya katika uchaguzi wa marudio uliofanyika Oktoba 26, 2017


MAMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo asubuhi tarehe 28 Novemba, 2017 amewasili Mjini Nairobi nchini Kenya ambako anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba amepokelewa na Mhe. Balozi Robinson Njeru Githae wa Kenya na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. Pindi Chana.

Sherehe za kuapishwa kwa Mhe. Rais Uhuru Kenyatta zinafanyika katika uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Nairobi
28 Novemba, 2017aki miliki ya picha

Ndugu waandishi wa habari: Nimeshikwa na mshtuko, simanzi baada ya kusambaa kwa  taarifa ambazo naweza kusema kuwa ni za uzushi kwamba  ninampango wa kujiondoa ndani ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema. naomba taarifa hizo zipuuzwe manahazina ukweli wowote na kwamba zinampango wa kunichafua mimi pamoja na Chama Changu.
Image result for mwita isaya akiwa katika kampeni
Ndugu wandishi wa habari : Napenda ieleweke kuwa  sijawahi kudhani wala kufikiria kuhama Chadema na kwenda kwenye chama chochote kile cha siasa. Chadema ni chama ambacho nimetoka nacho mbali tangu mwaka 2004 hadi leo, nimejenga chama kwa gaharama zangu mwenyewe.

Ndugu waandishi wa habari: Leo nimekuwa Meya wa jiji la Dar es Salaam kupitia Chama Changu cha Chadema,natambua kuwa  chama kimeniheshimu sana kwa kunipa nafasi hii hivyo sina sababu ya kuondoka kwani  ninania ya kuwatumikia Wananchi ambao wameniamini na wamenichagua kwa mapenzi yao wakiamini kuwa nitawaletea Maendeleo nikiwa ndani ya Chama Cha Chadema.

Nafahamu  tuhuma hizi zinatokana na aina ya utendaji wangu katika Jiji la Dar es Salaam kwani nimekuwa nikifanya kazi badala ya kupambana na serikali pale ambapo watu wanaamini kuwa mambo hayajaenda sawa.

Ndugu waandishi wa habari:  Kukaa kwangu kimya huku ,kutokufanya siasa za kiharakati ndani ya jiji la Dar es Salaam  haimanishi kwamba nipo upande wowote ama kukihujumu chama changu. Ila huu ni mfumo ambao nimeuchagua na kujijengea kwa ajili ya kuwatumikia wananchi nasio kufanya harakati za kisiasa kwakuwa nina  nia  ya kufanya maendeleo ndani ya jiji la Dar  es Salaam.

Ndugu waandishi wahabari: Naomba ifahamike kuwa hakuna Mkurya ambaye aliwahi kuwa msaliti,katika nafasi yoyote ambayo aliwahi kuwa nayo. Kutokana historia hiyo, naomba niaminike na wanachama na wananchi wote kuwa haitakuja kutokea Mkurya mimi nikakisaliti chama changu.

Nakama  itakuja kutokea nikafanya hivyo ninaweza kuhatarisha maisha yangu, Familia yangu, na hivyo kujikuta nikaingia kwenye matatizo makubwa ambayo kimsingi sio mazuri. Mama yangu ni mjane, kama itafanya hivyo Chadema wote Mkoa wa Mara hawawezi kuwaacha ndugu zangu salama .

Ndugu waandishi wa habari : Tangu nimeona watu wote waliohama ,kusaliti vyama vyao, maisha yao yamekuwa mabaya, nahata imani kwa Wananchi wao imepungua. Hivyo na Mimi  sitaki kuwa kama wao, ninania ya dhati ya kukitumikia chama changu kwa uaminifu mkubwa kama ambavyo wao wameniamini.

Kuliko kuhama Chadema ni heri mkanitafutie Mahala pengine pakuishi ambapo itakuwa ni mbinguni lakini sio hapa duniani ama kwenda kwenye Chama kingine chochote  cha kisisasa.  Kikubwa napenda kuwaeleza wana chama wote wa Chadema kuwa hivi sasa kila mmoja  tujielekeze kwa nguvu zetu zote kwenye kampeni hivi za uchaguzi mdogo wa madiwani unaotarajiwa kufanyika Novemba 26 mwaka huu.msikubali kutolewa kwenye maandalizi ya uchaguzi.

TAUSI  Entertainments & Talents ni miongoni mwa Kampuni ya Kitanzania iliyoanzishwa  Mei, 2016 huko Zanzibar ikiwa na lengo la kusaidia Vijana wa Kitanzania katika kukuza  tasnia ya muziki.
Akizungumza na Raia Tanzania, Mkurugenzi wa Kampuni ya Tausi Entertainment & Talent , Tausi Omary Mohamed , amesema lengo la kuanzisha kampuni hiyo,  kumetokana na kutaka kusaidia tasnia ya muziki kwa wale watakao kuwa na uhitaji  na wenye uwezo ambao kampuni yake itakuwatayari kufanya nao kazi.

Mkurugenzi Tausi Omary Mohamed
Aidha, Tausi, amesema kuwa kampuni hiyo ilianzishwa ikiwa na wasanii watatu, hadi kufikia Julai mwaka 2017, ilibakiwa na msanii mmoja Chidy Grenade , hivyo aliamua kumsaninisha mwengine Oktoba , 2017 ambaye  ni Sharara Tz kutoka Dar es Salaam.

Image result for Chidy Grenade
Miongoni mwa wasanii maarufu waliokuwa wakimilikiwa na Tausi Entertainment & Talent  ni pamoja na  Sultan King pamoja na Berry Black ambapo kwa sasa hawako tena  kwenye kampuni hiyo.
Image may contain: 1 person
Mbali na kujihusisha na maswala ya muziki lakini kampuni hiyo imeanzisha program ya Tausi Entertanment Search ikiwa na lengo la kusaka vipaji kama vile vichekesho, uimbaji pamoja na ku dansi (shake).
Image result for Sharara Tz

Programu hiyo ya Talent Search inafanyika mara moja kila mwaka huku pambano jengine likitarajiwa kufanyika mwakani Agosti 2018 Zanzibar.

“ Mimi sikuanzisha kampuni kwa ajili ya kushindana, najua zipo kampuni nyingi zinazosimamia wasanii, lakini lengo ni kusaidia Vijana hususani Zanzibar katika kuwapatia ajira ,na kufikia malengo yangu, hata kama zitaongezeka siku hadi siku sina shida maana kila mtu ana malengo yake.”Amesema  Tausi





Huyu ni mwanamke aliyethubutu kutoa alichonacho na kuona wengine wakinufaika nacho, lakini aliendelea kushikilia msimamo wake wa kuhamisha Tausi Talent Search Dar es Salaam baada ya kukamilisha mipango yake.

Miongoni mwa mafanikio aliyoyapata ni pamoja na kuwa na Mnyororo mkubwa wa watu wanaosaidiana katika kufikia malengo yake kama vile mitandao ikiwamo TV, Magazine  na Redio

Kuhusu kuchukua wasanii mkubwa na wanae, amesema lengo lake ni kutaka kushirikiana nae pale atakapo wahitaji wasanii hao kufanya nao kazi na wala sio kuwaiba.

Hivi sasa yupo katika mpango wa kuhakikisha anakuwa na Vijana wenye vipaji wengi watakao weza kuutangaza vema muziki wa Tanzania kimataifa kama ilivyo kwa wasanii wengine kama viele Ali Kiba na Diamond wanaoonekana kuliteka soko la Afrika Mashariki kwa sasa.


Aidha, Mkurugenzi Tausi amesema kuwa Vijana  wanaochipukia wasiwe na haraka ya kuwa star wanatakiwa wafanye kazi  zenye ubora na wawe na nidhamu na subira katika kufikia malengo. 

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget