Benki ya Exim nchini imefanya hafla fupi ya futuru (Iftar) pamoja na wateja wake huku ikibainisha iko katika mchakato kupunguza riba ili kuwawezesha wateja kunufaika na mikopo na huduma nyingine zitolewazo na benki hiyo.
Hatua hiyo imekuja hivi karibuni baada ya tamko la Serikali kupitia Waziri wa Fedha na Mipanga, Philip Mipango lililoyataka taasisi za kibenki kupunguza riba za mikopo kwa wateja ili waweze kunufaika.
Kaimu Mkurugenzi wa benki ya Exim Bw. Selemani Ponda akiongea na waandishi wa habari mara baada ya futari iliyofanyika hoteli ya New Afrika mapema jana jijini Dar es salaam.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Exim, Selemani Ponda wakati wa hafla hiyo iliyowakutanisha wafanyakazi na wateja wa benki hiyo.
Amesema benki hiyo huwa na utaratibu na kukutana na wateja wake katika Kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramdhani na kwamba tayari imeshafanya hivyo katika mikoa mingine ikiwemo Tanga, Mwanza na Mtwara.
“ Tumekutana na wateja wetu katika tafrija fupi ya Iftra mwezi huu wa ramdhan hatufanyi hapa hata mikoa mingine tumeshajumuika na wateja wetu nia ni kuwa nao karibu,” amesema.
Amebainisha kuwa tamko la Serikali la kuzitaka taasisi za kifedha kupunguza riba wamelisikia na mchakato wa kulifanyia unaendelea na kwamba wakati utakapofika riba zitawekwa wazi kwa wateja wao.
Amesisitiza kuwa benki inaamini bado inaendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake huku akiongeza kupunguzwa kwa riba ni njia mojawapo ya kuwanufaisha kwa kuwapatia riba nafuu.
Kwa upande wake, mteja wa benki hiyo, Moustafa Khatan ameziomba benki kutoa riba nafuu na kuajiri wazawa kwa usawa katika nafasi mbalimbali.
Naye Mwanzilishi wa Chama cha Watoa Huduma ya Oil na Gesi nchini(ATOGS) ambaye pia ni mteja wa benki hiyo, Abdulsamad Abdulrahim ameipongeza benki ya Exim kwa kuwakutanisha na kuiomba iendelee kutoa huduma bora.