Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dk. Angeline Lubala |
Na
Tiganya Vincent,Tabora
SERIKALI imeuagiza Uongozi wa Manispaa ya Tabora kuhakikisha
wanamaliza tatizo la uvamizi wa Viwanja vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi
(CCM) na vile vinavyomilikiwa na Taasisi nyingine na watu binafsi ili waweze
kuviendeleza.
Kauli hiyo imetolewa jana mjini Tabora na Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mabula wakati alipotembelea
Ofisi za Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora akiwa katika ziara ya siku moja
katika Chuo cha Ardhi Tabora.
Alisema kuwa ni vema Halmashauri zote
zikahakikisha zinaondoa migogoro ya ardhi kwa kuhakikisha watu wenye maeneo yao
ambayo yamevamiwa au kugawia watu wengine ambao sio wamiliki kihalali
wanawaondoa na kuwarejeshea watu au Taasisi ambazo ndio zinazomiliki maeneo
husika.
Naibu Waziri huyo alisema kuwa Mamlaka
zinapochelewa kutatua migogoro ya ardhi zinasababisha tatizo kuzidi kuwa kubwa
na kusababisha usumbufu kwa wamiliki halali.
Aidha Naibu Waziri huyo alizishauri Taasisi
na watu binafsi wanaomiliki maeneo yao kihalali kuhakikisha wanaweka alama
ikiwa ni pamoja na kupanda mimea hata kama maeneo yao bado hajapimwa ili
kupunguza migogoro.
Awali akitoa salamu za Chama cha Mapinduzi(CCM)
Mkoa wa Tabora kwa kiongozi huyo, Katibu wa CCM Mkoa wa Tabora Janeth Kayanda aliomba
Serikali kuwasaidia kuwarudishia viwanja vyao sita ambavyo vilivyomilikishwa
kwa watu wengine.
Alisema kuwa kitendo hicho kimesababisha
Chama kishindwe kupanga mipango mbalimbali ya kuendeleza maeneo husika kwa
sababu ya kuwepo na wavamizi hao na hivyo kumuomba kusaidia katika kutafutia ufumbusi
wa viwanja vyao ili waweze kutekeleza mipango waliokusudia katika viwanja
hivyo.
Katika hatua nyingine Katibu huyo wa Mkoa
alimwomba Naibu Waziri kuangalia jinsi ya kuwasaidia baadhi ya wakazi wa Tabora
ambao ni miongoni mwa wale 402 ambao nyumba zao zinatarajia kubomolewa
kupitisha ujenzi wa reli ya kisasa.
Alisema kuwa baadhi yao walipewa kimakosa viwanja hivyo na Mamlaka zinazohusika na
ugawaji wa viwanja na kufuata taratibu zote na kulipia lakini hivi sasa
wanatakiwa waondoke lakini miongoni hawana tena uwezo wa kujenga hata kama
wakipewa viwanja.
Naye Mkuu wa Mkoa Tabora Aggrey Mwanri
alimwakikishia Naibu Waziri huyo kuwa atahakikisha kuwa wavamizi wote wa
viwanja wa chama na vile vya taasisi
nyingine na watu binafsi wanaondolewa na kupewa wamiliki wake kihalali.
Kufuatia hali hiyo alimwagiza Mkurugenzi
Mteandaji wa Manispaa ya Tabora kuhakikisha ndani ya wiki mbili watu wote
waliovamia viwanja vya Chama wanaondoka nay eye anapata taarifa.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi yuko mkoani Tabora kwa ziara ya kikazi katika Chuo cha Ardhi ya siku
moja ambapo baada ya hapo atakwenda Singida na Morogoro.
Post a Comment