TAUSI Entertainments & Talents ni miongoni mwa Kampuni ya Kitanzania iliyoanzishwa Mei, 2016 huko Zanzibar ikiwa na lengo la kusaidia Vijana wa Kitanzania katika kukuza tasnia ya muziki.
Akizungumza na Raia Tanzania, Mkurugenzi wa Kampuni ya Tausi Entertainment & Talent , Tausi Omary Mohamed , amesema lengo la kuanzisha kampuni hiyo, kumetokana na kutaka kusaidia tasnia ya muziki kwa wale watakao kuwa na uhitaji na wenye uwezo ambao kampuni yake itakuwatayari kufanya nao kazi.
Mkurugenzi Tausi Omary Mohamed |
Aidha, Tausi, amesema kuwa kampuni hiyo ilianzishwa ikiwa na wasanii watatu, hadi kufikia Julai mwaka 2017, ilibakiwa na msanii mmoja Chidy Grenade , hivyo aliamua kumsaninisha mwengine Oktoba , 2017 ambaye ni Sharara Tz kutoka Dar es Salaam.
Miongoni mwa wasanii maarufu waliokuwa wakimilikiwa na Tausi Entertainment & Talent ni pamoja na Sultan King pamoja na Berry Black ambapo kwa sasa hawako tena kwenye kampuni hiyo.
Mbali na kujihusisha na maswala ya muziki lakini kampuni hiyo imeanzisha program ya Tausi Entertanment Search ikiwa na lengo la kusaka vipaji kama vile vichekesho, uimbaji pamoja na ku dansi (shake).
Programu hiyo ya Talent Search inafanyika mara moja kila mwaka huku pambano jengine likitarajiwa kufanyika mwakani Agosti 2018 Zanzibar.
“ Mimi sikuanzisha kampuni kwa ajili ya kushindana, najua zipo kampuni nyingi zinazosimamia wasanii, lakini lengo ni kusaidia Vijana hususani Zanzibar katika kuwapatia ajira ,na kufikia malengo yangu, hata kama zitaongezeka siku hadi siku sina shida maana kila mtu ana malengo yake.”Amesema Tausi
Huyu ni mwanamke aliyethubutu kutoa alichonacho na kuona wengine wakinufaika nacho, lakini aliendelea kushikilia msimamo wake wa kuhamisha Tausi Talent Search Dar es Salaam baada ya kukamilisha mipango yake.
Miongoni mwa mafanikio aliyoyapata ni pamoja na kuwa na Mnyororo mkubwa wa watu wanaosaidiana katika kufikia malengo yake kama vile mitandao ikiwamo TV, Magazine na Redio
Kuhusu kuchukua wasanii mkubwa na wanae, amesema lengo lake ni kutaka kushirikiana nae pale atakapo wahitaji wasanii hao kufanya nao kazi na wala sio kuwaiba.
Hivi sasa yupo katika mpango wa kuhakikisha anakuwa na Vijana wenye vipaji wengi watakao weza kuutangaza vema muziki wa Tanzania kimataifa kama ilivyo kwa wasanii wengine kama viele Ali Kiba na Diamond wanaoonekana kuliteka soko la Afrika Mashariki kwa sasa.
Aidha, Mkurugenzi Tausi amesema kuwa Vijana wanaochipukia wasiwe na haraka ya kuwa star wanatakiwa wafanye kazi zenye ubora na wawe na nidhamu na subira katika kufikia malengo.
Post a Comment