Image result for MEYA WA JIJI LA DAR MWITA
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ,aliyesimama, kulia ni Mkurugenzi wa jiji Sipora Liana,  kushoto ni Naibu Meya wa jiji Mussa Kafana
MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam , Isaya Mwita leo amewasilisha mpango wa bajeti wa mwaka 2018 hadi 2019 ambapo jumla ya shilingi bilioni 75.2 zitatumika kwa mwaka huo.

Hata hivyo mpango huo umepitishwa kwa kauli moja na Madiwani wote wa halmashauri hiyo huku wakimpongeza kwa  kusema kuwa jiji limepata Meya anayejali maslahi ya maendeleo katika halmashauri hiyo.

 Halmashauri hiyo imeandaa mpango huo kwa kuzingatia taratibu zinazotakiwa kufuatwa na mamlaka za Serikali za mitaa katika utayarishaji wa makadirio ya mapato na matumizi ya  mwaka wa fedha wa 2018 na 2019.

Akizungumzia  mpango huo kwenye mabaraza la Madiwani na waandishi wahabari , Meya Mwita amesema kuwa jiji limekadiria kukusanya na kutumia shilingi bilioni 75.2 ambapo itatokana kwenye  vyanzo mbalimbali vya mapato ikiwemo bilioni 18.1 zinatarajiwa kukusanywa kutoka kwenye vyanzo vya vyandani.

Aidha amefafanua kuwa mapato mengine  yatapatikana kutokana na halmashauri kubuni vyanzo vingine vya mapato sambamba na kuboresha mikakati ya ukusanyaji wa mapato.

Amefafanua kuwa utekelezaji wa bajeti hiyo umelenga kutekelaza mradi wa ujenzi wa kituo cha mabasi cha Mbezi Luis,kuboresha miundombinu ya Dampo,ujenzi wa vyoo vya Umma na kuhakikisha utoaji wa huduma usiokua na usumbufu kwa wananchi.

 Amesema halmashauri pia imepanga kutumia asilimia 65 ya mapato  ya ndani sawa na shilingi bilioni 11.7 kwa ajili ya kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo ,shilingi bilioni 1.08 zitatumika kwa ajili ya mfuko wa wanawake ,vijana na walemavu.

Akizungumzia suala la utalii ,Meya Mwita amesema kuwa katika bajeti hiyo  zaidi ya bilioni mbili zimetengwa ili kuboresha sekta ya hiyo ikiwemo kununua mabasi ,kutengeneza na kuboresha vivutio mbalimbali vilipo jijini hapa.

Ameongeza kua kuboreshwa kwa sekta hiyo kutaongezea pato la Taifa  pamoja na kutoa ajira kwa vijana waliosomea masuala ya utalii ambao kwa kiasi kikuba hawana ajira.

“ Kama jiji la Dar es Salaam tumeona ni wakati muafaka sasa wakuweka nguvu kwenye sekta ya utalii, ambayo kwa kiasi kikubwa kitakuwa ni kivutio kwa wageni kuja hapa ,maanye ni kwamba jiji litapata fedha nyingi kupitia mpango huo” amesema Meya Mwita.

Imetolewa leo Februali 24

Na Christina Mwagala Afisa habari Ofisi ya Meya wa jiji.