Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Articles by "siasa"

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa ahirisho la mwisho katika kesi ya kutumia lugha ya matusi dhidi ya Rais John Magufuli  inayomkabili mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee.
Tokeo la picha la HALIMA MDEE MAHAKAMANI
Akizungumza leo Ijumaa Juni 1, 2018 Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ametoa ahirisho hilo la mwisho kwa upande wa mashtaka baada ya wakili wa Serikali mwandamizi, Patrick Mwita kudai kesi ilipangwa kwa ajili ya kuanza kusikilizwa, hawana shahidi ikiwa ni mara ya tatu.

Baada ya kutolewa maelezo hayo, hakimu Simba alitoa ahirisho la mwisho na kupanga kesi hiyo kusikilizwa tena Juni 29, 2018 kwa mashahidi wa upande wa mashtaka kuanza kutoa ushahidi.

Katika kesi hiyo Mdee anadaiwa kufanya kosa hilo Julai 3, 2017 Makao Makuu ya Chadema yaliyopo mtaa wa Ufipa wilaya ya Kinondoni.

Anadaiwa kutamka “anaongea hovyo hovyo, anatakiwa afungwe breki” kitendo ambacho kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Halima alifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo Julai 10, 2017. Katika kesi hiyo mbunge huyo  anatetewa na mawakili, Peter Kibatala, Jeremiah Mtobesya na Hekima Mwasipu.

Mbunge wa Ubungo, Said Kubenea ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Kanda ya Pwani amefunguka na kusema mgombea wa Ubunge wa jimbo la Kinondoni kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu kuwa ni mtu makini na ndiye Lissu mdogo ambaye anastaili kwenda Bungeni.
Image result for kubenea
Kubenea amesema hayo leo Januari 27, 2018 kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa marudio ambao unatarajiwa kufanyika Februari 17, 2018 katika majimbo mawili ya Kinondoni na Siha.

Kubenea amesisitiza kuwa mgombea huyo ni kati ya watu makini ambao wanapaswa kufika Bungeni kuwatetea wananchi wa Kinondoni.

"Nina mfahamu Salum Mwalimu ni kati ya waandishi wa habari wachache nchi hii walio jasiri na wasioogopa wanafanya kile wanachokiamini, ameandika stori kubwa na kuripoti matokeo makubwa sana na kutetea hadhi za binadamu, amefanya kazi kubwa kutetea misingi ya uandishi wa habari mkimpeleka Bungeni mtakuwa mmetupeleka chachu nyingine, mtakua mmemleta Lissu mwingine mdogo na kwenda kumpandikiza Bungeni" alisema Kubenea

Mbali na hilo Kubenea aliwataka wananchi kupuuza maneno yanasosambazwa kuwa Salum Mwalimu si Mtanzania na kusema huyo ni raia wa Tanzania na amekulia Tanzania bara hivyo waachane na maneno hayo yanayosambazwa na watu wa Chama Cha Mapinduzi

HAKIMU Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Mbeya, Michael Mteite hii leo ametoa uamuzi wa kutojitoa na kuendelea kusikiliza kesi inayomkabili mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.  Pia mawakili watatu wa utetezi wamejitoa katika kesi hiyo.
Hatua hiyo inafuatia baada ya Sugu na mwenzake Emanuel Masonga  ambaye ni katibu mkuu wa Chadema kanda ya nyanda za juu kusini kumkataa hakimu huyo.Wanakabiliwa na kesi ya uchochezi na wamerudishwa rumande hadi Februari 8, 2018.

Hata hivyo mbunge Sugu ameomba wiki mbili za kupanga kujitetea


Sababu ya kumnyima dhamana mshtakiwa Sugu na mwenzake ni hofu ya mshtakiwa kutohudhuria mahakamani hapo mara kwa mara ili hali Hakimu anataka kesi hiyo iishe mapema.

SABABU TATU ALIZOTOA SUGU KUMKATAA  HAKIMU

“Mheshimiwa Hakimu dhamira yangu imenituma nikukatae wewe Hakimu, kwa sababu tatu zifuatazo…

1. Sijawahi kuona hakimu yuko bias kama wewe ikiwemo kuninyima dhamana bila sababu za msingi kisheria na kikatiba.

2. Jana nilishuhudia kielelezo cha tape recoder kikitoka mikononi mwa Mwanasheria wa serikali kuja mahakamani kinyume cha sheria na hoja za wakili wangu Mwabukusi ulizipinga.

3. Kwenye mabishano umekiri kesi hii imekupa shida, mi ni Mkristo sitaki upate shida naomba nikukatae ili aje hakimu mwingine aendeshe kesi kwa uhuru bila kupata shida na mazingira ya shinikizo lolote lile.

Kwa sababu hizo naomba nikukatae and  I’m very serious about it, nakukataa”

Wakati kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge katika majimbo ya Kinondoni na Siha, zikianza kwa vitimbi, mgombea wa CCM, Maulid Mtulia amewekewa pingamizi lenye vipengele vitano.

Uchaguzi huo utakaoshirikisha vyama 12, utafanyika Februari 17 huku ukitarajiwa kuwa na mpambano mkali baina ya CCM na Chadema inayoungwa mkono na vyama vitano vya Ukawa ambavyo NLD, NCCR-Mageuzi, CUF ya upande wa Maalim Seif Sharif Hamad na Chaumma iliyojiunga hivi karibuni.

Uchaguzi huo unafanyika baada ya waliokuwa wabunge, Godwin Mollel (Siha, Chadema) na Maulid Mtulia (Kinondoni, CUF) kujivua uanachama kwa maelezo kuwa wanamuunga mkono Rais John Magufuli na baadaye kujiunga na CCM.

Chama hicho tawala kimewapitisha wawili hao kutetea majimbo hayo bila ya kuendesha mchakato wa ndani.

Kwa staili kama hiyo, Chadema imemsimamisha Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu katika jimbo la Kinondoni na Elvis Mosi (Siha).

Tayari CCM katika jimbo la Siha na CUF upande wa mwenyekiti anayetambuliwa na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, Profesa Ibrahim Lipumba wamezindua kampeni jana.

Wagombea walirejesha fomu juzi katika ofisi ya jimbo la iliyopo Magomeni.

Lakini saa chache kabla ya kuanza kampeni, Mwalimu aliwasilisha pingamizi dhidi ya mgombea wa CCM, akiwa na hoja tano, ikiwemo ya kutofanya mrejesho wa gharama za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Wakili wake, Frederick  Kihwelo amesema  kuwa kwanza, Mtulia  hajafanya mrejesho wa gharama za uchaguzi wa mwaka 2015, alipogombea kwa tiketi ya CUF.

“Jambo hili hufanywa na mtu yeyote aliyegombea nafasi ya udiwani, ubunge na urais na haijalishi kama alishinda au kushindwa,” alisema Kihwelo.

“Unapaswa kuandaa mchanganuo wa gharama zako za uchaguzi na kuzipeleka ofisi ya NEC.”

Alisema hoja ya pili ni Mtulia kushindwa kukidhi matakwa ya kisheria kwa kutojaza kwa usahihi fomu zake, kwa madai kuwa zimepigwa muhuri wa katibu wa CCM badala ya muhuri wa chama hicho tawala.

“Muhuli ulipigwa katika fomu yake unasomeka wa katibu wa chama badala ya muhuri wa chama. Hii inaonyesha chama hakijamthibitisha kugombea. Jambo hili liliwasumbua sana Chadema mwaka 2014 kwa baadhi ya wagombea wao kuenguliwa, ” alisema Kihwelo.

Alisema hoja ya mwisho ni Mtulia kujaza fomu akieleza kuwa anajishughulisha na kilimo cha mbogamboga, jambo ambalo Kihwelo amesema si kweli.

“Hiki kilimo cha mbogamboga amekianza lini kwa sababu tunajua alikuwa mbunge. Tunamtaka athibitishe hili,” alisema.

Msimamizi msaidizi wa uchaguzi wa Kinondoni, Latifa Almasi alisema wamepokea mapingamizi lakini haweka wazi idadi yake, na kubainisha kuwa leo msimamizi mkuu wa uchaguzi huo, Aron Kagurumjuli, atayatolea ufafanuzi

Chama cha ACT Wazalendo, kimesema hakitashiriki kwenye uchaguzi wa ubunge kwenye majimbo ya Kinondoni na Siha kutokana na kutoridhishwa na hali halisi na mazingira yaliyoandaliwa na tume ya uchaguzi (NEC).
Tokeo la picha la act wazalendo
ACT kimesema kwamba chama tawala kinatumia jeshi la polisi na watendaji wa serikali, ili kutengeneza mazingira ya kuwatisha wananchi na kuiba kura hata pale inapotokea wapinzani wameshinda. Hayo yamesemwa leo na chama hicho kilipokutana na waandishi wa habari ambapo Msafiri Mtamelwa, Ado Shaibu na Idrisa Koeta ndiyo waliokuwa wazungumzaji wakuu.

Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho-Bara, Msafiri Mtemelwa amesema changamoto walizozilalamikia katika uchaguzi wa Januari 13 katika majimbo ya Singida Kaskazini, Songea Mjini na Longido bado hazijafanyiwa kazi.

Amesema malalamiko ya chama hicho kwa NEC ni matumizi ya nguvu ya vyombo vya dola dhidi ya vyama vya upinzani kwa lengo la kukisaidia chama tawala CCM.

Uchaguzi wa Siha na Kinondoni unafanyika baada ya waliokuwa wabunge wa majimbo hayo kuhamia CCM Desemba mwaka jana.

Tokeo la picha la SALUMU MWALIMU KURUDISHA FORM YA KUGOMBEA KINONDONI

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar, Salum Mwalimu amefanikiwa kurudisha fomu ya kugombea Ubunge jimbo la Kinondoni huku akiwataka wanachama wa chama hicho kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha muda mfupi.

Mhe. Salum ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari vilivyoweza kujitokeza katika ofisi za Tume ya Uchaguzi Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam leo alasiri(Jumamosi).

"Nimefarijika kwamba fomu imepokelewa na haina mapungufu yeyote yale, kwa hiyo hatuna shaka lolote katika fomu yetu kwa maana tumeikagua na kuuliza maswali katika kipengele jinsi tulivyojaza na wakatujibu tupo sahihi. Imani yangu ni kwamba hawajaona kosa ambalo wanaweza kulikalia kimya walisubiri ili lilete matatizo baadae", alisema Mhe. Salum Mwalimu.

Aidha, Mhe. Salum aliendelea kufafanua baadhi ya mambo kwa kusema hatoweza kutangaza siku ya kuanza kampeni rasmi mpaka itakapofika alasiri ya kesho (Jumapili) kwa maana muda huu wa katikati ameuacha ili kama kutakuwa na watu waweze kuweka mapingamizi yao.

"Kwa hiyo baada ya muda huo kupita siku ya kesho bila ya shaka nitakuwa mgombea rasmi wa jimbo la Kinondoni ambaye nisiyekuwa na doa kwa ajili ya mapambano hayo", alisistiza Mhe. Salum Mwalimu.

Pamoja na hayo, Mhe. Salum aliendelea kwa kusema "kikubwa labda niwaambie hatukuja ku-beep wala hatu-beep kamwe haitakuja kutokea ku-beep katika jimbo la Kinondoni. 

Tunamaanisha na tunaamini kabisa kama nidhamu ya siasa waliyoikataa, hapa watairudisha na wasipoikubali kuirudisha Kinondoni maana yake ustaarabu katika siasa tunaamini utakuwa umekwishamalizika. Hatutokuwa wa kulia, safarii hii ikibidi tutawasababisha wale waliosababisha sisi tunalialia wao ndio walie".

Kwa upande mwingine Mhe. Salum Mwalimu amesema amedhamilia na amejitoa kusimamia haki ya wananchi wa Jimbo la Kinondoni na kuahidi hatoweza kuyumba katika hilo.

Mbunge wa Jimbo la Siha, Mkoani Kilimanjaro kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dk. Godwin Oloyce Mollel, aliyetangaza kujivua uanachama wa chama chake na kujiuzulu ubunge amewashukuru wananchi wake wa Siha kwa ushirikiano mkubwa waliompa wakati akiwa madarakani.

Godwin Mollel amejiuzulu nafasi yake ya Ubunge pamoja na kujivua uanachama wa CHADEMA huku akiomba wanachama wa Chama cha Mapinduzi kumpokea na kusema kuwa sababu kubwa iliyomfanya ahame ni kutokana na kuridhishwa na utendaji kazi wa Rais John Pombe Magufuli katika kupigania rasilimali za nchi

Ndugu waandishi wa habari: Nimeshikwa na mshtuko, simanzi baada ya kusambaa kwa  taarifa ambazo naweza kusema kuwa ni za uzushi kwamba  ninampango wa kujiondoa ndani ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema. naomba taarifa hizo zipuuzwe manahazina ukweli wowote na kwamba zinampango wa kunichafua mimi pamoja na Chama Changu.
Image result for mwita isaya akiwa katika kampeni
Ndugu wandishi wa habari : Napenda ieleweke kuwa  sijawahi kudhani wala kufikiria kuhama Chadema na kwenda kwenye chama chochote kile cha siasa. Chadema ni chama ambacho nimetoka nacho mbali tangu mwaka 2004 hadi leo, nimejenga chama kwa gaharama zangu mwenyewe.

Ndugu waandishi wa habari: Leo nimekuwa Meya wa jiji la Dar es Salaam kupitia Chama Changu cha Chadema,natambua kuwa  chama kimeniheshimu sana kwa kunipa nafasi hii hivyo sina sababu ya kuondoka kwani  ninania ya kuwatumikia Wananchi ambao wameniamini na wamenichagua kwa mapenzi yao wakiamini kuwa nitawaletea Maendeleo nikiwa ndani ya Chama Cha Chadema.

Nafahamu  tuhuma hizi zinatokana na aina ya utendaji wangu katika Jiji la Dar es Salaam kwani nimekuwa nikifanya kazi badala ya kupambana na serikali pale ambapo watu wanaamini kuwa mambo hayajaenda sawa.

Ndugu waandishi wa habari:  Kukaa kwangu kimya huku ,kutokufanya siasa za kiharakati ndani ya jiji la Dar es Salaam  haimanishi kwamba nipo upande wowote ama kukihujumu chama changu. Ila huu ni mfumo ambao nimeuchagua na kujijengea kwa ajili ya kuwatumikia wananchi nasio kufanya harakati za kisiasa kwakuwa nina  nia  ya kufanya maendeleo ndani ya jiji la Dar  es Salaam.

Ndugu waandishi wahabari: Naomba ifahamike kuwa hakuna Mkurya ambaye aliwahi kuwa msaliti,katika nafasi yoyote ambayo aliwahi kuwa nayo. Kutokana historia hiyo, naomba niaminike na wanachama na wananchi wote kuwa haitakuja kutokea Mkurya mimi nikakisaliti chama changu.

Nakama  itakuja kutokea nikafanya hivyo ninaweza kuhatarisha maisha yangu, Familia yangu, na hivyo kujikuta nikaingia kwenye matatizo makubwa ambayo kimsingi sio mazuri. Mama yangu ni mjane, kama itafanya hivyo Chadema wote Mkoa wa Mara hawawezi kuwaacha ndugu zangu salama .

Ndugu waandishi wa habari : Tangu nimeona watu wote waliohama ,kusaliti vyama vyao, maisha yao yamekuwa mabaya, nahata imani kwa Wananchi wao imepungua. Hivyo na Mimi  sitaki kuwa kama wao, ninania ya dhati ya kukitumikia chama changu kwa uaminifu mkubwa kama ambavyo wao wameniamini.

Kuliko kuhama Chadema ni heri mkanitafutie Mahala pengine pakuishi ambapo itakuwa ni mbinguni lakini sio hapa duniani ama kwenda kwenye Chama kingine chochote  cha kisisasa.  Kikubwa napenda kuwaeleza wana chama wote wa Chadema kuwa hivi sasa kila mmoja  tujielekeze kwa nguvu zetu zote kwenye kampeni hivi za uchaguzi mdogo wa madiwani unaotarajiwa kufanyika Novemba 26 mwaka huu.msikubali kutolewa kwenye maandalizi ya uchaguzi.

Image result for picha za lipumba cuf

Mwenyekiti wa (CUF)Profesa Lipumba amefunguka na kusema kuwa Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad ana kesi ya kujibu na kudai yeye kawaponza wabunge nane waliovuliwa uanachama wa CUF

Profesa Lipumba amesema hayo leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari na kusema Katibu Mkuu wa (CUF)  Mhe. Maalim Seif na yeye anayake ya kujibu mbele za Kamati ya Maadili na Nidhamu ya CUF.


"Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na kuna wananchama wengine wengi tu ambao pia wana makosa ya kuweza kujibu mbele ya Kamati ya Nidhamu na Maadili katika watu wote hao Katibu Mkuu yumo na yeye ndiye amewaponza hawa wabunge nane wa Viti Maalum ambao wamevuliwa uanachama na ndugu zangu wa Zanzibar na wale wabunge wengine wale msiwe mnasikiliza na kufuata kila anachosema Katibu Mkuu atakuponza kama alivyowaponza wajumbe wa baraza la wawakilishi" alisema Lipumba

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa CUF Taifa  Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesema mpaka sasa wabunge wote nane ambao wanasemakama wamefukuzwa uanachama wameamua kufungua kesi Mahakama Kuu kupinga maamuzi feki ambayo yamefanywa na Baraza Kuu feki na kuitaka Mahakama itamke kuwa wao ni wanachama halali wa CUF na wabunge halali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lakini pia Katibu Mkuu amesema kuwa Baraza Kuu halali la CUF litakutana kwa dharura siku ya kesho Ijumaa tarehe 28/07/2017 kujadili mambo mbalimbali ambayo yanaendelea katika chama hicho na kutangaza hatua ambazo zitafuata.

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget