Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Latest Post

Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Maulana Sheikh Hemed Jalala akiongea na Waandishi wa Habri katika Kikao cha kuzungumzia kumbukumbu ya Kuzaliwa Mtoto wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), ambae ni Bi,Fatma Zahra (a.s), kulia kwake ni Sheikh Muhammad Abdu.
Tarehe kama ya leo (20, Jamadal Akhirah,1439 sawa na 09-03-2018) leo amezaliwa bint wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ambae ni Bibi Fatma Zahra (a.s),Mtoto huyu au Bint huyu au Mama huyu kwasababu ya daraja lake alilokuwanalo ndani ya Uislamu, Viongozi wa Dini ya Kiislamu, Masheikh wakaitangaza siku ambayo aliozaliwa Mama huyu ni siku ya Mwanamke wa Kiislamu Duniani,siku hiyo tumekuwa tukiikumbuka kila mwaka, siku aliyozaliwa mama huyu ni siku ya Mwanamke wa Kiislamu Duniani kote.
 
Yanayotufanya tumkumbuke mama huyu, kwanza ni mwanamke mtakatifu, pili ni mwanamke aliegubikwa na sifa nyingi nzurinzuri zilizojaa ndani ya kitabu kitakatifu cha Quran, lakini vilevile mama huyu amegubikwa na sifa nyingi kutoka kwenye kinywa cha Mtume Muhammad (s.a.w.w), Mama huyu alikuwa kipenzi cha mtume Muhammad (s.a.w.w).

Tunapozungumza Wanawake watakatifu kama vile mama Asia, kama vile mama Khadija, kama vile Mariam aliemzaa Nabii Issa / Yesu (a.s), tunamzungumza vilevile Bi Fatma Zahra ni katika gurupu la wanawake hao.

Bi Fatma Zahra alikuwa na Elimu, Maarifa bila shaka tunahitajia Mama zatu na Dada zetu leo wawe na maarifa na Elimu nzuri,Dunia leo inatafuta maadili mema, dunia leo inachangamoto kubwa ya kupoteza maadili yao, ambayo Mungu amewaumba nayo, Bi Fatma Zahra (a.s) alisifika na maadili mema katika Nyanja zote, pia alisifika na Ukarimu.

Tunaamini vilevile Nyumba ya watu wenye Imani, Nyumba ya Watu wanaomtambua Mungu, Nyumba ya watu wenye hofu na Mungu, Nyumba hiyo inakuwa nyumba salama, bila shaka nyumba inapokuwa salama, jamii inakuwa salama, jamii inapokuwa salama Taifa nalo linakuwa salama, kwahivyo Nyumba ya Bi Fatma Zahra (a.s) ni Myumba ya Mwanamke ambae alikuwa akimuabudu Mungu.

Katika siku hii ya Mwanamke wa Kiislamu Duniani napenda nigusie jambo zima la haki za Mwanamke ndani ya Uislamu, ziko baadhi ya fikra zinazoona Uislamu haukumpa Mwanamke haki zake, laa, napenda nisieme katika siku hii ya Mwanamke wa Kiislamu Duniani kwa kukumbuka kuzaliwa kwa Binti ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), niseme yakwamba Uislamu unamuangalia Mwanamke na Uislamu unampa Mwanamke haki zake zote.

Mwanamke anayohaki ya kurithi ndani ya Uislamu, Dini ya Uislamu inampa Mwanamke haki ya Kumiliki kama vile mwanaume anavyomiliki,Haki ya kufanya Kazi,Haki ya kuendesha gari,haki ya usawa na haki zingine ambazo ziko kwa mujibu wa dini ya Uislamu.

Katika siku ya leo siku ya Mwanamke wa Kiislamu Duniani napenda nizungumzie jambo la kuvaa sitara au hijabu, Hijabu au Sitara katika Uislamu hakiwekwa kama jambo la kumdhalilisha mwanamke laaa, sitara au hijabu ambayo yakuigwa kutoka kwa Bint ya Mtume Fatma Zahra (a.s), Sitara au hijabu yake haikumzuia kufanya kazi, sitara yake haikumzuia kufanya mambo ya Kiislamu, 


sitara yake haikumzuia kuingia darasani kusomesha, sitara yake haikumfanya aache kutoa Hotuba mbele ya Maswahaba wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), kwa hivyo sitara au hijabu ni kitu cha kumsitiri mwanamke, ni heshima kwa mwanamke,ni adabu kwa mwanamke, bali mwanamke amekuwa na dhamani kubwa kwa sababu ya sitara yake.

Mwisho napenda kugusia jambo muhimu sana ambalo ni jambo la kuigwa kutoka kwa binti ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) ambae ni Fatma Zahra (a.s), Jambo la Malezi, Mwanamke moja ya kazi aliyokuwa nayo ni kulea jamii iliyokuwa njema,Kama tunataka tutengeneze jamii ya Wachamungu, jamii ya wakweli, jamii ya watu wenye imani, jamii ya watu wanaopenda kusaidiana, ni lazima hili lianze katika ngazi ya familia, na hakuna analolitengeneza hilo isipokuwa ni Mama.

Mama ndio mwenye nafasi ya kutengeneza jamii yenye wakweli, mama ndio mwenye nafasi ya kutengeneza wabunge ambao kesho watatuwakilisha katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ahadi zao walizotuahidi na kuzitekeleza, kwasababu gani, Mwakilishi huyu ameleleka katika nyumba ambayo inapoahidi inatekeleza, 


kama tunataka kutengeneza Wachapa kazi ambao hawachoki, kama tunataka kuunda watu ambao ni hapa kazi hilo linarudi katika ngazi ya familia na unaona Bi Fatma Zahra (a.s) angalia alivyowalea na kuwatengeneza Watoto wake kama Imam Hassan (a.s), Imam Hussein (a.s) na Bi Zainab (a.s).

Bi.Fatma Zahra ni Mtoto wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), Mama yake ni Bi.Khadija, Mume wake ni Sayyidina Ali (a.s), Watoto wake ni Imam Hassan (a.s), Imam Hussein (a.s) na Bi.Zainab (a.s), Babu yake ni Abdallah, Bibi yake ni Amina.

Imetolewa na
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania
Maulana Sheikh Hemed Jalala

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas  akiwahutubia wajumbe wa baraza kuu la umoja wa wanawake manispaa ya Iringa na kusema kuwa bado anaumizwa na matokeo ya ubunge wa jimbo la Iringa mjini baada ya wapinzani kushinda kwa kishindo mwaka 2015 kwa ni kitendo ambacho hakukitegemea.
Mwenyekiti wa umoja wa wanawake UWT manispaa ya Iringa Ashura jongo akimtoa hofu MNEC Salim Asas juu ya kukomba jimbo baada ya kulipoteza kwa kusalitia mwaka 2015 
 Baadhi ya wageni waliokuwa wamealikwa kwenye baraza hilo kwa ajili ya kujifunza na kutoa mapendekezo pale wanapopata nafasi
 Baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi mkoani Iringa walipokuwa wakimsikiliza kwa umakini mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas alipokuwa anatoa ya moyo kuhusu kushindwa katika uchaguzi wa mwaka 2015

Na Fredy Mgunda,Iringa.

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas bado anaumizwa na matokeo ya ubunge wa jimbo la Iringa mjini baada ya wapinzani kushinda kwa kishindo mwaka 2015 kwa ni kitendo ambacho hakukitegemea.

Akizungumza wakati wa baraza la UWT manispaa  ya Iringa Asas alisema kuwa usaliti ulifanywa katika uchaguzi wa mwaka 2015 umekuwa ukimuumiza hadi sasa na kitendo anafikiri kitadumu moyoni mwake hata kwa miaka kumi kwakuwa bado anakumbuka mara kwa mara.

“Naombeni niongee ukweli kitendo kilichofanywa na wanaccm wa manispaa ya Iringa katika uchaguzi wa mwaka 2015 kilikuwa kitendo ambacho ni usaliti mkubwa ambao unaumiza sana kichwa changu” alisema Asas

Asas alisema kuwa uchaguzi huo kulikuwa na wanaccm wengi ambao mchana walikuwa ccm na usikuwa walikuwa kwa wapinzani hivyo lazima tuondoe usaliti kwenye chama bila hivyo tutaendelea kushindwa kila siku.

“Unakuta rasilimali zilizokuwa zinatolewa na  chama cha mapinduzi zote zinatumika kwa wapinzani kuhakikisha wanaiangusha ccm,sasa hicho kitu ndio ambacho kinaniumiza sana kichwa hadi hii leo” alisema Asas

Asas aliutaka umoja wa wanawake (UWT) manispaa ya Iringa kufanya kazi kwa umoja unatakiwa na kuhakikisha kuwa ccm inakuwa ila na isiyo na makundi ili kufika mwaka wa uchaguzi wanashinda kwa kishindo kwa kutumia umoja wao.

“Nawaombe muutunze umoja huu ambao sasa mnao hadi kipindi cha uchaguzi wowote ule ambao upo mbele yetu na kuhakikisha kuwa tunashinda kila chaguzi kwa kishindo kwa kuwa nyie akina mama ndio huwa mnakula ambazo haziamishiki” alisema Asas

Kwa upande wake mwenyekiti wa UWT manispaa ya Iringa Ashura jongo alimuhakikishia MNEC Salim Asas kuwa kosa lilofanyika mwaka 2015 halitajirudia tena katika chaguzi yoyote ambayo itakuwa inafanyika katika manispaa ya Iringa.

“Ndugu MNEC kwa kweli tumejifunza na tunajutia kitu kilichofanyika mwaka 2015 hivyo tunakuhadi kuwa kwenye umoja wetu wa wanawake Manispaa ya Iringa hakitaa tokea kama kilivyotokea,na tutashinda chaguzi zetu kwa kuwa kila mtu anaumia na kilichotokea mwaka 2015” alisema Jongoo

Jongoo alimshukuru MNEC kwa kurudisha umoja kwa wanaccm mkoa wa Iringa kwa kuwa anafanya kazi kubwa kuhakikisha kila kitu kinakuwa kama kinavyokusudiwa na kuhakikisha umoja ambao umetengenezwa na viongozi wapya unadumu hadi watakapomaliza uchaguzi.

“Mheshimiwa MNEC umoja ambao tunao hivi sasa tunatakiwa kuulinda na kuudumisha hadi kipindi cha chaguzi zote na kuhakikisha kuwa ccm inashinda kwa kushinda na kuendelea kuwa ngoja ya chama hicho kama ilivyokuwa hapo awali” alisema Jongoo


MBUNGE wa jimbo la Mtama kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM,  Nape Nnauye amelaani mfumo wa baadhi ya viongozi wanaobadili utaratibu wa ukomo wao wa utawala na kujiongezea miaka au mihula ya kutawala.

Nape amefananisha kitendo hicho kuwa ni sawa na ushetani na kuwataka vijana wa Kiafrika kupambana  kupinga mfumo huo kwa kile alichodai kuwa  unakandamiza demokrasia.

“Huu ulevi wa baadhi ya viongozi wa Afrika kutamani na kubadili ukomo wa wao kuwa madarakani ni ushetani na lazima upingwe kwa nguvu zote hasa na vijana kabla utaratibu huu haujaota mizizi na kusambaa! Hii ni zaidi ya kansa“amenena  Nape Nauye kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Baadhi ya nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Uganda na Rwanda tayari nchi hizo zimebadili mfumo wa ukomo wa urais madarakani ambapo Rais atahudumu kwa miaka 7 na Uganda wamefuta kabisa hadi ukomo wa umri wa Rais kustaafu.





Image result for MEYA WA JIJI LA DAR MWITA
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ,aliyesimama, kulia ni Mkurugenzi wa jiji Sipora Liana,  kushoto ni Naibu Meya wa jiji Mussa Kafana
MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam , Isaya Mwita leo amewasilisha mpango wa bajeti wa mwaka 2018 hadi 2019 ambapo jumla ya shilingi bilioni 75.2 zitatumika kwa mwaka huo.

Hata hivyo mpango huo umepitishwa kwa kauli moja na Madiwani wote wa halmashauri hiyo huku wakimpongeza kwa  kusema kuwa jiji limepata Meya anayejali maslahi ya maendeleo katika halmashauri hiyo.

 Halmashauri hiyo imeandaa mpango huo kwa kuzingatia taratibu zinazotakiwa kufuatwa na mamlaka za Serikali za mitaa katika utayarishaji wa makadirio ya mapato na matumizi ya  mwaka wa fedha wa 2018 na 2019.

Akizungumzia  mpango huo kwenye mabaraza la Madiwani na waandishi wahabari , Meya Mwita amesema kuwa jiji limekadiria kukusanya na kutumia shilingi bilioni 75.2 ambapo itatokana kwenye  vyanzo mbalimbali vya mapato ikiwemo bilioni 18.1 zinatarajiwa kukusanywa kutoka kwenye vyanzo vya vyandani.

Aidha amefafanua kuwa mapato mengine  yatapatikana kutokana na halmashauri kubuni vyanzo vingine vya mapato sambamba na kuboresha mikakati ya ukusanyaji wa mapato.

Amefafanua kuwa utekelezaji wa bajeti hiyo umelenga kutekelaza mradi wa ujenzi wa kituo cha mabasi cha Mbezi Luis,kuboresha miundombinu ya Dampo,ujenzi wa vyoo vya Umma na kuhakikisha utoaji wa huduma usiokua na usumbufu kwa wananchi.

 Amesema halmashauri pia imepanga kutumia asilimia 65 ya mapato  ya ndani sawa na shilingi bilioni 11.7 kwa ajili ya kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo ,shilingi bilioni 1.08 zitatumika kwa ajili ya mfuko wa wanawake ,vijana na walemavu.

Akizungumzia suala la utalii ,Meya Mwita amesema kuwa katika bajeti hiyo  zaidi ya bilioni mbili zimetengwa ili kuboresha sekta ya hiyo ikiwemo kununua mabasi ,kutengeneza na kuboresha vivutio mbalimbali vilipo jijini hapa.

Ameongeza kua kuboreshwa kwa sekta hiyo kutaongezea pato la Taifa  pamoja na kutoa ajira kwa vijana waliosomea masuala ya utalii ambao kwa kiasi kikuba hawana ajira.

“ Kama jiji la Dar es Salaam tumeona ni wakati muafaka sasa wakuweka nguvu kwenye sekta ya utalii, ambayo kwa kiasi kikubwa kitakuwa ni kivutio kwa wageni kuja hapa ,maanye ni kwamba jiji litapata fedha nyingi kupitia mpango huo” amesema Meya Mwita.

Imetolewa leo Februali 24

Na Christina Mwagala Afisa habari Ofisi ya Meya wa jiji.

Baraza la Mitihani la Tanzania limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) leo Januari 30, 2018 ambapo kiwango cha ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 7 ukilinganisha na mwaka jana 2016.

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde ametangaza matokeo hayo leo jijini Dar es Salaam na kusema ufaulu kwa wanafunzi umeongezeka kwa asilimia 7 ukilinganisha na matokeo ya mwaka jana.

"Jumla ya Watahiniwa 287,713 ambao sawa na asilimia 77.09%  kwa shule za kawaida na vituo vya kujitegemea wamefaulu ambao katika ya hao wasichana wapo 143,728 sawa na asilimia 75.21% wakati wavulana wapo 143,985 sawa na asilimia 79.06%. Mwaka jana wanafunzi waliofaulu mitihani ya kidato cha nne walikuwa 277,283 ambao ni asilimia 70.09% hivyo ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 7" alisema Msonde

Mbali na hilo Msonde aliweza kuweka wazi kuwa jumla ya wanafunzi 265 wamebainika kufanya udanganyifu mbalimbali katika mitihani hiyo ambayo ilianza kufanyika Oktoba 30, 2016 mpaka Novemba 17, 2016


 Shule 10 kitaifa ambapo shule iliyoongoza  inatoka Mkoani  Mbeya.shule hizo ni 
TOP 10 YA SHULE BORA.
1. St. Francis Girls ya Mbeya
2. Feza Boys ya Dar es salaam
3. Kemebos ya Kagera 
4. Bethel Sabs Girls ya Iringa 
5. Anwarite Girls ya Kilimanjaro 
6. Marian Girls Pwani 
7. Canossa ya Dar es salaam 
8. Feza Girls ya Dar es salaam 
9. Marian Boys ya Pwani 
10. Shamsiye Boys ya Dar es salaam 
TOP 10 YA SHULE ZA MWISHO KITAIFA
10. Mtule ya Kusini Unguja
9. Nyeburu ya Dar es salaam
8. Chokocho ya Kusini Pemba
7. Kabugaro ya Kagera
6. Mbesa ya Ruvuma
5. Furaha ya Dar es salaam
4. Langoni ya Mjini Magharibi
3. Mwenge S.M.Z ya Mjini Magharibi
2. Pwani Mchangani ya Kaskazini Unguja
1. Kusini ya Kusini Unguja

MAAMUZI YA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI KUHUSU RUFAA MOJA YA MGOMBEA UBUNGE NA RUFAA TANO ZA WAGOMBEA UDIWANI

Kwa kuzingatia masharti ya Kifungu cha 40(6) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, ikisomwa pamoja na Kanuni za 34 na 35 za Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2015, Tume ilipokea Rufaa moja (1) kutoka kwa Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) akipinga maamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo kuhusu pingamizi alilomuwekea Mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Aidha, kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 44 (5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, ikisomwa pamoja na Kanuni za 28 na 29 za Kanuni za Serikali za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani) za mwaka 2015, Tume ilipokea Rufaa tano (5) za Wagombea  Udiwani  kutoka katika Kata ya Isamilo – Halmashauri ya Jiji la Mwanza, wakipinga Maamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo.  Rufaa tatu (3) ni za wagombea walioondolewa kwenye kugombea ili warejeshwe na Rufaa mbili (2) zinaomba Tume itengue uteuzi wa mgombea Udiwani aliyeteuliwa katika Kata hiyo.

Katika kikao chake cha kawaida kilichofanyika tarehe 26 Januari 2018 siku ya Ijumaa, Tume ilipitia Rufaa hizo na kuamua kama ifuatavyo:

Mosi, kuhusu Rufaa ya Mgombea Ubunge, Tume imekubaliana na maamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi na hivyo Mgombea aliyekatiwa Rufaa wa CHADEMA anaendelea kuwa mgombea wa Ubunge Jimbo la Kinondoni.

Pili, kuhusu Rufaa za Wagombea Udiwani Kata ya Isamilo katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza, kupinga kuondolewa kugombea Udiwani katika Kata hiyo, Tume imewarejesha kuwa Wagombea Udiwani wawili wa vyama vya CHADEMA na CUF.

Tatu, Tume imekubaliana na maamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi ya kumuondoa katika orodha ya wagombea Udiwani mgombea wa Chama cha UDP. Hivyo hatakuwa mgombea katika kata hiyo

Nne, Tume imekataa rufaa mbili zilizokuwa zinapinga uteuzi wa mgombea wa CCM aliyeteuliwa katika Kata hiyo na hivyo, mgombea wa CCM anaendelea kugombea Udiwani katika kata husika.

Taarifa rasmi za maamuzi ya Tume zimetumwa kwa Wasimamizi wa Uchaguzi ili wawapatie wahusika maamuzi hayo.

Kailima, R.K
MKURUGENZI WA UCHAGUZ

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget