Naibu Meya wa Ilala Omary Kumbilamoto |
NAIBU Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Vingunguti Omary Kumbilamoto ameeleza sababu
zilizopelekea Zahanati ya Vingunguti kufuzu na kupatiwa cheo cha nyota nne na
serikali kupitia wakaguzi wake (TRN) na imekuwa miongoni mwa Zahanati tano
zilizofuzu.
Akizungumza
mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Zahanati Ibrahim Aeshi Nduze,
Naibu Meya Kumbilamoto ameeleza kuwa hali ya mara ya kwanza katika zahanati
hiyo haikuwa sawia lakini kwa jitihada
zake na kushirikiana na Halmashauri na Serikali alifanikiwa kufanya mambo
mbalimbali katika maboresho ya zahanati hiyo na hatimae imefanikiwa kupewa
hadhi ya nyota nne.
Aliyataja
mambo yaliyoweza kuyafanya katika Zahanati hiyo kuwa ni Ununuzi wa Gari ya Wagonjwa
(Ambulance), mashine ya kufulia,Jenereta, choo kwa kinamama wanaojifungua,
utanuzi wa maabara, ufungaji wa feni nne, mashine tatu za kupimia uzito kwa
watoto,kipimo cha presha na kiti cha kubebea wagonjwa.
Zahanati
nyingine zilizoweza kupandishwa hadhi katika Halmashauri hiyo ni Tabata,
Mongolandege, Kinyerezi na Kadilugambwa.
Taarifa
kutoka kamati ya Zahanati imeeleza kuwa mwanzo ilikua na nyota mbili ambapo zahanati
nyingine zilikua na nyota tatu hivyo vingunguti imepanda nyota mbili.
Kamati hiyo
imewashukuru wananchi kwa mawazo, maoni, na changamoto walizozitoa ambazo zimefanyiwa
kazi na kuiwezesha kupata nyota mbili za
ziada.
Katika hatua
nyingine kamati imemshukuru pia Diwani Kumbilamoto kwa kuwaongoza, kuwashauri,
na kutoa mchango wa hali na mali ii kufikia malengo.
Post a Comment