Meya Mwita awasilisha Mpango wa bajeti bilioni 75.2, 2018/ 2019
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ,aliyesimama, kulia ni Mkurugenzi wa jiji Sipora Liana, kushoto ni Naibu Meya wa jiji Mussa Kafana |
MSTAHIKI
Meya wa jiji la Dar es Salaam , Isaya Mwita leo amewasilisha mpango wa bajeti wa
mwaka 2018 hadi 2019 ambapo jumla ya shilingi bilioni 75.2 zitatumika kwa mwaka
huo.
Hata hivyo mpango
huo umepitishwa kwa kauli moja na Madiwani wote wa halmashauri hiyo huku
wakimpongeza kwa kusema kuwa jiji
limepata Meya anayejali maslahi ya maendeleo katika halmashauri hiyo.
Halmashauri hiyo imeandaa mpango huo kwa
kuzingatia taratibu zinazotakiwa kufuatwa na mamlaka za Serikali za mitaa
katika utayarishaji wa makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka wa fedha wa 2018 na 2019.
Akizungumzia
mpango huo kwenye mabaraza la Madiwani
na waandishi wahabari , Meya Mwita amesema kuwa jiji limekadiria kukusanya na
kutumia shilingi bilioni 75.2 ambapo itatokana kwenye vyanzo mbalimbali vya mapato ikiwemo bilioni
18.1 zinatarajiwa kukusanywa kutoka kwenye vyanzo vya vyandani.
Aidha amefafanua
kuwa mapato mengine yatapatikana
kutokana na halmashauri kubuni vyanzo vingine vya mapato sambamba na kuboresha
mikakati ya ukusanyaji wa mapato.
Amefafanua
kuwa utekelezaji wa bajeti hiyo umelenga kutekelaza mradi wa ujenzi wa kituo
cha mabasi cha Mbezi Luis,kuboresha miundombinu ya Dampo,ujenzi wa vyoo vya Umma
na kuhakikisha utoaji wa huduma usiokua na usumbufu kwa wananchi.
Amesema halmashauri pia imepanga kutumia asilimia
65 ya mapato ya ndani sawa na shilingi
bilioni 11.7 kwa ajili ya kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo ,shilingi
bilioni 1.08 zitatumika kwa ajili ya mfuko wa wanawake ,vijana na walemavu.
Akizungumzia
suala la utalii ,Meya Mwita amesema kuwa katika bajeti hiyo zaidi ya bilioni mbili zimetengwa ili
kuboresha sekta ya hiyo ikiwemo kununua mabasi ,kutengeneza na kuboresha
vivutio mbalimbali vilipo jijini hapa.
Ameongeza kua
kuboreshwa kwa sekta hiyo kutaongezea pato la Taifa pamoja na kutoa ajira kwa vijana waliosomea
masuala ya utalii ambao kwa kiasi kikuba hawana ajira.
“ Kama jiji
la Dar es Salaam tumeona ni wakati muafaka sasa wakuweka nguvu kwenye sekta ya
utalii, ambayo kwa kiasi kikubwa kitakuwa ni kivutio kwa wageni kuja hapa
,maanye ni kwamba jiji litapata fedha nyingi kupitia mpango huo” amesema Meya
Mwita.
Imetolewa leo
Februali 24
Na Christina
Mwagala Afisa habari Ofisi ya Meya wa jiji.