Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

KIDATO CHA SITA, WALIMU KUFANYA MTIHANI KESHO

Image result for katibu mtendaji baraza la mitihani tanzania
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania Dk. Charles Msonde

NA MWANDISHI WETU, DAR

BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza kufanika kwa Mitihani ya kidato cha sita na ualimu ambapo itafanyika kuanzia kesho (leo)  7 hadi 25 Mei 2018 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam jana ,  Katibu Mkuu wa Baraza hilo Dokta Charles Msonde alisema kuwa jumla ya watahiniwa 87643 wamesajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha sita mwaka huuu  ambapo kati yao  wa shule ni 77222 na  wa kujitegemea ni 10421.

Dk. Msonde alifafanua kuwa  katika katika kuelekea kufanya mtihani huo, jumla ya Shule za Sekondari zitakazo fanyika mtihani huo ni 674,  vituo vya watahiniwa wa kujitegemea  231 huku vyuo vya ualimu vikiwa 125 kwa Tanzania bara na Zanzibar

Aliongeza kuwa  kati ya watahiniwa wa shule 77222 waliosajiliwa kufanya mtigahi huo , wavulana  ni 45105 sawa na  asilimia 58.41,wasichana  32117 sawa na asilimia 41.59.

Aidha aliongeza kuwa  “ katika  watahiniwa hao,kuna wenye ulemavu waskuona, ambapo wao pia wanahaki ya kufanya mtihani huo, na jula yao kwa mwaka huu wapo 12 na wale  wenye uono hafifu wapo 56 ambapo maandishi ya karatasi zao hukuzwa” alifafanua Dk. Msonde.

Hata hivyo kwa upande wa mtihani wa ualimu jumla ya watahiniwa ni 7422 wamesajiliwa kufanya kozi za ualimu kwa ngazi ya  cheti  na Stashahada ambapo kati yao wavulana  ni 4931 na wasichana  ni 2491.

Dk. Msonde alieleza kuwa , idadi ya watahiniwa waliosajiliwa katika ngazi ya Cheti ni 5234 ambapo wavulana ni 3204 na  wasichana  2030, huku  watahiniwa waliosajiliwa kwa  ngazi ya Stashahada ni 2188 ,wavulana  1727 na  wasichana 464.

 

 Akizungumzia maandalizi ya mtihani huo alisema kuwa  yamekamilika kwa asilimia 100 nchi nzima ikiwa ni pamoja na kusambazwa Mitihani hiyo kwa wahusika, vitabu vya kujibia sambamba na  nyaraka zote muhimu katika mikoa  Tanzania Bara na Zanzibar.

Sambamba na hilo, aliwakumbusha wananchi kuthamini na kutambua umuhimu wa wanafunzi kufanya Mitihani hiyo kwakuwa  ndio daraja la pekee la kufikia mafanikio yao.

"Pia nitumie fursa hii kutoa wito kwa kamati za Mitihani ,Halmashauri,  Manispaa na Majiji yote kuhakikisha kuwa taratibu za Mitihani zote zinazingatiwa,   nawaonya mjiepushe na mianya ya rushwa kwani Baraza hatutasita kuwachukulia hatua stahiki” alisistiza Dk. Msonde.

Aliongeza kuwa “ wito wangu pia kwa wananchi tunaomba ushirikiano katika kipindi hiki, unaruhusiwa kutoa taarifa za kiuhalifu ama uvunjwaji wa sheria za Mitihani na kuripoti sehemu husika. "


Mwishooo.

Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget