Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

WAKULIMA WA KIJIJI CHA IPILIMA WILAYANI MUFINDI WANUFAIKA NA MAFUNZO YA SHAMBA DARASA KUTOKA YARA TANZANIA


Aidan Timos (pichani kulia) ni mkulima wa mahindi na nyanya kutoka kijiji cha Ipilimo, wilayani Mufindi mkoani Iringa. Aidan amekuwa mkulima mashururi aliefanikiwa kubadili kilimo chake cha mazoea na kwenda kwenye kilimo cha biashara baada ya kupata elimu ya lishe linganifu ya mimea kutoka Yara Tanzania Ltd miaka miwili iliyopita. 

Kutokana na jitihada zake kwenye kilimo, wanakijiji walimteua kuwa Mwenyekiti wa kijiji hicho. Mwanzoni mwa msimu huu wa mahindi, Timos aliwakaribisha Yara Tanzania Ltd kijijini kwao kwa ajili ya kutengeneza shamba darasa ambalo wakulima katika kijiji hicho waliweza kujifunza kwa vitendo. "Kupitia mimi wakulima wengi wamenufaika na pia nawashukuru Yara kutuwekea mashamba darasa kwenye kijiji chetu ili wale ambao bado hawajapata elimu ya mbolea basi wajifunze kwa vitendo".Pichani kushoto ni Afisa Ugani wa Yara Tanzania Wilayani Mufindi, Andrew Mwangomile.

Afisa Ugani wa Yara Tanzania Wilayani Mufindi, Andrew Mwangomile akitoa mafunzo ya shamba darasa kwa Wakulima wananchi wa kijiji cha Ipilimo, wilayani Mufindi mkoani Iringa.
Wakulima wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mafunzo ya utumiaji bora ya mbolea kwa vitendo.
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget