Hatua hiyo inafuatia baada ya Sugu na mwenzake Emanuel Masonga ambaye ni katibu mkuu wa Chadema kanda ya nyanda za juu kusini kumkataa hakimu huyo.Wanakabiliwa na kesi ya uchochezi na wamerudishwa rumande hadi Februari 8, 2018.
Hata hivyo mbunge Sugu ameomba wiki mbili za kupanga kujitetea
Sababu ya kumnyima dhamana mshtakiwa Sugu na mwenzake ni hofu ya mshtakiwa kutohudhuria mahakamani hapo mara kwa mara ili hali Hakimu anataka kesi hiyo iishe mapema.
SABABU TATU ALIZOTOA SUGU KUMKATAA HAKIMU
“Mheshimiwa Hakimu dhamira yangu imenituma nikukatae wewe Hakimu, kwa sababu tatu zifuatazo…
1. Sijawahi kuona hakimu yuko bias kama wewe ikiwemo kuninyima dhamana bila sababu za msingi kisheria na kikatiba.
2. Jana nilishuhudia kielelezo cha tape recoder kikitoka mikononi mwa Mwanasheria wa serikali kuja mahakamani kinyume cha sheria na hoja za wakili wangu Mwabukusi ulizipinga.
3. Kwenye mabishano umekiri kesi hii imekupa shida, mi ni Mkristo sitaki upate shida naomba nikukatae ili aje hakimu mwingine aendeshe kesi kwa uhuru bila kupata shida na mazingira ya shinikizo lolote lile.
Kwa sababu hizo naomba nikukatae and I’m very serious about it, nakukataa”
Post a Comment