MBUNGE wa jimbo la Mtama kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM, Nape Nnauye amelaani mfumo wa baadhi ya viongozi wanaobadili utaratibu wa ukomo wao wa utawala na kujiongezea miaka au mihula ya kutawala.
Nape amefananisha kitendo hicho kuwa ni sawa na ushetani na kuwataka vijana wa Kiafrika kupambana kupinga mfumo huo kwa kile alichodai kuwa unakandamiza demokrasia.
“Huu ulevi wa baadhi ya viongozi wa Afrika kutamani na kubadili ukomo wa wao kuwa madarakani ni ushetani na lazima upingwe kwa nguvu zote hasa na vijana kabla utaratibu huu haujaota mizizi na kusambaa! Hii ni zaidi ya kansa“amenena Nape Nauye kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Baadhi ya nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Uganda na Rwanda tayari nchi hizo zimebadili mfumo wa ukomo wa urais madarakani ambapo Rais atahudumu kwa miaka 7 na Uganda wamefuta kabisa hadi ukomo wa umri wa Rais kustaafu.
Post a Comment