Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

March 2018

Ujumbe wa Rais mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete katikati ya wiki hii uliteka mtandao wa kijamii wa Twitter na kusambaa kwenye Whatsapp, akionesha sehemu ya maisha yake baada ya urais.

Dkt. Kikwete ambaye alihamia Msoga mkoani Pwani kwa ajili ya mapumziko baada ya kutoka Ikulu, aliwepa picha kadhaa akiwa anakula chakula kwenye sahani na bakuli moja na wazee ambao walihudhuria msiba wa baba yake mdogo, Said Lumaliza katika kijiji cha Msigi.

“Tukila chakula na ndugu zangu msibani kwa baba yangu mdogo marehemu Said Lumaliza(1917-2018) katika kijiji cha Msigi karibu na Msoga. Hii ndiyo fahari ya maisha ya kustaafu.!” alitweet mara mbili kwa Kiswahili na Kiingereza, Machi 8.

Watumiaji wa mtandao huo ambao wengine walitoka nje ya nchi walisifu maisha ya kujishusha ya rais huyo mstaafu na kueleza kuwa ni viongozi wachache waliokuwa na cheo kama chake ambao wanaweza kurejea kwenye maisha ya aina hiyo.

“Kuna Maisha baada ya kustaafu. Itafika muda ulinzi kamili itakua ni yale uliyo wafanyia watu na ndicho nilicho jifunza hapo,” aliandika Samuel Isaya.

“Wewe ni rais wa mfano kwa Afrika pamoja na kuwa na mapungufu yako kama binadamu. Hongera sana mhe Mungu akutangulie ktk muda wote wa Maisha yako,” Zakayo Sarwatt.

“It’s very rare to see a former African president from any African country spending time with low class citizens,” aliandika Hermescash. Kwa tafsiri isiyo rasmi, “Ni mara chache sana utaona marais wa zamani Afrika kutoka nchi yoyote wakitumia muda wao na watu wa hali ya chini.”

Ikiwa kila tarehe 8 ya mwezi machi nchi zote duniani zinasherekea siku ya mwanamke duniani kwa kufanya mambo mbalimbali ikiwa ni kuenzi na kupongeza michango mbalimbali iliyotolewa ama inayoendelea kutolewa na wanawake.
Mkurugenzi mtendaji wa Lecri Consult Bi. Edna Kamaleki akitoa ufafanuzi wa jambo fulani kwa wageni waalikwa, katika maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani mapema leo jijini Dar es salaam.

Katika kuhakikisha siku hii inaenziwa vyema mashirika mawili yaliyoamau kuungana na kufanya kitu kizuri kwa siku hii nayo ni Lecri Consult pamoja na Hodari Tanzania.

Na kwa mujibu wa kauli mbiu ya kimataifa ya mwaka huu inayosema “Chagiza maendeleo yako” hii ikijaribu kuwapa msukumo wanawake katika kujitafutia maendeleo yao wenyewe.

Mashirika hayo yameenzi siku hii kwa kufanya kongamano na wanawake pamoja na wanaume ili kuwajuza mambo mbalimbali ikiwa  ni haki na wajibu wao kama wanawake na pia kuwapa mwanga wanaume nini cha kufanya ili kupunguza vitendo vya ukatili wa wanawake na watoto.

Katika kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa British Council jijini Dar es salaam liliudhuliwa na maafisa mbalimbali kutoka serikalini na asasi za kiraia ili kuweza kubadilishana uzoefu na kuelimishana mengi kuhusu haki zao kama wanawake.

Lakini pia katika kongamano hilo waliweza kuwaonyesha kwa kiasi gani wanawake wanaweza kuwa wamiliki wa ardhi yao wenyewe kwa mujibu wa sharia na sio kila siku kuwa nyuma ya mwamvuli wa wanume.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hodari Tanzania Bi. Emelda Lulu Urio akiongea na wageni waalikwa waliohudhuria tafrija ya maadhimisho ya siku ya Mwanamke duniani iliyofanyika British Council jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hodari Tanzania Bi. Emelda Lulu Urio akiendelea kutoa elimu kwa wanawake na wanaume waliofika katika tafrija hiyo.
Mkurugenzi wa LAPF kanda ya Dar es salaam Bi. Amina Kassim kiwaelezea wageni waalikwa fursa zinazopatikana katika shirika hilo na kwa kiasi gani LAPF inawajali wanawake kwa kuwapa huduma stahiki kwa gharama nafuu.
Mkurugenzi wa LAP kanda ya Dar es salaam Bi. Amina Kassim akiongea na wageni waalikwa.

Afisa Ustawi Jamii wa wilaya ya Ilala Bi. Francisca Makoye akielezea wao kama ustawi wa jamii nini majukumu yao na wanafanya nini ili kuwakomboa wanawake dhidi ya ukatili wanaofanyiwa na wanaume zao au jamii kwa ujumla.

Mkurugenzi wa Benki ya NMB tawi la Samora Bw. Sospeter Magesse akielezea kwa namna gani benki hiyo inafanya kazi kwa ukaribu kwa kushirikiana na wanawake kote nchini.
Maafisa kutoka mashirika mbalimbali ya kiserikali na binafsi wakifuatilia kwa umakini mawasilisho yanayotolewa na wawezeshaji.

Washiriki wa maadhimisho wakiwa katika picha ya pamoja.

    ANGALIA VIDEO HII KUJUA MENGI YALIYOTOKEA..
                     

Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Maulana Sheikh Hemed Jalala akiongea na Waandishi wa Habri katika Kikao cha kuzungumzia kumbukumbu ya Kuzaliwa Mtoto wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), ambae ni Bi,Fatma Zahra (a.s), kulia kwake ni Sheikh Muhammad Abdu.
Tarehe kama ya leo (20, Jamadal Akhirah,1439 sawa na 09-03-2018) leo amezaliwa bint wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ambae ni Bibi Fatma Zahra (a.s),Mtoto huyu au Bint huyu au Mama huyu kwasababu ya daraja lake alilokuwanalo ndani ya Uislamu, Viongozi wa Dini ya Kiislamu, Masheikh wakaitangaza siku ambayo aliozaliwa Mama huyu ni siku ya Mwanamke wa Kiislamu Duniani,siku hiyo tumekuwa tukiikumbuka kila mwaka, siku aliyozaliwa mama huyu ni siku ya Mwanamke wa Kiislamu Duniani kote.
 
Yanayotufanya tumkumbuke mama huyu, kwanza ni mwanamke mtakatifu, pili ni mwanamke aliegubikwa na sifa nyingi nzurinzuri zilizojaa ndani ya kitabu kitakatifu cha Quran, lakini vilevile mama huyu amegubikwa na sifa nyingi kutoka kwenye kinywa cha Mtume Muhammad (s.a.w.w), Mama huyu alikuwa kipenzi cha mtume Muhammad (s.a.w.w).

Tunapozungumza Wanawake watakatifu kama vile mama Asia, kama vile mama Khadija, kama vile Mariam aliemzaa Nabii Issa / Yesu (a.s), tunamzungumza vilevile Bi Fatma Zahra ni katika gurupu la wanawake hao.

Bi Fatma Zahra alikuwa na Elimu, Maarifa bila shaka tunahitajia Mama zatu na Dada zetu leo wawe na maarifa na Elimu nzuri,Dunia leo inatafuta maadili mema, dunia leo inachangamoto kubwa ya kupoteza maadili yao, ambayo Mungu amewaumba nayo, Bi Fatma Zahra (a.s) alisifika na maadili mema katika Nyanja zote, pia alisifika na Ukarimu.

Tunaamini vilevile Nyumba ya watu wenye Imani, Nyumba ya Watu wanaomtambua Mungu, Nyumba ya watu wenye hofu na Mungu, Nyumba hiyo inakuwa nyumba salama, bila shaka nyumba inapokuwa salama, jamii inakuwa salama, jamii inapokuwa salama Taifa nalo linakuwa salama, kwahivyo Nyumba ya Bi Fatma Zahra (a.s) ni Myumba ya Mwanamke ambae alikuwa akimuabudu Mungu.

Katika siku hii ya Mwanamke wa Kiislamu Duniani napenda nigusie jambo zima la haki za Mwanamke ndani ya Uislamu, ziko baadhi ya fikra zinazoona Uislamu haukumpa Mwanamke haki zake, laa, napenda nisieme katika siku hii ya Mwanamke wa Kiislamu Duniani kwa kukumbuka kuzaliwa kwa Binti ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), niseme yakwamba Uislamu unamuangalia Mwanamke na Uislamu unampa Mwanamke haki zake zote.

Mwanamke anayohaki ya kurithi ndani ya Uislamu, Dini ya Uislamu inampa Mwanamke haki ya Kumiliki kama vile mwanaume anavyomiliki,Haki ya kufanya Kazi,Haki ya kuendesha gari,haki ya usawa na haki zingine ambazo ziko kwa mujibu wa dini ya Uislamu.

Katika siku ya leo siku ya Mwanamke wa Kiislamu Duniani napenda nizungumzie jambo la kuvaa sitara au hijabu, Hijabu au Sitara katika Uislamu hakiwekwa kama jambo la kumdhalilisha mwanamke laaa, sitara au hijabu ambayo yakuigwa kutoka kwa Bint ya Mtume Fatma Zahra (a.s), Sitara au hijabu yake haikumzuia kufanya kazi, sitara yake haikumzuia kufanya mambo ya Kiislamu, 


sitara yake haikumzuia kuingia darasani kusomesha, sitara yake haikumfanya aache kutoa Hotuba mbele ya Maswahaba wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), kwa hivyo sitara au hijabu ni kitu cha kumsitiri mwanamke, ni heshima kwa mwanamke,ni adabu kwa mwanamke, bali mwanamke amekuwa na dhamani kubwa kwa sababu ya sitara yake.

Mwisho napenda kugusia jambo muhimu sana ambalo ni jambo la kuigwa kutoka kwa binti ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) ambae ni Fatma Zahra (a.s), Jambo la Malezi, Mwanamke moja ya kazi aliyokuwa nayo ni kulea jamii iliyokuwa njema,Kama tunataka tutengeneze jamii ya Wachamungu, jamii ya wakweli, jamii ya watu wenye imani, jamii ya watu wanaopenda kusaidiana, ni lazima hili lianze katika ngazi ya familia, na hakuna analolitengeneza hilo isipokuwa ni Mama.

Mama ndio mwenye nafasi ya kutengeneza jamii yenye wakweli, mama ndio mwenye nafasi ya kutengeneza wabunge ambao kesho watatuwakilisha katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ahadi zao walizotuahidi na kuzitekeleza, kwasababu gani, Mwakilishi huyu ameleleka katika nyumba ambayo inapoahidi inatekeleza, 


kama tunataka kutengeneza Wachapa kazi ambao hawachoki, kama tunataka kuunda watu ambao ni hapa kazi hilo linarudi katika ngazi ya familia na unaona Bi Fatma Zahra (a.s) angalia alivyowalea na kuwatengeneza Watoto wake kama Imam Hassan (a.s), Imam Hussein (a.s) na Bi Zainab (a.s).

Bi.Fatma Zahra ni Mtoto wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), Mama yake ni Bi.Khadija, Mume wake ni Sayyidina Ali (a.s), Watoto wake ni Imam Hassan (a.s), Imam Hussein (a.s) na Bi.Zainab (a.s), Babu yake ni Abdallah, Bibi yake ni Amina.

Imetolewa na
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania
Maulana Sheikh Hemed Jalala

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget