Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Articles by "afya"


bil1
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wa kwanza kushoto akikata utepe kuashiria uzinduzi  wa mpango wa mfumo  wa matumizi  ya kielektroniki katika sekta ya afya  uliofanyika jijini Dar es salaam  katikati ni  Mwenyekiti mwenza wa Bill & Melinda gates foundation,bilionea Bill Gates na kulia ni Waziri wa TAMISEMI Simbachawene.
bil2
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wa kwanza kushoto akimkabidhi zawadi Mwenyekiti mwenza wa Bill & Melinda gates foundation,bilionea Bill Gates wakati wa uzinduzi  wa mpango wa mfumo  wa matumizi  ya kielektroniki katika sekta ya afya uliofanyika jijini Dar es salaam.
bil3
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wa kwanza kushoto akionyesha kitabu cha  mpango wa mfumo  wa matumizi  ya kielektroniki katika sekta ya afya  uliofanyika jijini Dar es salaam pamoja na  Mwenyekiti mwenza wa Bill & Melinda gates foundation,bilionea Bill Gates katikati na kulia ni Waziri wa TAMISEMI Simba Chawene.
bil4
Mwenyekiti mwenza wa Bill & Melinda gates foundation,bilionea Bill Gates akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau wa sekta ya afya hawapo pichani wakati wa uzinduzi  wa mpango wa mfumo  wa matumizi  ya kielektroniki katika sekta ya afya  uliofanyika jijini Dar es salaam.
bil5
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau wa sekta ya afya hawapo pichani wakati wa uzinduzi  wa mpango wa mfumo  wa matumizi  ya kielektroniki katika sekta ya afya unaosimamiwa na Taasisi ya Bilionea Billgate Bill & Melinda Gates  uliofanyika jijini Dar es salaam.
bil6
Mwenyekiti mwenza wa Bill & Melinda gates foundation,bilionea Bill Gates wa kwanza kushoto akisaini kitabu cha wageni wakati alipokutana na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wa pili kushoto katika  ofisi ndogo  ya wizara hiyo jijini Dar es salaam ili kuzindua mpango wa mfumo  wa matumizi  ya kielektroniki katika sekta ya afya.
bil7
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katikati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa afya wa kwanza kulia ni  Mwenyekiti mwenza wa Bill & Melinda gates foundation,bilionea Bill Gates na Katibu Mkuu Afya, Dkt. Mpoki Ulisubisya kushoto  katika  ofisi ndogo  ya wizara hiyo jijini Dar es salaam ili kuzindua mpango wa mfumo  wa matumizi  ya kielektroniki katika sekta ya afya.
bil8
Wadau mbalimbali wa sekta ya afya wakimsikiliza kwa makini  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu hayupo pichani  jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa mpango wa mfumo  wa matumizi  ya kielektroniki katika sekta ya afya.

001
Mgeni rasmi, Flora Kimaro ambaye ni Mkurugenzi  wa Huduma za Uuguzi Taasisi ya MOI akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani yaliofanyika Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili leo. Pamoja na maadhimisho hayo Chama cha Wakunga Nchini (TAMA) kimepongezwa kwa kutoa huduma za afya ambapo watu wanapima afya leo katika hospitali hiyo. Siku ya Wakunga Duniani huadhimishwa Mei 5, kila mwaka, lakini TAMA tawi la Muhimbili imeamua kuadhimisha siku hii katika wiki ya unyonyeshaji duniani.
002
Baadhi ya wananchi waliofika katika siku ya maadhimisho hayo wakimsikiliza mgeni rasmi,
003
Mgeni rasmi akikakata utepe akiashiria kuanza kwa shughuli za maadhimisho hayo ikiwa ni pamoja na kupima watu mbalimbali afya
005
Mmoja wa wauguzi, Gladisia Kessy akimpima afya mmoja wa watu waliofika Muhimbili leo kwa ajili ya kushuhudia maadhimisho hayo.
004
Mgeni rasmi pamoja na baadhi ya maofisa wa Muhimbili wakiwamo wakunga wakielekea meza kuu leo.
006
Baadhi ya watu wakifuatilia maadhimisho hay oleo.
007
Maofisa wa Muhimbili wakiwamo wakunga wakiwa katika picha pamoja leo.

IMG-20170726-WA0020
Madaktari bingwa kutoka China wakifuatilia ufunguzi huo
# 2
Daktari Bingwa kutoka China akipokea mkono wa asante kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya Dk.Kigwangalla mara  baada ya kupokea Cheti cha shukrani alichokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Agrey Mwanri
# 3 a
Dk.Kigwangalla akimuongoza Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania
………………………………………
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh.  Aggrey Mwanri amezindua rasmi kambi maalum ya huduma za Afya juu ya upimaji wa Afya bure kwa wananchi mbalimbali Wilayani Nzega, ndani ya Hospitali ya Wilaya ya Nzega.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanri ambaye alikuwa mgeni rasmi, aliwapongeza waandaaji wa kambi hiyo kwani itasaidia kuboresha afya za wananchi ili kuwa na afya njema.
“Wananchi wanahitaji Afya njema, tunapongeza kwa kambi hii kwani madaktari bingwa waliokuja hapa watatua matatizo ya msingi kwenye afya zetu. Hivyo wananchi mujitokeze kwa wingi” aleleza RC Mwanri.
Aidha, Mh. Mwanri amewapongeza  Madaktari bingwa kutoka China ambao wanaendesha kambi hiyo ya siku Sita, iliyoanza rasmi Julai 24 na inatarajia kumalizika Julai 30.
Hata hivyo, Mh. Mwanri aliwaagiza Wakurugenzi wote wa Mkoa wa Tabora waupokee mpango huo wa kambi za huduma za Afya ili uende mkoa mzima kwani wanakosa fursa ya kuonana na Madaktari bingwa.
“Ni jambo zuri, tunaomba Wakurugenzi wote mulipokee suala ili wa Mkoa wa Tabora ili liendelee Mkoa mzima. Pia ni wasaha kwa wananchi wote kupeana taarifa ili zienee kwa watu wote wajitokeze hapa Nzega kupatiwa huduma za upimaji na matibabu.” Alieleza Mh. Mwanri huku akimuagiza Mganga Mkuu ahakikishe anaratibu mpango huo uenee Mkoa nzima wa Tabora.
Kwa upande wake,Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Vijijini ameshukuru Serikali ya China kwa kufanikisha tukio hilo ikiwemo kutoa dawa za Maralia kwani kwa msingi huo utasaidia kuokoa maisha ya wananchi wa Nzega.
“Tunapokea kwa mikono miwili msaada huu wa kutoka Serikali ya China hasa kupitia kwa Balozi wake hapa nchini Tanzania. Dawa hizi ni nyingi nahakika zitasaidia wananchi wote kuanzia wilaya ya Nzega na Mkoa nzima wa Tabora kwa ujumla. Nawashukuru sana wananchi wanaojitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuja kupata  huduma za matibabu kwenye kambi hii ya madaktari bingwa hapa Nzega” alieleza Dak. Kigwangalla.
Zoezi hilo la Upimajj wa Afya Bure Wilayani Nzega, limeandaliwa na Wabunge wa majimbo yote ya  Nzega ambapo imeanza kuanzia hiyo Julai 24 na itatarajiakumalizika Julai 30, huku kwa wakazi wote wa Nzega na jirani wata pima afya zao bure na kupata huduma za matibabu bure, ikiwemo upasuaji.
Tayari timu ya Madaktari bingwa wa kila fani ya tiba wapo kwenye kambi hiyo inayoendelea kwenye Hospitali ya Wilaya ya Nzega.

TO1
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimjulia hali mtoto Nasib Robert,(kushoto) ni mama wa mtoto Veronica Chilala,wakati alipo tembelea wodi ya watoto katika hospitali ya  Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
TO2
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wakati alipo tembelea hospitali ya  Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
TO3
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipo kabidhi gari mbili za kisasa za kubebea wagonjwa,katika hospitali ya  Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
TO4
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua gari ya kubebea wagonjwa wakati alipokabidhi gari mbili za kisasa za kubebea wagonjwa,katika hospitali ya  Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
TO5
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua vifaa ndani ya gari la kubebea wagonjwa baada ya kukabidhi gari mbili za kisasa za kubebea wagonjwa,katika hospitali ya  Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………………..
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara katika hospitali ya wilaya ya Ruangwa na amekabidhi magari mawili ya kubebea wagonjwa.
Amesema kati ya magari hayo moja ni kwa ajili ya hospitali hiyo ya wilaya na la pili litapelekwa katika kituo cha afya cha Mandawa.
Waziri Mkuu amekabidhi magari hayo leo (Jumatano, Julai 12, 2017), alipotembelea hospitali hiyo, ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi Mkoani Lindi.
Amesema magari hayo ni muendelezo wa mkakati wa Serikali ya awamu ya tano wa kuboresha huduma za afya kwa wananchi wake.
 “Rais wetu Dkt. John Magufuli amedhamiria kuwaondolea wananchi kero mbalimbali zinazowakabili zikiwemo za huduma za afya, hivyo tuendelee kumuunga mkono.”
Waziri Mkuu amesema magari hayo ya kisasa yatasaidia kurahisisha usafiri kwa  wagonjwa wanaohitaji matibabu ya dharura katika hospitali kubwa.
 Kabla ya kukabidhi magari hayo, Waziri Mkuu alitembelea wodi ya  akina  mama na ya  watoto waliolazwa katika hospitali hiyo na amesema kwamba ameridhishwa na hali ya utoaji huduma.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Mheshimiwa Rashid Nakumbya amesema magari hayo ni faraja kwao kwa kuwa walikuwa na changamoto ya usafiri kwa wagonjwa wa dharura.
“Tunatambua na kuthamini jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano katika halmashauri yetu na Taifa kwa ujumla, nasi tutayatumia magari haya kama ilivyokusudiwa.”
Awali, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa, Dkt. Regan Rajuu amesema hali ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika hospitali hiyo umeongezeka kutoka asilimia 80 Desemba, 2016 na kufikia asilimia 90 Juni 2017.
Pia Waziri Mkuu alitembelea shule ya Sekondari ya Kassim Majaliwa iliyoanza kujengwa Desemba, 23, 2016 kwa michango ya Halmashauri, fedha za mfuko wa jimbo pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Kaimu Mkuu wa shule hiyo, Mwalimu Emmanuel Sechawe alisema msingi wa kuanzisha shule hiyo ulitokana na uwepo wa wanafunzi 319 waliofaulu darasa la saba mwaka 2016 kukosa nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza katika shule zilizopo.
Mbali na kutembelea shule hiyo, pia Waziri Mkuu alifanya ukaguzi wa maendeleo ya mradi wa ujenzi wa gereza la wilaya ya Ruangwa, ambalo litakapokamilika litapunguza msongamano wa wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Nachingwea.

KC1
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa. Mohamed Janabi akipeana mkono na Kiongozi wa Msafara wa baadhi ya Wabunge kutoka Uganda Mhe. Cecilia Barbara wakati wa ziara yao katika Taasisi hiyo kwa lengo la kujifunza leo Jijini Dar es Salaam.
KC2
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa. Mohamed Janabi akielezea jambo wakati wa ziara ya Wajumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii wa Bunge la Uganda waliotembelea Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Wabunge hao wametembelea Taasisi hiyo ili kujionea namna inavyofanya majukumu yake.
KC3
Mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Zungu akizungumza jambo mbele ya Wabunge kutoka Uganda walipotembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Kiongozi wa Msafara wa Wabunge kutoka Uganda Mhe. Cecilia Barbara na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa. Mohamed Janabi (katikati).
KC4
Baadhi ya Wabunge kutoka Uganda wakifuatilia Maelezo kuhusu namna Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) inavyofanya kazi wakati wa ziara yao katika Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
KC5
Baadhi ya Wabunge kutoka Uganda wakiwa katika sehemu ya mapokezi ya kuingia Wodi ya Watoto katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) leo Jijini Dar es Salaam.
KC6
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa. Mohamed Janabi (mwenye tai nyekundu) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wabunge kutoka Uganda walipotembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa lengo la kujifunza leo Jijini Dar es Salaam.Picha zote: Frank Shija – MAELEZO
………………………………………………………….
Na.Agness Moshi-MAELEZO
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imekua mkombozi kwa wagonjwa wa moyo Afrika Mashariki kufuatia kupungua kwa gharama za matibabu ukilinganisha na ilivyokua hapo awali.
Akizungumza na waandishi wa habari  leo jijini Dar es Salaam, Mbunge wa  jimbo la Dokolo nchini Uganda Bi.Cecilia Barbara alipotembelea taasisi hiyo ili kuona na kujifunza  jinsi Serikali ya Tanzania inavyotoa huduma za Afya kwa wananchi wake .
Bi.Cecilia  amesema  taasisi hii ni msaada mkubwa kwa Afrika Mashariki kwasababu itasaidia kupunguza idadi ya wagonjwa wa moyo wanaopelekwa  nchini India au Afrika Kusini  kwa matibabu kama ilivyo awali baadala yake watatibiwa Tanzania au nchini kwao.
“Tunahitaji kubadilishana mawazo kama wana Afrika Mashariki, kwasababu kwa kuja hapa tumegundua tunavifaa na uwezo wa kupunguza gharama za matibabu ya moyo“ Alisema Bi.Cecilia.
Bi Cecilia amesema  kutokana na ubora huduma zinazotolewa na taasisi hii  tangu kuanzishwa kwake  serikali ya Uganda imekubali  kuja kutembelea Tanzania ili kujifunza na kuanzisha mradi kama huu.
“Hatukujua kama Tanzania kuna mradi mkubwa kama huu na unaofanya kazi nzuri lakini kwa kuja tumejua na tunategemea kuanzisha mradi kama huu japo itatuchukua muda kufikia hatua iliyofikiwa na Tanzania”aliongeza Bi.Cecilia .
Naye Afisa Mwandamizi Kitengo cha Utafiti wa Bunge la Uganda Mhe. Jonathan Enamu  amesema kuwa amejifunza mengi kwenye ziara hii na ameona ni jinsi gani gharama za matibabu zimepungua kwa wagonjwa wa moyo. “Nimejifunza mengi, ikiwemo jinsi ya kupunguza  gharama za matibabu na namna bima za afya zinavyoweza kutumika katika matibabu“ alisema Bw. Enamu.
Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Prof. Mohamed Janabi  amesema kuwa , wanatoa huduma kwa watu wote kuanzia daraja la chini  na watu kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Uganda,comoro,Yemen na Kenya.
 Prof.Janabi amesema kuwa taasisi hiyo imefanikiwa kutumia shilingi bilioni 1.65 badala ya shilingi bilioni 4.72 ambayo ni sawa na kupunguza takribani asilimia 65 ya gharama za matibabu ya magonjwa ya moyo nchini kama wangewapeleka India kwa matibabu
Prof. Janabi alifafanua kuwa kwa mgonjwa mmoja wa maradhi ya moyo anatibiwa kwa shilingi milioni 35-40 tofauti na nchini India ambapo mgonjwa mmoja anatumia shilingi milioni 120.
Aidha Profesa Janabi ameishukuru Serikali kwa kuipa ushirikiano taasisi hiyo kwani kwa mwaka huu wa fedha Taasisi imepokea asilimia 100 ya bajeti itakayosaidia kuendesha shughuli zao kwa kiwango cha kuridhisha.
Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii na  Mbunge wa ilala Mhe. Azzan Mussa Zungu (MB) amesema  kuwa wamewapeleka  wageni hao kwenye taasisi ya moyo ili waweze kujifunza na kuona ni jinsi gani Tanzania imefanikiwa kupunguza gharama za matibabu kwa wagonjwa wa moyo
“wameona namna sisi Tanzania tulivyopunguza gharama kutoka kuwapeleka watu 300 kwa mwaka nje kwa matibabu ya moyo mpaka sasa watu wanne tu, ambao tunawapeleka si kwa sababu hatuna uwezo bali ni kwa sababu ya vifaa havijakidhi “ alisema Mhe.Zungu.
Taasisi ya  Moyo Jakaya Kikwete ilianzishwa rasmi mwaka 2014 inashughulika na utoaji wa matibabu kwa wagonjwa wa moyo, kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa udaktari,ufamasia na uuguzi. Pia taasisi hii inashirikiana na nchi nyingine duniani kwa kubadilishana maarifa,uzoefu na kufanya mafunzo mbalimbali.                               

jana1
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akisaini kitabu cha wageni alipotembelea katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
jana2
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwaeleza viongozi mbalimbali waliotembelea viwanja vya  maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jinsi Taasisi yake inavyofanya kazi za kutibu magonjwa ya Moyo na umuhimu wa kupima afya mara kwa mara japo mara moja kwa mwaka.
jana3
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiongea jambo na Mkurugenzi wa Huduma za Biashara wa Tan Trade Fidelis Mugenyi wakati alipotembelea  maonyesho ya Kimataifa ya biashara yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam.
jana4
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  Aika Nnkya akimsikiliza Haubert Makoke  ambaye alimuuliza swali kuhusu magonjwa ya Moyo wakati alitembelea banda la Taasisi hiyo lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya kupima magonjwa ya Moyo bure, kupata ushauri  na kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo wanazozitoa.
jana5
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimpa ushauri kuhusu afya ya Moyo Mzee John Lihame aliyembelea banda la Taasisi hiyo lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya kupima magonjwa ya Moyo bure, kupata ushauri na kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo wanazozitoa.
jana6
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Bashir Nyangasa akiwaonyesha wananchi waliotembelea banda la Taasisi hiyo  lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jinsi upasuaji wa Moyo unavyofanyika.

Image result for picha ya ummy mwalimu


HOTUBA YA MHESHIMIWA UMMY MWALIMU (MB), WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KATIKA UFUNGUZI WA MKUTANO WA KWANZA WA KUPITIA UTEKELEZAJI WA MKAKATI WA UBORESHAJI WA KASI YA UIBUAJI WA WAGONJWA WA KIFUA KIKUU NCHINI, KATIKA UKUMBI WA KILIMANI LANDMARK, DODOMA, JULAI 4, 2017

  • Katibu Mkuu wamjw,
  • Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI ,
  • Mganga Mkuu Kiongozi,
  • Wajumbe kutoka Global Fund,
  • Wakurugenzi na Wawakilishi wa USAID, CDC, EGPAF, AGPAHI, Save the Children, FHI, MDH, AMREF, KNCV, Delloite, Baylor, Water Reeds na wengine,
  • Wakurugenzi kutoka TAMISEMI na WAMJW,
  • Mameneja Mipango ya NTLP, RCH na NACP,
  • Waganga Wakuu wa Mikoa na Waganga Wakuu wa Wilaya,
  • Waratibu wa Mikoa na Wilaya wa TB na Ukoma na TBHIV,
  • Watoa huduma kutoka Vituo vya Afya katika Halmashauri,
  • Waandishi wa Habari,
  • Waalikwa wote,
  • Mabibi na Mabwana.
Awali ya yote nitumie fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutujalia afya njema na kutuwezesha kukutana hapa. Pili, niwashukuru waandaaji kwa kunialika katika mkutano huu muhimu; mkutano wa kwanza wa kitaifa wa kufanya mapitio ya utekelezaji wa mkakati wa uboreshaji wa kasi ya uibuaji wa wagonjwa wa kifua kikuu. Hii ni hatua muhimu kujiangalia na kuona njia tunayopitia katika juhudi za kuhakikisha tunawafikia kila mwenye uhitaji wa huduma za matibabu ya kifua kikuu. Vile vile, nitumie fursa hii kuwakaribisha wajumbe wote na nawapongeza kwa kuchukua muda wenu kuja kuhudhuria kikao kazi hiki muhimu. Natambua pia ya kuwa kuna wajumbe wengine wamesafiri umbali mkubwa na wengine wametoka nje ya nchi; “napenda kusema wote karibuni sana hapa Dodoma, makao makuu ya nchi yetu”.
Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana,
Utoaji wa huduma za afya usiozingatia ubora huathiri kila mtu, si tu wateja na wagonjwa wetu, hata sisi watoa huduma. Huduma zikiwa mbovu zinawafanya hata wanaozihitaji kukata tamaa na kutojitokeza vituoni. Malengo Endelevu ya Maendeleo na mkakati wa Dunia wa kutokomeza kifua kikuu (End TB Strategy)  yametilia mkazo utoaji wa huduma za afya zenye ubora wa hali ya juu na kwamba si budi juhudi za makusudi kufanyika ili kila mhitaji kufikiwa. Masuala ya ubora wa huduma za afya yamepewa kipaumbele katika mkakati mpya uliotolewa na Shirika la Afya Duniani wa kutokomeza kifua kikuu ifikapo mwaka 2035. Wakati huo huo, kikao cha Baraza la Shirika la Afya Duniani kilochoketi mwezi uliopita kimeziagiza nchi wanachama na Shirika la Afya Duniani (WHO) kutilia mkazo wa kipekee mipango yakinifu ya ubora katika utoaji huduma zote za afya. Kikao hicho, kimewataka wahisani na mashirika yenye uwezo kuzisaidia nchi zenye uhitaji ili kuzijengea ujuzi wa kuboresha misingi ya huduma bora za afya.
Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana,
Changamoto kubwa tuliyonayo hapa kwetu Tanzania, ni kutoweza kuifikia sehemu kubwa ya wagonjwa wa kifua kikuu. Kiasi cha wagonjwa zaidi ya 100,000 wa kifua kikuu hatuwafikii kila mwaka. Licha ya kuwa na mazingira yaliyosawa na maeneo mengine mfano katika Mikoa ya Rukwa, Katavi, Simiyu, Shinyanga, Kigoma, Kagera, Dodoma, Iringa, Mara na Singida inagundua wagonjwa wachache sana ikilinganishwa na Mikoa ya Mbeya, Lindi, Mtwara na Tanga.  Tafiti nyingi zimeonyesha kwamba, tunahitaji mbinu mpya za kuboresha huduma tunazozitoa ili kuhakikisha kila mgonjwa na mteja anayekuja katika vituo vyetu vya huduma anapata fursa ya kuchunguzwa kikamilifu ili kubaini kama anaugua kifua kikuu au la.
Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana,
Mkakati wa uboreshaji kasi ya uibuaji wagonjwa wa kifua kikuu ni mkakati uliojaa mbinu za kiuendeshaji ili kuvipa uwezo vituo vyetu vya huduma kufanya uchunguzi wa kina kwa kila mteja anayepata huduma vituoni na kuwapata wote wenye kuugua kifua kikuu na kuwaanzishia matibabu. Mathalan, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma katika miezi sita baada ya kuanza kutekeleza mkakati huu wameongeza wastani wa kuibua wagonjwa wa kifua kikuu kutoka 28 hadi 54 kwa mwezi. Tunahitaji kubadili mtazamo wetu na utendaji kazi wetu hasa suala zima la  kuhakikisha tunafanya upekuzi na uchunguzi wa wagonjwa vituoni, tusingoje mgonjwa atufuate na kutueleza dalili za kifua kikuu akiwa kituoni, hivyo ni vyema juhudi zetu zianzie kuwatambua wagonjwa hawa katika jamii.

Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana,
Ili kuhakikisha tunaweka misingi mizuri ya utekelezaji wa mkakati huu, Wizara ikishirikiana na Global Fund, imetengeneza kitita kiongozi ili kutoa mwongozo kwa watoa huduma katika kila kitengo na kliniki ndani ya vituo vya huduma jinsi ya kufanya hatua kwa hatua kubaini kifua kikuu kwa kila mwenye kugua bila kukosa. Mkakati huu muhimu unatoa fursa kwa kila kitengo kujitathmini ili kuweka misingi timilifu ya uchunguzi wa kifua kikuu kwa wateja wote wanaohudhuria matibabu katika eneo lao. Kitita hiki kinaviwezesha vituo vyetu vya huduma kumfikia kila mmoja mwenye uhitaji wa uchunguzi wa kifua kikuu, kutoa huduma zinazozingatia usawa, usalama wa mgonjwa au mteja na huduma zinazokidhi viwango vya Kimataifa.
Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana,
Tunao wajibu wa kuhakikisha mkakati huu unatekelezwa kwa ufanisi uliokusudiwa, ili tufikie lengo hilo, Wizara kwa mara ya kwanza imeanzisha rejesta mpya ya wanaohisiwa kuwa na kifua kikuu itakayowekwa katika kila ngazi ya utoaji wa huduma za Afya hapa nchini. Tayari rejesta hizi zimesambazwa na kuanza kutumika katika mikoa 16 iliyoanza kutekeleza zoezi hili. Kesho kutwa, wote hapa tutashuhudia kuzinduliwa kwa mkakati huu maalumu wa uboreshaji huduma za uibuaji wagonjwa wa kifua kikuu katika Halmashauri.  Zana hizi zitatoa mwanga na kuangaza njia bora za kuchunguza kifua kikuu na kubaini wote wenye kuugua katika jamii yetu mijini na vijijini. Mafanikio endelevu ya mkakati huu, yanategemea jinsi tutakavyojipanga kuanzia ngazi ya zahanati hadi wasimamizi ngazi ya kitaifa katika Wizara ya Afya na TAMISEMI. Mbinu zinazoelekezwa ni za kawaida, nyepesi na zinaeleweka vizuri na utekelezaji wake utaleta matokeo chanya na unaweza kufikiwa na kila mtoa huduma. Kazi zilizoainishwa katika kutekeleza mkakati huu zinatoa chagizo kwa watoa huduma vituoni na wasimamizi kuwajibika kikamilifu, kila mmoja katika nafasi yake na kujenga timu imara katika kila eneo la kazi.
Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana,
Nimetaarifiwa kuwa, utekelezaji wa mkakati huu ulianza mnamo Julai, 2016, ambapo ni mwaka mmoja sasa tokea vituo vya mwanzo katika Mikoa ya Mbeya na Dodoma ianze kuweka msukumo mpya. Kuanzia hapo, Mikoa 16, wilaya 48 na vituo 187 nchini kote vimeweza kuanza utekelezaji. Katika mkutano huu wa kwanza wa kufanya mapitio na tathmini ya utekelezaji wa mkakati huu, ninafarijika kuwa umehudhuriwa na wajumbe wa RHMT na CHMT na watumishi kutoka vituo vya huduma katika Mikoa hiyo yote 16 ambao wote ni walengwa wakuu katika kufanikisha jukumu hili.
Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana,
Napenda kubainisha changamoto mbili kuu tunazo hitaji kukabiliana nazo, Moja, kuanzisha mfumo imara wa ufuatiliaji na usimamizi elekezi, Pili, ni kuhakikisha tunatoa usimamizi imara na wenye tija katika kuimarisha ufanyaji kazi kama timu ya ushindi na kuvifanya vituo vyetu kutoa huduma kwa wagonjwa wa kifua kikuu zilizo za bora na endelevu. Kufikia hatua hizi yatubidi kuimarisha timu za uboreshaji huduma vituoni (Quality Improvement teams – QIT) na kuzipa uwezo zaidi wa kusimamia viwango vya ubora wa huduma za afya katika maeneo yao ya kazi vituoni, hospitali na vituo vya ngazi za chini pia.


Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana,
Napenda kuwaaminisha ya kuwa, tukiweza kuwabaini wale wanaofanya vizuri zaidi katika vituo vilivyo katika Halmashauri zetu na tukawatumia kueneza utendaji wao mzuri katika maeneo mengine inaweza kuleta matokeo chanya kwa haraka na kupata mafanikio endelevu. Watendaji bingwa hawa, watatusaidia kurahisisha hatua za ugatuzi na kupanua huduma hizi katika nchi nzima. Ili mpango huu ulete mafanikio tunayoyatarajia, inabidi timu za uendeshaji za Mikoa na Halmashauri kuwapa kila msaada ili wafanye vizuri zaidi na kuimarisha ubora wa mfumo mzima wa afya katika maeneo yetu.

Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana,
Mkakati huu na utekelezaji wa kazi nyingine za kuimarisha mfumo wetu wa huduma bora za afya hatuwezi kuvifanya peke yetu; yatubidi kuzitelekeleza katika ushirika wa pamoja kati ya Serikali na wadau wetu. Ni napenda kutumia fursa hii, kuwashukuru wadu wetu wa maendeleo kwa ushirikiano na misaada mnayoendelea kutupatia. Wote kwa pamoja tunawashukuru sana.
Hitimisho:
Kwa mara nyingine tena nitumie fursa hii kuwashukuru wadau wa maendeleo kwa kutusaidia kuimarisha miundo mbinu ya Afya, mifumo ya uendeshaji huduma za afya na udhibiti wa magonjwa mbali mbali yakiwemo UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria. Ni imani yangu pia ya kuwa ushikaino huu utazidi kuimarika na kusonga mbele ili tuweze kuboresha utoaji wa huduma za Afya. Ni imani yangu vile vile kwamba kongamano hili ni fursa ya kipekee kubadilishana uzoefu wa namna ya kutenda kazi kwa ufanisi wa hali ya juu katika kuibua mbinu bunifu mbali mbali ili kuboresha huduma katika mikoa na Halmashauri zetu.
Baada ya kusema haya machache, sasa napenda kutamka rasmi kuwa, mkutano huu umefunguliwa.
Asanteni kwa kunisikiliza.

unnamed
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Tano wa Sayansi ya Afya waChuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS) Dk. Irene Kida akitoa majumuisho ya Mkutano huo mbele ya Mkurugenzi wa Elimu ya juu, Wizara ya Elimu, Sayansi, teknolojia na mafunzo ya Ufundi, Profesa Sylvia Temu (wa tatu kushoto meza kuu) wakati wa hafla fupi ya kuhitimisha mkutano huo uliofanyika kwa mwishoni mwa wiki  jijini Dar es Salaam. Wengine ni pamoja na walimu na uongozi wa chuo hicho akiwemo Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa MUHAS, Prof. Appolinary Kamuhabwa ( wa pili kushoto)
1
Mkurugenzi wa Elimu ya juu, Wizara ya Elimu, Sayansi, teknolojia na mafunzo ya Ufundi, Profesa Sylvia Temu (wa pili kushoto) akisikiliza maelezo kuhusiana na dawa za asili zinazoandaliwa na kitengo cha tiba asili katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS) alipotembelea maonyesho ya shughuli zinazofanywa na MUHAS mara baada ya kuhitimisha Mkutano wa tano wa kisayansi ulioandaliwa na chuo hicho jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. Wanaoshuhudia ni pamoja na viongozi wa Chuo hicho akiwemo  na Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa MUHAS, Prof. Appolinary Kamuhabwa (kushoto)

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla amekabidhi jumla ya vifaa 831 vyenye thamani ya jumla ya Shilingi milioni 400, kwa kituo cha Afya Mkoani Kibaha Mjini, vifaa vilivyotolewa na Mbunge wa jimbo hilo, Mh. Silvestry Koka.

Awali kabla ya kukabidhi vifaa hivyo, Dk. Kigwangalla alipata wasaha wa kukagua maeneo ya majengo ya Kituo hicho cha Afya huku akbaini mambo mbalimbali aliyoagiza yafanyiwe kazi ili kituo hicho kiweze kuwa Hospitali ya Wilaya pindi itakapokamilisha vigezo
Wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Dk. Kigwangalla alipongeza juhudi za Mh. Koka kwa kujali wananchi wake kwani hadi kuweza kupata vifaa hivyo aliweza kutumia maarifa na ukaribu wake na wananchi wake hivyo kufika kwa vifaa hivyo vitakuwa faraja kubwa kwa Wanakibaha na wananchi wote wa maeneo jirani.

“Nampongeza Mbunge Koka kwa kuwaletea vifaa hivi. Kwani ni vizuri na vitakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Kibaha na maeneo yake ya jirani. Nakupongeza sana sana” alieleza Dk. Kigwangalla wakati wa tukio hilo la kukabidhi vifaa hivyo.

Aidha, aliwataka wananchi wa Kibaha mjini waweze kuwa karibu na Mbunge wao na wamwamini kwani anawajali ndio maana anawatumikia kwa kila njia ikiwemo kuwaletea maendeleo kwa ujumla.
Kwa upande wake, Mbunge wa Kibaha Mjini Mh. Silvestry Koka amemshukuru Naibu Waziri Dk. Kigwangalla kwa kuweza kufika na kujionea Kituo hicho sambamba na kukabidhi vifaa huku akimuomba kuendelea kufika mara kwa mara kujionea mipango ya Afya jimboni humo.
“Leo hiii najisikia faraja kwa vifaa hivi kuweza kufika  hapa jimboni kwangu kutoka nchini Marekani. Nawaomba vitumike kwa uangalifu mkubwa sana na viweze kuwa msaada kwetu” alieleza Mh. Koka.
Awali alieleza kuwa, kiasi cha shilingi milioni 32  fedha zilizotolewa na Halmshauri ya mji wa Kibaha ziweza kusaidia usafirishaji wa vifaa hivyo kutoka nchini Marekani huku yeye kama Mbunge akitumia gharama ya shilingi milioni 12 kwa ajili ya kuwaleta wataalam kwa ajili ya ukaguzi na kuvifunga vifaa hivyo.
Mbunge huyo ameeleza kuwa, vifaa hivyo vitagawia katika zahanati na vituo vyote vilivyopo mjini Kibaha na maeneo mengine yenye uhitaji.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza katika tukio hilo la kukabidhi vifaa tiba vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini, Mh. Koka

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla akikabidhia  nyaraka zenye vifaa tiba akikabidhiwa na  Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini, Mh. Koka
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla akikabidhi nyaraka yenye idadi ya vitu hivyo vya vifaa tiba kwa uongozi wa Kituo cha Afya Mkoani Kibaha Mjin wakati wa tukio hilo la kukabidhi vifaa tiba vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini, Mh. Koka

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla akishuhudia vitu hivyo vilivyotolewa  na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini, Mh. Koka

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi akiwa katika picha wakati wa tukio hilo

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla kisalimiana na na uongozi wa Mkoa na Wilaya ya Kibaha




Afisa
Muuguzi kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Cesilia Meela akiwatoa
damu baadhi ya Wakazi wa eneo la Mbagala, Jijini Dar es salaam wakati wa
zoezi la kuchangia damu lililofanywa na Taasisi ya Doris Mollel kwa
kushirikiana na Benki ya CBA, iliyofanyika kwenye Kituo kikuu cha
Mabasi, Mbagala Rangi Tatu, jijini Dar es Salaam jana. Jumla ya Units
106 zilipatikana.

Sehemu
ya Wakazi wa eneo la Mbagala Rangi Tatu wakishiriki zoezi la uchangiji
damu, llililofanywa na Taasisi ya Doris Mollel kwa kushirikiana na Benki
ya
CBA, iliyofanyika kwenye Kituo kikuu cha Mabasi, Mbagala Rangi Tatu,
jijini Dar es Salaam jana.

Mdau
Pina Mshana alikuwa ni mmoja wa waliochangia damu katika zoezi hilo,
ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya siku ya Damu Duniani.



Wachangia damu wakiwa kwenye foleni.


MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget