Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Articles by "Kimataifa"

Iran,US nuclear dealRis wa Iran, Hassan Rouhani, amesema kwamba endapo rais Trump atafanikiwa kusitisha makubaliano ya mpamgo wa nuklia na Tehran, Marekani itambue wazi itakabiliwa na "majuto ya kihistoria"
Tamko hilo la rais Rouhani, lililotolewa kwenye runinga, limekuja wakati waziri wa masuala wa nchi za nje wa Uingereza wa kigeni, Boris Johnson, amekwenda mjini Washington kama sehemu ya jitihada za kumshawishi rais Trump na utawala wake wasiutelekeze mpango wa nyuklia.
Tarehe ya mwisho ya kutoa maamuzi kwa serikali ya Marekani juu ya Iran inatarajiwa kufikia ukingoni wiki moja ijayo.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani alisema rais wa Marekani amesisitiza ahadi yake ya kuhakikisha kwamba Iran haipati kamwe silaha ya nyuklia. Na katika siku za hivi karibuni, Rais Trump alimweleza rais wa Ufaransa aliyekuwa ziarani na viongozi wa Ujerumani kwamba anaamini makubaliano ya kimataifa ya kukabiliana na mpango wa nyuklia wa Iran ulikuwa mzuri sana.
Wakati wote Korea Kaskazini imekuwa ikiikosoa Marekani , lakini kumekuwa na mashambulizi machache katika wiki za hivi karibuni, wakati wa mipango ya Rais Trump kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un.
Taarifa hii ya karibuni ni kama tahadhari ya kuwa majadiliano kati ya nchi hizo mbili hayatakuwa rahisi.Wakati huo huo Korea ya Kaskazini imeishutumu Marekani kwa uchochezi wa makusudi dhidi ya Pyongyang kwa kutoa ushauri wa vikwazo havitaondolewa mpaka hapo itakapondoa silaha zake za nyuklia.
Wakati huo huo Korea ya Kaskazini imeishutumu Marekani kwa uchochezi wa makusudi dhidi ya Pyongyang kwa kutoa ushauri wa vikwazo havitaondolewa mpaka hapo itakapondoa silaha zake za nyuklia.
Wakati wote Korea Kaskazini imekuwa ikiikosoa Marekani , lakini kumekuwa na mashambulizi machache katika wiki za hivi karibuni, wakati wa mipango ya Rais Trump kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un.
Taarifa hii ya karibuni ni kama tahadhari ya kuwa majadiliano kati ya nchi hizo mbili hayatakuwa rahisi.
CHANZO BBC NEWS

Picha ni Prepetua Martine ambae ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake wa Basihaya.
Khadija Mahamba Dar es salaam.

Licha ya serikali na wanaharakati mbalimbali kupinga vikali unyanyasaji wa watoto lakini bado tatizo hili linaonekana kutokoma katika baadhi ya maeneo ikiwemo Chasimba bunju jijini Dar es salaam

Akiongea na habari 24 Bi. Prepetua Martine ambae ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake wa Basihaya na makamu mwenyekiti wa  jukwaa hilo kwa kata ya Bunju amesema unyanyasaji wa watoto na malezi mabovu ya kulala chumba kimoja wazazi na watoto wao  kwa baadhi ya wazaza wa mtaa wa Chasimba yamekuwa ni changamoto kubwa katika mtaa huo.

Aidha ameongeza kuwa  ni vyema kila mtu  akawa mlinzi wa mwenzake dhidi ya matendo maovu yatayofanywa na jirani yake  ili kunusuru tatizo hilo ambalo limeshika kasi katika mtaa huo.
Mazingira halisi ya wakazi wa eneo la Chasimba Bunju jijini Dar es salaam.
Pia ametoa wito  kwa wananchi wa mtaa huo kutokaa kimya pindi waonapo matatizo ya unyanyasaji au tukio lolote ambalo ni uvunjifu wa sheria kwani kwa kukaa kimya kwao kutafanya watu kutobadilika na kuendeleza unyanyasaji.

Pia amewataka wazazi kuhakikisha  kila mtoto apelekwe Shule kwa mujibu wa sheria za nchi na kwa kipindi hiki ambacho mh. rais magufuli amejitolea kufanya elimu iwe bure.

 Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa akishtakiwa kwa kesi mbili.

Katika kesi moja anadaiwa kuchoma moto nyumba ya Mary Tesha aliyokuwa akiishi Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Alphonce Muyinga.

Mchungaji Msigwa ambaye ni mshtakiwa wa saba katika kesi zote mbili amefikishwa mahakamani leo Jumatano Januari 24,2018 baada ya kuripoti kituo kikuu cha Polisi.

Katika kesi hiyo namba 6 ya mwaka 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, David Ngunyale, Wakili wa Serikali, Felix Chakla amedai kati ya Januari 5 na 14,2018  washtakiwa walipanga njama za kuharibu mali.

Pia wanadaiwa Januari 15,2018 walibomoa nyumba ya Anjelus Mbogo aliyekuwa diwani wa Mwangata aliyejiuzulu kutoka Chadema na kuhamia CCM.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema Iringa Mjini, Leonce Marto; diwani mteule wa Viti Maalumu, Rehema Mbeta na Patrick Madati.

Mchungaji Msigwa na wenzake wako nje kwa dhamana baada ya kila mmoja kusaini bondi ya Sh2 milioni.

Katika kesi ya pili, Mchungaji Msigwa na wenzake sita wanadaiwa kupanga njama ya kutenda uhalifu kinyume cha sheria.

Wakili Chakla mbele ya hakimu Ngunyale amedai Januari 17,2018  washtakiwa kwa pamoja walichoma nyumba ya Tesha aliyokuwa akiishi Muyinga.

Kwa shauri hilo namba 7 la mwaka 2018, washtakiwa wanadaiwa Januari 17,2018 waliichoma moto nyumba hiyo iliyopo kata ya Kihesa katika Manispaa ya Iringa.

Washtakiwa walikana kosa na hakimu  Ngunyale aliwaachia kwa dhamana baada ya kila mmoja kudhaminiwa na wadhamini wawili waliosaini bondi ya Sh3 milioni.

Mchungaji Msigwa na wenzake katika kesi hizo wanawakilishwa na wakili wa kujitegemea Anthony Rutebuka. Hakimu Ngunyale ameahirisha kesi hizo hadi Februari 2,2018

Swara hukaribia reli nyakati za usiku kulamba chuma za reli wakitafuta virutubishi muhimu vya mwili.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionSwara hukaribia reli nyakati za usiku kulamba chuma za reli wakitafuta virutubishi muhimu vya mwili.
Watafiti nchini Japana wameiwekea treni kipasa sauti ambacho kinabweka kama mbwa na kutoa mlio wa swara ili kuzuia treni kugonga swara njiani.
Gazeti la Asahi Shimbun lilisema kuwa sauti hizo zinatumiwa kuwafukuza swara kutoka kwa reli kwa lengo la kupunguza idadi ya wanaogongwa na kuuawa na treni.
Maafisa kutoka kwa taasisi ya reli wanasema kuwa mlio wa sekunde tatu wa swara humfanya swara kuwa makini na kusikiliza, ukifuatiwa na sekunde 20 za mbweko wa mbwa, inaweza kusababisha swara kukimbia.
Watafiti wanasema kuwa majaribio ya usiku wakati swara wanakusanyika kando ya reli yanesababisha swara hao kupungua.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionWatafiti wanasema kuwa majaribio ya usiku wakati swara wanakusanyika kando ya reli yanesababisha swara hao kupungua.
Watafiti wanasema kuwa majaribio ya usiku wakati swara wanakusanyika kando ya reli yamesababisha swara hao kupungua.
Swara hukaribia reli nyakati za usiku kulamba chuma za reli wakitafuta virutubishi muhimu vya madini ya mwili.
Wizara ya uchukuzi nchini Japan inasema kuwa kulikuwa na visa 613 vya treni kugonga swara na wanyama wengine mwaka 2016.
Treni zingine huunda kuwa na sura ya mbwaHaki miliki ya pichaWIKIMEDIA/KANSAI EXPLORER
Image captionTreni zingine huunda kuwa na sura ya mbwa

Viongozi wa Korea kaskazini na kusini walipokutanaKOREA kusini imesema itashughulika na Korea kaskazini kwa kile alichokiita '' Macho ya wazi'' baada ya kukamilika mpango wa kuweka timu moja ya pamoja katika michezo ya majira ya baridi ya Olympics inayofanyika mwezi ujao.
Akizungumza na BBC Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Korea kusini Kang Kyung-wha amesema licha ya makubaliano yaliyopo, dhumuni kubwa linabaki kuwekwa vikwanzo kushughulika na vitisho vya nyuklia.
Amesema mkutano uliojumuisha nchi 20, ambao umefanyika katika mji wa Vancouver ulikuwa ukihusu jinsi bora ya kuweka vikwazo hivyo. Lakini pia amezingatia mahitaji ya kibinadamu kwa watu wa Korea kaskazini.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Korea Kusini Kyang Kyung-what ameupongeza ushirikiano huo kati ya nchi yake na kaskazini.
Amesema pia anataka kuona misaada ya kibinadamu ikipelekwa Korea kaskazini.
Katika hatua nyingine, Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Marekani Rex Tillerson, amesema nchi yake na washirika wao ikiwemo China, haijawahi wakaunganika pamoja kama sasa dhidi ya kitisho cha nyuklia kilichowekwa na Korea kaskazini.
CHANZO BBC NEWS

Stock image of a close up of schoolgirl typing text message on a mobile phone at a desk in aclassroomHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMkuu wa polisi amesema kwamba mashtaka yaliwekwa kama onyo kwa vijana wengine wanaosmabasza picha za ngono
Zaidi ya vijana 1,000 wameshtakiwa na polisi Denmark kwa kusambaza. picha na video za ngono
Wameshitakiwa kwa kutumia mtandao wa jamii wa Facebook Messenger kusambaza vipande vya video vilivyoonesha vijana wawili wenye miaka 15 wakifanya mapenzi.
Polisi wamesema kwa sababu vijana hao walikuwa wenye umri chini ya miaka 18, mashtaka yawaweza ongezeka hadi kosa la kusambaza picha zisizo ma maadili ya watoto.
Kampuni ya Facebook iiliwataarifu mamlaka wa Marekani ambao wakawatoa taarifa kwa polisi Denmark.
Kama wakipatikana na hatia ya kusambaza picha zisizo na maadili kwa watoto, watawekwa kwenye orodha ya wadhalilishaji ya watoto kingono kwa miaka 10.
Vijana elfu moja na nne wanamashtaka nchi nzima ikiwa ni baada ya kusambaza picha na video kwa kutumia app hiyo ya kutuma ujumbe mwishoni wa mwaka jana.
Baadhi ya watuhumiwa wenye umri juu ya miaka 18 waliitwa katika vituo vya polisi kuhojiwa.
Watuhumiwa chini ya miaka 18 wapatikana kupitia wazazi wao.
Mkuu wa polisi wa Denmark amesema mashitaka hayo yanakuja kama onyo kwa vijana kuthubutu kutuma video za ngono.
Yeyote atakayepatwa na hatia na mashtaka hayo anaweza kupata kifungo cha siku 20.
Kumekuwa na wito kwa serikali ya Denmark kuchukua hatua zaidi kuzuia picha za ngono ili kulipa kisasi.
CHANZO BBC NEWS

David Allen Turpin (left) and Louise Anna TurpinHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWazazi  David Allen Turpin, 57, na Louise Anna Turpin, 49, walikamatwa kwa mashtaka ya mateso na kuhatarisha maisha ya watoto.
WAZAZI  wawili wamekamatwa huko California baada ya polisi kupata watu 13 waliokuwa wameshikiliwa mateka nyumbani kwao wakiwemo wengine waliofungiwa kwenye vitanda vyao kwa minyororo na makufuli.
David Allen Turpin, 57, na Louise Anna Turpin, 49, walikamatwa kwa tuhuma za mateso na kuhatarisha maisha ya watoto.
Watu hao 13 walio na umri wa kati ya miaka miwili na 29, walipatikana kwenye nyumba eneo la Perris kilomita 95 kusini mashariki mwa Los Angeles.
Maafisa waligundua hilo Jumapili wakati mmoja wa watoto hao alifanikiwa kuponyokana na kupiga namba ya dharura akitumia simu ambayo alipata ndani ya nyumba.
Msichana huyo ambaye polisi wanasema alionekana kuwa na umri wa miaka 10, alidai kuwa ndugu zake wengine 12 walikuwa wakishikiliwa na wazazi wao.
Picha zinonyesha familia iliyo na sare na yenye furahaHaki miliki ya pichaDAVID-LOUISE TURPIN/FACEBOOK
Image captionPicha zinonyesha familia iliyo na sare na yenye furaha
Polisi baadaye walipata watoto kadhaa wakiwa wamefungiwa kwenye vitanda vyao kwa nyororo na makufuli gizani katika mazingira yenye harufu mbaya.
Lakini wazazi hawakuweza kutoa sababu ni kwa nini watoto hao walifungwa kwa njia kama hiyo.
Polisi walishangazwa kugundua kuwa saba kati ya wale waliokuwa wakizuiliwa kwenye nyumba hiyo walikuwa ni watu wazima wa kati ya umri wa miaka 18 na 29.
Waathirirwa walioneka kudhoofika kiafya na wachafu.
Waathiriwa hao wote kwa sasa wanatibiwa kwenye hospitali za eneo hilo kulingana na rekodi, wazazi hao waliishi Texas kwa miaka mingi kabla ya kuhamia California.
Turbin anatajwa kuwa alikuwa na kazi nzuri kama mhandisi kwenye kampuni ya ndege na teknolojia ya ulinzi ya Northrop Grumman.
Hata hivyo kutokana na kuwa na watoto wengi na mke wake kutokuwa na kazi, matumizi yake yalizidi kipato chake na mara mbili alitangazwa kufilisika.
Kwenye tovuti ya elimu ya California Turpin anatajwa kuwa mkuu wa shule ya Sandcastle, ambayo ni shule ya kibinafsi iliyo nje ya nyumba yake.
Shule hiyo ilifunguliwa mwezi Machi mwaka 2011, kwa mujibu wa mtandao huo. Watoto sita walijiunga na shule hiyo katika viwango tofauti.
Wazazi wake Turpin walisema kuwa wajukuu wao walisomea nyumbani lakini hawajaiona familia hiyo kwa miaka minne au mitano.
CHANZO BBC NEWS

Miili ya askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliouawa na waasi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) inarejeshwa nchini leo.

Taarifa ya ofisi ya habari ya JWTZ imesema miili ya askari hao itawasili nchini leo Jumatatu Desemba 11,2017 saa kumi na mbili jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Awali, akizungumzia na waandishi wa habari jana Jumapili Desemba 10, 2017 Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali James Mwakibolwa alisema miili ya askari hao ingerejeshwa nchini kati ya Jumanne Desemba 12, au Jumatano Desemba 13,2017 kwa ushirikiano kati ya Serikali na Umoja wa Mataifa (UN).

Mwakibolwa alisema askari hao walivamiwa kambini na waasi wa ADF na mapigano yalidumu kwa takriban saa 13. Alisema askari 14 wa JWTZ waliuawa, 44 wamejeruhiwa na wengine wawili  hawajulikani walipo.

Alisema tukio hilo lililotokea Desemba 7,2017 katika kambi ndogo iliyopo katika daraja la Mto Simulike, kaskazini mashariki mwa Wilaya ya Beni, Jimbo la Kivu nchini DRC.

Wanajeshi wakijiandaa kwa sherehe ya kuapishwa kwa rais Uhuru Kenyatta katika uwanja wa michezo wa Kasarani NairobiHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWanajeshi wakijiandaa kwa sherehe ya kuapishwa kwa rais Uhuru Kenyatta katika uwanja wa michezo wa Kasarani Nairobi
USALAMA umeimarishwa katika mji mkuu wa Kenya Nairobi wakati wa siku ambayo rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuapishwa kwa awamu ya pili ya urais.
Takriban viongozi 13 wa mataifa tofauti wanatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo.
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga ambaye alisusia marudio ya uchaguzi ameitisha kufanyika kwa mkutano wa upinzani licha ya mkutano huyo kupigwa marufuku.
Uchaguzi wa mwezi Agosti ulifutiliwa mbali na mahakama kutokana na kile kilitajwa kuwa uchaguzi usio huru na haki.
Marudio ya uchaguzi wa Oktoba 26 ulimpatia Uhuru Kenyatta asilimia 98 ya kura huku waliojitokeza kushiriki katika shughuli hiyo wakiwa asilimia 39.
Sherehe hiyo ya siku ya Jumanne inayofanyika katika uwanja wa michezo wa Kasarani jijini Nairobi inatarajiwa kuanza mwenzo wa saa nne.
Waandalizi wanatarajia watu 60,000 kujaza uwanja huo huku skrini kubwa zikiwa zimewekwa nje ya uwanja huo kwa wale watakaoshindwa kuingia.
Rais Kenyatta anakabiliwa na wakati mgumu wa kuliunganisha taifa hiloHaki miliki ya pichaEPA
Image captionRais Kenyatta anakabiliwa na wakati mgumu wa kuliunganisha taifa hilo
Baadhi ya watumbuizaji wanaotarajiwa kuhudhuria sherehe hiyoHaki miliki ya pichaAFP
Image captionBaadhi ya watumbuizaji wa kabila la Maasai wanaotarajiwa kuhudhuria sherehe hiyo
Naibu wa rais William Ruto, pia ataapishwa.
Miongoni mwa viongozi wa kigeni wanaotarajiwa ni waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, rais wa Uganda, Yoweri Museveni na rais wa Rwanda Paul Kagame.
Upinzani nchini humo umewataka wafuasi wake kususia sherehe hiyo na badala yake kukusanyika katika mkutano ili kuwakumbuka wafuasi waliouawa katika ghasia tangu uchaguzi wa mwezi Agosti.
Upinzani ulikabiliana na Polisi baada ya uchaguzi wa Agosti 8Haki miliki ya pichaEPA
Image captionUpinzani ulikabiliana na Polisi baada ya uchaguzi wa Agosti 8
Maafisa wapolisi wameonya upinzani huo dhidi ya kufanya mkutano huo.
CHANZO BBC NEWS

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget