Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Articles by "Makala kimataifa"

RUSHWA ni miongoni mwa vitu vinavorudisha nyuma maendeleo ya nchi nyingi duniani, kutokana na kukwamisha maendeleo na kusababisha kukosekana kwa haki, utawala bora wa sheria na uvunjifu wa sheria katika nchi nyingi duniani.

Licha ya kuwa rushwa ni tatizo kwa nchi nyingi duniani, lakini kuna nchi zinatajwa kuwa na kiwango kidogo cha rushwa huku sababu kubwa ikitajwa kuwepo kwa utawala bora, uwazi katika kufanya maamuzi na kiwango kizuri cha maisha.

Kwa mujibu wa Corruption Perception Index hizi ndizo nchi 10 zenye kiwango kidogo cha rushwa kwa mwaka 2017.

1: Denmark

Licha ya kuwa miongoni mwa nchi zenye furaha duniani, Denmark inatajwa pia kuwa nchi namba moja yenye kiwango kidogo cha rushwa ambapo kwa mujibu wa Corruption Perception Index nchi hiyo inapata 92% kwa mwaka 2017.


2: New Zealand

Ni nchi namba mbili kuwa na kiwango kidogo cha rushwa duniani ambapo sababu kubwa inayofanya nchi hii kuwa na kiwango kidogo cha rushwa ni uwepo wa utawala bora. Serikali ya New Zealand hufanya maamuzi kwa uwazi na hali nzuri ya kiuchumi.

3: Finland
Miongoni mwa sababu inayoifanya Finland kuwa na kiwango kidogo cha rushwa kwa mujibu wa taasisi ya kuchunguza rushwa duniani ni uwepo wa hali ya haki na usawa na hali nzuri ya kiuchumi. Imepata 89%.

4: Sweden
Kwa mujibu wa Katiba ya Sweden, Bunge lina nafasi kubwa ya kufanya maamuzi ukilinganisha na serikali. Hali hii inaifanya serikali ya nchi hiyo kuogopa kufanya makosa ya rushwa kwa sababu ya Bunge kuwa na nguvu kubwa. Aidha, katika nchi hii matumizi mabaya ya madaraka huonekana pia kama rushwa.

5: Norway
Norway ni miongoni mwa nchi zenye kiwango kidogo cha rushwa, na kwa mujibu wa Corruption Perception Index, inapata 86% kwa kuweza kupambana na rushwa kwa mwaka 2017.

6: Switzerland
Switzerland imefanikiwa kupambana na rushwa kwa 86% na kwa mujibu wa taasisis ya kupambana na rushwa, nchi hiyo imefanikiwa kwa sababu Katiba yake inaruhusu wananchi kujihusisha katika majidiliano wakati serikali inafanya maamuzi kupitia njia ya kura za maoni.

7: Singapore
Kwa mujibu wa Corruption Perception Index, Singapore imefanikiwa kwa zaidi ya 84% kupambana na rushwa na inatajwa kuwa nchi ya saba kwa mwaka 2017 kuwa na kiwango kidogo cha rushwa.

8: Uholanzi
Uholanzi ni miongoni mwa nchi zinazotajwa na Corruption Perception Index kwa kuwa na kiwango kidogo cha rushwa ambapo sababu kubwa inayochangia ni uwepo wa program za kuzuia rushwa.

9: Luxembourg 
Inatajwa kuwa moja kati ya nchi ndogo na tajiri zaidi katika nchi za Umoja wa Ulaya ambapo sababu kubwa inayoifanya nchi hiyo kuwa mongoni mwa nchi zenye kiwango kidogo cha rushwa ni hali ya uchumi kuwa nzuri kwa kila raia wa nchi hii.

10: Canada.
Canada ni miongoni mwa nchi zenye kiwango kidogo cha rushwa duniani ambapo moja ya sababu kubwa inayochangia kuwepo kwa kiwango kidogo cha rushwa ni Bunge la nchi hiyo kuwa na nguvu zaidi ya serikali hivyo kupelekea serikali kufanya maamuzi kwa uwazi na utawala bora.


USS Carl Vinson Picha: 14 Aprili 2017Image caption Meli ya kubeba ndege za kivita ya USS Carl Vinson (kushoto) na meli nyingine zilielekea Bahari ya Hindi

KUNDI  la meli za kivita za Marekani, ikiwemo meli yenye uwezo wa kubeba ndege za kivita, hazikuwa zinaelekea upande wa Korea Kaskazini kama ilivyoripotiwa awali, bali zilikuwa zinaelekea eneo tofauti.

Jeshi la wanamaji la Marekani lilikuwa limetangaza 8 Aprili kwamba kundi hilo la meli likiongozwa na meli kubwa ya Carl Vinson lilikuwa likielekea rasi ya Korea, kama hatua ya kuionya Korea Kaskazini.

Wiki iliyopita, Rais wa Marekani Donald Trump pia alitangaza kwamba kundi kubwa la meli za kivita lilikuwa likitumwa eneo hilo.

Lakini imebainika kwamba ukweli ni kuwa meli hizo zilikuwa zinaelekea eneo tofauti.

Taarifa zinazsema kwamba kufikia mwishoni mwa wiki, zilikuwa zimesafiri mbali sana na rasi ya Korea na zilikuwa zinapitia mlango wa bahari wa Sunda kuingia katika Bahari ya Hindi.

Wakuu wa jeshi la wanamaji la Marekani katika Bahari ya Pasifiki walisema Jumanne kwamba walikuwa wamefutilia mbali safari ya meli hizo katika bandari ya Perth.

Hata hivyo, wanajeshi wake walikuwa wamekamilisha mazoezi ya pamoja ya kijeshi yaliyokuwa yamepangwa awali kati ya majeshi ya Marekani na Australia katika pwani ya kaskazini magharibi mwa Australia.

Baada ya mazoezi hayo, meli hizo zilielekea Singapore mnamo Aprili  8 mwaka huu, kundi hilo la meli sasa "linaelekea Magharibi mwa Pasiki kama lilivyoamrishwa".

mapMwandishi wa BBC anayeangazia habari za Korea Stephen Evans anasema bado haijabainika iwapo kulitokea suitafahamu katika mawasiliano au labla Marekani ilipotosha watu makusudi kujaribu kumtia wasiwasi kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.

Awali, Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence alionekana kutoyumba alipohutubia wanahabari akiwa kwenye meli ya kivita ya USS Ronald Reagan ambayo imetia nanga Japan.

Aliapa kwamba Marekani iko tayari "kushinda shambulio lolote na kukabiliana na matumizi yoyote ya silaha za kawaida au za nyuklia kwa nguvu zake zote."

Korea Kaskazini na Marekani zimekuwa zikijibizana vikali viki za hivi karibuni na safari ya meli hizo ilikuwa imeibua uwezekano wa Marekani kutekeleza shambulio la mapema kujaribu kulemaza mfumo wa kijeshi wa Korea Kaskazini.

Jumatano,  Pence alitaja taifa hilo kuwa "tishio kubwa zaidi na la dharura kwa amani na usalama" katika maeneo ya Asia na Pasifiki.
Chanzo BBC NEWS

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget