Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Latest Post

Image result for naibu Meya ilala
Naibu Meya wa Ilala Omary Kumbilamoto
NA MWANDISHI WETU, Dar

NAIBU  Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Vingunguti Omary Kumbilamoto ameeleza sababu zilizopelekea Zahanati ya Vingunguti kufuzu na kupatiwa cheo cha nyota nne na serikali kupitia wakaguzi wake (TRN) na imekuwa miongoni mwa Zahanati tano zilizofuzu.

Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti  wa Kamati ya Zahanati Ibrahim Aeshi Nduze, Naibu Meya Kumbilamoto ameeleza kuwa hali ya mara ya kwanza katika zahanati hiyo haikuwa sawia  lakini kwa jitihada zake na kushirikiana na Halmashauri na Serikali alifanikiwa kufanya mambo mbalimbali katika maboresho ya zahanati hiyo na hatimae imefanikiwa kupewa hadhi ya nyota nne.

Aliyataja mambo yaliyoweza kuyafanya katika Zahanati hiyo kuwa ni Ununuzi wa Gari ya Wagonjwa (Ambulance), mashine ya kufulia,Jenereta, choo kwa kinamama wanaojifungua, utanuzi wa maabara, ufungaji wa feni nne, mashine tatu za kupimia uzito kwa watoto,kipimo cha presha na kiti cha kubebea wagonjwa.

Zahanati nyingine zilizoweza kupandishwa hadhi katika Halmashauri hiyo  ni  Tabata, Mongolandege, Kinyerezi na Kadilugambwa.

Taarifa kutoka kamati ya Zahanati imeeleza kuwa mwanzo ilikua na nyota mbili ambapo zahanati nyingine zilikua na nyota tatu hivyo vingunguti imepanda nyota mbili.

Kamati hiyo imewashukuru wananchi kwa mawazo, maoni, na changamoto walizozitoa ambazo zimefanyiwa kazi na kuiwezesha  kupata nyota mbili za ziada.

Katika hatua nyingine kamati imemshukuru pia Diwani Kumbilamoto kwa kuwaongoza, kuwashauri, na kutoa mchango wa hali na mali ii kufikia malengo.



Image result for waziri mkuu kasimu majaliwa
WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA.

WAZIRI Mkuu 
Kassim Majaliwa, amewaonya mawaziri na kuwataka  wasitumie madaraka yao kama fursa ya kujitajirisha wao binafsi badala yake wametakiwa watumie madaraka hayo kwa manufaa ya taifa.

Majaliwa alitoa angalizo hilo  jana alipozungumza na baadhi ya mawaziri, manaibu na makatibu wakuu katika kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Alisema Rais John Magufuli amesisitiza kwamba amewateua ili wafanye kazi, hivyo wasitumie madaraka waliyopewa kwa maslahi yao binafsi.

“Madaraka haya ya uwaziri si fursa ya kujipatia utajiri, tunatakiwa tufanye kazi kwa weledi, uadilifu, bidii na uaminifu mkubwa ili kuondoa kero za wananchi kwa wakati,” alisema Majaliwa.


Waziri   aliwataka mawaziri na manaibu waziri wazingatie Katiba ya nchi, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali ya serikali katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, mawaziri hao wanatakiwa wasimamie utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa kuanzia mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021.

Pia aliwataka kusimamia utekelezaji wa ahadi zote zilizopo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 pamoja na ahadi alizozitoa Rais Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi.

Waziri Mkuu aliwaagiza mawaziri wahakikishe wanakwenda kufanya ufuatiliaji wa tathmini ya utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo inayohusu sekta zao.

Kadhalika, aliwataka mawaziri hao wakasimamie kikamilifu ukusanyaji wa mapato na kuanzisha vyanzo vipya vya ukusanyaji pamoja na kudhibiti mianya ya upotevu.

Vilevile aliwataka mawaziri hao wakapunguze urasimu katika utekelezaji wa malengo ya Serikali kwa sababu wananchi wanahitaji kuhudumiwa kwa wakati.

Mawaziri waliohudhuria kikao hicho ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), Suileiman Jaffo pamoja na manaibu wake, Joseph Kandege na George Kakunda; Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na Naibu wake, Dk. Faustine Ndungulile.

 Wengine ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe na Naibu wake, Jumaa Aweso; Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage na Naibu wake, Mhandisi Stella Manyanya.

Wamo pia Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na Naibu wake, Japhet Hasunga; Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako na Naibu wake, William ole Nasha; Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega na makatibu wakuu wa wizara hizo.

TAASISI  ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU imeita Waandishi wa habari jiji  Dar es salaam leo na kutoa onyo kwa Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari wa Chadema ambae alipeleka ushahidi wa rushwa kwa taasisi hiyo dhidi ya Mkuu wa Wilaya Arumeru Alexander Mnyeti.

TAKUKURU imesema “Ni kama Mh. Nassari na wenzie wanataka kulifanya hili swala kama la kisiasa badala ya kuwa la kisheria, namuonya Mh. Nassari ameshaleta taarifa yake kwetu, atuachie tufanye kwa mujibu wa sheria na sio kutushinikiza kama kauli aliyoitoa jana….. ‘nitaendelea kutoa series’ “

“Hii Taasisi haishinikizwi na mtu yeyote na hapaswi hata mara moja kutushinikiza…. natoa onyo jingine, endapo ataendelea na utaratibu huu tutachukua hatua za kisheria dhidi yake”


Mji wa Cairo una wakazi 22.8 milioni Mji wa Cairo una wakazi 22.8 milioni
JIJI  la Cairo Nchini Misri ndilo hatari zaidi kwa wanawake kuishi duniani miongoni  mwa majiji duniani, utafiti wa shirika la Thomson Reuters Foundation unaonesha nimeripoti.

Jiji la London nalo ndio mji bora zaidi kwa wanawake kuishi.

Mji wa Kishasha nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo unafuata Cairo, nao mji wa Lagos nchini Nigeria ni wa nane kwenye orodha hiyo.
Jumla ya majiji 19 makubwa yalichunguzwa - ambayo ni majiji yenye idadi ya watu inayofika milioni kumi na zaidi.

Miongoni mwa yaliyozingatiwa kwenye utafiti huo ni unyanyasaji wa kingono, utamaduni unaowadhalilisha wanawake pamoja na upatikanaji wa huduma bora ya afya kwa wanawake, fedha na elimu.

Wataalamu katika haki za wanawake waliombwa ushauri wao wakati wa kufanywa kwa utafiti hao, miongoni mwao akiwa mwanahabari Shahira Amin, ambaye aliambia Thomson Reuters:

"Mambo yote kuhusu wanawake katika jiji hilo ni hatari. Hata kutembea tu barabarani, na hunyanyaswa sana, kwa maneno na kwa vitendo."
CHANZO BBC NEWS

IDADI ya watu waliouawa kwenye mlipuko mkubwa wa bomu katika eneo lenye shughuli nyingi kwenye mji mkuu wa Somalia Mogadishu siku ya Jumamosi, imefikia watu 300 hadi sasa, kwa mujibu wa ripoti ya shirika la hahari la Reuters.

Takriban watu wengine 300 walijeruhiwa kwa mujibu wa AFP, wakati lori lililokuwa limejazwa milipuko lilipolipuka karibu na lango la hoteli.

Reuters walimnukuu Ahmed Ali, muuguzi anayefanya kazi kwenye hospitali moja akisema kuwa miili 160 haikuweza kutambuliwa na hivyo ilizikwa na serikali jana.
Anasema kuwa miili mingine ilizikwa na jamaa zao.
Haki miliki ya picha Reuters
Hilo ndilo shambulizi baya zaidi kutokea nchini Somalia tangu kundi la al-Shabab lianzishe harakati zake mwaka 2007.
Rais Mohamed Abdullahi "Farmajo" Mohamed alilaumu kundi la al-Shabab kwa shambulizi hilo katili.

"Tumethibitisha kuwa watu 300 waliuawa kwenye mipuko huo. Idasi ya waliokufa huenda bado ikaongezeka na kuna watu kadha ambao bado hawajulikani waliko," Abdikadir Abdirahman, mkurugenzi wa idara ya magari ya kusafirisha wagonjwa aliliambia shiria la Reuters.
Haki miliki ya picha AFP


Uongozi wa Mlimani City umelifungia duka kubwa (supermarket) ya Nakumatt iliyopo eno hilo jijini Dar es salaam, baada ya kukosa bidhaa za kutosha kwa muda mrefu na kudaiwa kodi za huduma mbalimbali.

Taarifa ya kufungiwa huko imetolewa leo na Meneja Mkuu wa Mlimani City, Pastory Mroso  na kusema kwamba kabla ya kufungiwa walishapewa notisi miezi minne kufanyia marekebisho tatizo hilo, lakini hakuna hatuo yoyote walioichukua, na kisha kuwapa tena notisi ya mwisho ya siku kumi ambayo ilikuwa inaisha siku ya Jumamosi, na kuamua kuwafungia asubuhi ya leo.



Pastory Mroso ameendelea kwa kusema kwamba tatizo hilo limekuwa likiwaathiri wafanyakazi na hata bidhaa za wafanyabiashara wengine, na pia wamelishalitolea taarifa serikalini kwa hatua zingine zaidi.

Image result for naibu waziri wa ardhi
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dk. Angeline  Lubala

Na Tiganya Vincent,Tabora

 SERIKALI imeuagiza  Uongozi wa Manispaa ya Tabora kuhakikisha wanamaliza tatizo la uvamizi wa Viwanja vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) na vile vinavyomilikiwa na Taasisi nyingine na watu binafsi ili waweze kuviendeleza.

Kauli hiyo imetolewa jana mjini Tabora na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mabula wakati alipotembelea Ofisi za Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora akiwa katika ziara ya siku moja katika Chuo cha Ardhi Tabora.

Alisema kuwa ni vema Halmashauri zote zikahakikisha zinaondoa migogoro ya ardhi kwa kuhakikisha watu wenye maeneo yao ambayo yamevamiwa au kugawia watu wengine ambao sio wamiliki kihalali wanawaondoa na kuwarejeshea watu au Taasisi ambazo ndio zinazomiliki maeneo husika.

Naibu Waziri huyo alisema kuwa Mamlaka zinapochelewa kutatua migogoro ya ardhi zinasababisha tatizo kuzidi kuwa kubwa na kusababisha usumbufu kwa wamiliki halali.

Aidha Naibu Waziri huyo alizishauri Taasisi na watu binafsi wanaomiliki maeneo yao kihalali kuhakikisha wanaweka alama ikiwa ni pamoja na kupanda mimea hata kama maeneo yao bado hajapimwa ili kupunguza migogoro.

Awali akitoa salamu za Chama cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Tabora kwa kiongozi huyo, Katibu wa CCM Mkoa wa Tabora Janeth Kayanda aliomba Serikali kuwasaidia kuwarudishia viwanja vyao sita ambavyo vilivyomilikishwa kwa watu wengine.

Alisema kuwa kitendo hicho kimesababisha Chama kishindwe kupanga mipango mbalimbali ya kuendeleza maeneo husika kwa sababu ya kuwepo na wavamizi hao na hivyo kumuomba kusaidia katika kutafutia ufumbusi wa viwanja vyao ili waweze kutekeleza mipango waliokusudia katika viwanja hivyo.

Katika hatua nyingine Katibu huyo wa Mkoa alimwomba Naibu Waziri kuangalia jinsi ya kuwasaidia baadhi ya wakazi wa Tabora ambao ni miongoni mwa wale 402 ambao nyumba zao zinatarajia kubomolewa kupitisha ujenzi wa reli ya kisasa.

Alisema kuwa baadhi yao walipewa kimakosa  viwanja hivyo na Mamlaka zinazohusika na ugawaji wa viwanja na kufuata taratibu zote na kulipia lakini hivi sasa wanatakiwa waondoke lakini miongoni hawana tena uwezo wa kujenga hata kama wakipewa viwanja.

Naye Mkuu wa Mkoa Tabora Aggrey Mwanri alimwakikishia Naibu Waziri huyo kuwa atahakikisha kuwa wavamizi wote wa viwanja wa chama na vile vya  taasisi nyingine na watu binafsi wanaondolewa na kupewa wamiliki wake kihalali.

Kufuatia hali hiyo alimwagiza Mkurugenzi Mteandaji wa Manispaa ya Tabora kuhakikisha ndani ya wiki mbili watu wote waliovamia viwanja vya Chama wanaondoka nay eye anapata taarifa.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi yuko mkoani Tabora kwa ziara ya kikazi katika Chuo cha Ardhi ya siku moja ambapo baada ya hapo atakwenda Singida na Morogoro.

Aliko Dangote, Tajiri namba moja barani Afrika Aliko Dangote, Tajiri namba moja barani Afrika
TAJIRI namba moja barani Afrika Aliko Dangote ambaye pia ni mwekezaji mkubwa nchini Tanzania amemuonya Rais John Pombe Magufuli kuwa sera zake nchini humo zinawaogopesha wawekezaji.

Dangote ambaye amewekeza dola za kimarekani 650 kwenye uzalishaji wa saruji, amesema wakati umefika kwa raisi Dk. Magufuli kuzipitia upya sera zake ama akubali kuingia katika hatari ya kuwapoteza wawekezaji wote nchini humo.

Raisi Magufuli alipoingia madarakani, wawekezaji na wafanyabisahara walifurahishwa kwa jinsi alivyopambana na rushwa lakini miaka miwili baadae, baadhi ya wafanyabiashara wamegubikwa na hofu hasa baada ya kuona mazingira ya kibiashara yamebadilika kutokana na mfumo wake wa utawala.

Mapema mwaka huu rais Magufuli alianzisha uchunguzi wa kina katika sekta ya madini na kubaini uhalifu mkubwa ambao ulisababishwa kuundwa kwa sheria mpya ya madini.

Katika kongamano lililofanyika mjini London, mfanyabiashara huyo alisema sheria mpya zinazoundwa Tanzania zinaiweka nchi hiyo kwenye hatari ya kuwafukuza wawekezaji wote na kushindwa kuwarejesha tena.

Serikali nchini humo ina amini kwamba sheria hizo zitawanufaisha wananchi kutokana na rasilimali za taifa lao licha ya kwamba makampuni ya kigeni yamekuwa yakipinga mabadiliko hayo ya sheria kwa madai hazitekelezeki.

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget