Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Latest Post

Amani Fongo ‘Man Fongo’.

MSANII wa muziki wa Singeli nchini, Amani Fongo ‘Man Fongo’ mwishoni mwa wiki iliyopita alinusurika kifo baada ya kutereza juu ya paa la nyumba wakati akiweka balbu ya umeme.

Akisimulia mkasa huo kwa Risasi Vibes, Man Fongo alisema tukio hilo lilitokea Sinza jijini Dar alikohamia ambako alikuwa akisimamia mafundi waliokuwa wakiifanyia ukarabati nyumba hiyo, ambapo alipoanguka, mkono wake mmoja uliingia katika chuma kimoja cha geti na kum-pasua kiasi cha kutokezea upande wa pili.

“Nashu-kuru kwa sasa naendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu, kiukweli sijui ilikuwaje mpaka nikatereza kwani nilishtukia nimedondoka na kuumia, maumivu niliyoyapata siwezi hata kuyaelezea kwa kweli,” alisema Man Fongo.


SIKU mbili baada ya gazeti hili kuripoti kuhusu uwapo wa maiti 15 zilizoopolewa baharini mfululizo katika siku za karibuni, zikiwa zimefungwa ndani ya viroba katika pwani za Dar es Salama na Zanzibar,-

Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali (IGP) Simion Sirro, amesema miili hiyo inafanyiwa uchunguzi wa vinasaba (DNA) ili kuwatambua.

IGP Sirro alisema jeshi lake linazo maiti zilizookotwa katika pwani ya Bahari ya Hindi na miili hiyo iko katika hatua ya uchunguzi zaidi.

Akizungumza na ITV jana, IGP Sirro alisema miili hiyo inachukuliwa vinasaba kwa ajili ya utambuzi ili kujua ni raia wa nchi gani.

"Jeshi la Polisi tayari limeshachukua hatua za awali za utambuzi kwa kuchukuliwa vinasaba maiti hizo ili kufahamu ni raia wa wapi na tukishakamilisha kazi hiyo, tutatangaza watu waliopotelewa na ndugu zao kuja kufanya utambuzi," alisema.

Alisema ingawa watu wanadhani kwamba mauaji hayo yamefanywa na Polisi, jeshi lake huwa halina kificho pindi linapokabiliana na wahalifu kwenye mapambano.

Alisema inapotokea polisi ikaua majambazi katika mapigano ya kurushiana risasi, huweka wazi tukio hilo na siyo kwenda kuwatumbukiza baharini.

Mwanaharakati Sheikh Issa Ponda juzi aliitaka serikali kutoa kauli kuhusu jambo hilo ambalo lilifichuliwa na Nipashe kwa mara ya kwanza Jumatatu.

Akizungumza na Nipashe kwa simu juzi, Sheikh Ponda ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu Tanzania, alisema kwa muda mrefu wamekuwa wakipaza sauti kuhusu uwapo wa mauji ya raia kwenye mikoa ya kusini mwa Tanzania lakini haijasikilizwa.
"Tunapongeza Nipashe kwa habari hii," alisema Sheikh Ponda kwa sababu "imefichua mambo mengi."

"Haya tumeshayasema lakini hakuna aliyetusikiliza. Ni wakati mwafaka serikali ikatoa tamko kwa vile vyombo vya dola vimeonyesha kushindwa kueleza miili hiyo ni ya watu gani na inatoka wapi, (na kibaya) zaidi wanasema wanatambua miili mitatu iliyookotwa ambayo kwa sasa iko Muhimbili."

Sheikh Ponda alisema mauaji hayo ni makubwa na hayajawahi kutokea katika serikali zilizopita, kwa miili kusambaa baharini na wavuvi kuipoa.

Alisema jambo hilo si la kawaida, lakini hakuna hatua zozote zinazochukuliwa wala kutolewa taarifa ya kina na serikali kuhusu hali hiyo.

"Jumuiya inaona ni wakati mwafaka kwa serikali kutueleza kwa kuwa vyombo vya dola havijui au havitaki kutoa taarifa juu ya kile kinachoendelea hadi maiti kuokotwa zikiwa ndani ya viroba baharini," alisema.

Kwa mujibu wa vyanzo vya uhakika vilivyozungumza na Nipashe mwishoni mwa wiki iliyopita, miili hiyo iliokotwa kwa nyakati tofauti na wavuvi ambao waliwajulisha polisi, waliofika kuichukua.

Kuwapo kwa idadi kubwa ya miili inayoopolewa kutoka baharini au kukutwa fukweni ikiwa imefungwa kama mzigo kumefanya wavuvi na wafanyabiashara wa samaki kaskazini mwa wilaya ya Kinondoni kuingiwa na hofu pia.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Boaz, juzi alikiri kuopolewa kwa miili kwenye fukwe za Bahari ya Hindi ikiwa imefungwa kwenye mifuko maalum inayofanana na viroba.

"Zipo maiti zimeopolewa na wavuvi katika Pwani ya Dar es Salaam, zikiwa ndani ya mifuko zimeshonewa ndani," DCI Boaz alithibitisha.

Alipoulizwa idadi na maeneo zinakotoka na zinakohifadhiwa, alisema: "Hilo waulize makamanda wa polisi wa mikoa ya kipolisi, siwezi kuwa na takwimu hizo."

Alisema zaidi: "Pia kuhusu zinatoka wapi ni mapema sana kujua kwa kuwa zimebebwa na mawimbi ya bahari hadi kuokotwa maeneo husika.

"Bahari ni pana sana na maiti hizo zinasombwa na mawimbi, hatujui zinatoka wapi, ila waulize ma-RPC (makanda wa polisi) wa mikoa husika."

Wavuvi waliozungumza na Nipashe mwishoni mwa wiki walisema uwapo wa idadi kubwa ya miili hiyo umesababisha baadhi yao kunyamaza wanapoona miili zaidi ikielea baharini.

“Polisi tunawajulisha, wanakuja, wanabeba maiti lakini hakuna siku wametueleza ni za kina nani," alisema mvuvi mmoja wa Kunduchi aliyezungumza na Nipashe kwa sharti la kutotajwa jina gazetini akihofia usalama wake.

"Wavuvi tunafahamiana na ikitokea mwenzetu amekufa au chombo kimezama majini tunafahamu.

"Lakini tangu Agosti mwanzoni tunaokota miili ikiwa imeandaliwa (imefungwa) kabisa na siyo ya wenzetu.”

Wavuvi hao walisema wamepokea taarifa kutoka wenzao wa eneo la Kizimkazi, Zanzibar, kwamba huko nako pia zimeokotwa maiti tano.

Mvuvi mmoja wa Kunduchi alisema mwishoni mwa wiki iliyopita ziliokotwa maiti tano katika eneo la Bongoyo na nne nyuma ya kisiwa cha Mbudya, jijini Darc es Salaam.

Alisema kati ya maiti tisa hizo, moja ilikuwa ya mwanamke na kwamba zilikuwa zimefungwa kamba miguuni, kichwani na tumboni.

MKUU wa Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma, Simon Odunga, ambaye hivi karibuni alimcharaza viboko mzazi wa mtoto aliyemtuhumu kupiga mawe gari lake, Chindika Pingwa, amemwomba radhi mzazi huyo na kumpa zawadi ya mbuzi jike na Sh. 100,000.

Kipigo cha DC huyo, kilimsababishia Chindika maumivu makali na kushonwa nyuzi tisa kichwani.

Tukio hilo lilitokea Agosti 11, mwaka huu, katika barabara ya Kondoa – Dodoma kwenye kijiji cha Paranga wilayani Chemba. Katika tukio hilo, gari la DC huyo lenye namba za usajili STL 669 lilipigwa mawe na watoto na kusababisha kioo cha nyuma kuvunjika.

Akizungumza na Nipashe jana, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mrongia kilichoko Kijiji cha Kambianyasa wilayani Chemba, anachoishi mzazi huyo, Marius Roman, alisema Odunga alifika juzi katika kitongoji hicho na kukutana na mzee Chindika pamoja na uongozi wa kijiji na hatimaye kuomba msamaha kwa kitendo alichokifanya.

Alisema pamoja na kuomba radhi, Odunga alimpa mzee Chindika Sh. 100,000 na mbuzi jike kama sehemu ya kuonyesha kujutia kosa alilolifanya.

Alisema pamoja na kuomba radhi, Odunga aliahidi kuendelea kugharimia matibabu yake hadi pale afya yake itakapoimarika, ili aweze kuendelea na shughuli zake za kila siku.

Roman alisema kitendo alichofanya DC huyo, kimeonyesha uungwana mkubwa kwa sababu ameona kosa lake na kuamua kuomba radhi kwa mwananchi huyo.

Kwa upande wake, Chindika alimshukuru mkuu huyo wa wilaya kwa kuonyesha uungwana na kuomba radhi kwa kitendo alichokifanya. Pia alikiri kupewa mbuzi, lakini alikataa kuzungumzia kiasi cha pesa alizopatiwa.

Alipozungumza na Nipashe, Odunga alikiri kukutana na mzazi huyo pamoja na uongozi wa kijiji kuzungumzia suala hilo, ikiwamo kuomba msamaha kwa yale yaliyotokea na kumpatia Chindika mbuzi na fedha taslimu Sh. 100,000.

Odunga alisema ameamua kufanya hivyo baada ya kuona alifanya kitendo kile akiwa na jazba na ameona ni vyema kuomba radhi, ili aendelee kushirikiana na wananchi wake.

Alisema pia atahakikisha anaweka mikakati ya kusimamia usalama barabarani kwenye eneo hilo, ili kuwakinga watoto wanaojitokeza barabarani kurusha mawe kwenye magari yanayopita.

“Tumeweka mikakati na viongozi wa kijiji hicho, ili kuhakikisha usalama wa barabarani unakuwapo,” alisema Odunga.

Mourners react on July 24, 2017, in the Dalori IDP (Internally Displaced People) camp outside Maiduguri, after a suicide bomb attack that killed fourHaki miliki ya pichaAFP
Image captionThe Boko Haram insurgency has devastated many lives across north-eastern Nigeria
KUMEKUWA na ongezeko kubwa la  idadi ya watoto wanaotuhumiwa kama washambuliaji wa kujitolea mhanga na wanamgambo wa Boko Haram, kaskazini mashariki mwa Nigeria, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto Unicef, linasema kuwa tayari visa 83 vimeripotiwa mwaka huu, mara nne zaidi ya vile vya mwaka wote wa 2016.
55 kati yao walikuwa ni wasichana walio na umri chini ya miaka 15 na kwenye kisa kimoja, bomu lilifungwa kwa mtot ambaye alikuwa amebewa na msichana mdogo.
Unicef inasema mbinu hii imezua hofu kwa watoto wanaoachiliwa na Boko Haram kulingana na Umoja wa Mataifa, watoto 127 wametumiwa kama walipuaji kaskazini mashariki mwa Nigeria tangu mwaka 2014.
Wanamgambo wa Boko Haram mara kwa mara wamewatumia watoto, na wamewateka mamia ya wasichana wa shule na kuwalazimisha watoto wavulana kujiunga na jeshi lao.
CHANZO BBC NEWS

Trump amekuwa akipingwa kwa kutoa baadhi ya kauli zenye utata
Image captionTrump amekuwa akipingwa kwa kutoa baadhi ya kauli zenye utata
MAMIA ya wafuasi wa Rais wa Marekani Donald Trump wamekusanyika katika mji wa Phoenix, Arizona kwa mkutano utakaohutubiwa nae hivi punde.
Hata hivyo inasemekana kuwa wapinzani wa Trump pia wamekusanyika kwa ajili ya kumpinga.
Meya wa mji huo awali alimtaka Trump achelewe kufika kwa madai ya kusababisha ubaguzi wa rangi nchini Marekani.
Kulikua na waliompinga pia katika mkutano huo
Image captionKulikua na waliompinga pia katika mkutano huo
Ni kutokana na maneno ya Trump juu ya mgogoro ulioibuka kati ya weupe na weusi mapema mwezi huu mjini Charlottesville.
CHANZO BBC NEWS

Kim Jong-unHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKorea inasisitiza kuwa ina haki ya kuwa na mpango wa nyuklia kwa usalama wake
NCHI ya Marekani  imetangaza vikwazo kwa kampuni kadha za Urusi na Uchina na watu ambao inawalaumu kwa kusaidia mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.
Hatua hii imetokea baada ya baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa, ikiwemo Urusi na China kupiga kura ya kuiwekea viwazo zaidi Korea Kaskazini.
Wizara ya fedha nchini Marekani ilisema kuwa vikwazo hivyo vitaongeza shinikizo kwa Korea Kaskazini lakini hatua hiyo imeighadhabisha China.
soldiers trainingHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKorea Kaskazini inapinga mazoezi ya pamoja kati ya Korea Kusini na Marekani
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Rex Tilleron, wakati huo huo ameipongeza Korea Kaskazini kwa kujizuia siku za hivi karibuni.
"Hatujashuhudia urushaji wa makombora na vitendo vya uchokozi kutoka Korea Kaskazini tangu azimio la baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa lianze kutekelezwa," alisema.
Wizara ya fedha itaendelea kuongeza shinikizo kwa Korea Kaskazini kwa kuenga wale wanaosaidia kuendelea kwa mipango ya nyuklia na ya makombora ya masafa marefu.
soldiers trainingHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKorea Kusini inasema kuwa mazoezi hayo ni ya kujikinga
Hatua hiyo inamaanisha kuwa watu nchini Marekani na kampuni za Marekani haziruhusiwi kufanya biashara na kampuni zinazosaidia programu za Korea Kaskazini.
China ilijibu mara moja kwa kutoa wito kwa Marekani ikitaka irekebishe makosa yake ya kuadhibu makampuni ya China.
CHANZO BBC NEWS


Na Tiganya Vincent, RS-TABORA

Maafisa Ugani wa Kata, Vijiji na Wilaya zote zinazolima tumbaku mkoani Tabora wametakiwa kuwa na mashamba darasa ambayo wakulima watayatumia kama sehemu ya kwenda kujifunza juu ya uzalishaji wa tumbaku kwa tija na  ubora unaotakiwa ili waweze kuongeza kipato chao.

Kauli hiyo ilitolewa jana katika Chuo cha Mafunzo ya Kilimo Tumbi na Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri wakati akifungua mafunzo ya siku sita ya  Maafisa Ugani 114  yakiwa na lengo la  kuwajengea uwezo wa kusimamia vizuri zao la tumbaku na wakulima wake.

Alisema kuwa baada ya mafunzo hayo ni jukumu la Wataalamu kwenda kuwasaidia wakulima  wa tumbaku ili wabadilike katika kilimo chao kwa ajili ya kuondokana na unyonge wa uzalishaji ambao haumpi mazao na bei nzuri katika masoko ya tumbaku.

Bw. Mwanri alisema kuwa zoezi hilo ni pamoja na Maafisa hao kuwa karibu na wakulima kuanzia wakati wa matayarisho ya vitalu hadi wanapokuwa wanapokwenda tumbaku yao katika masoko ili kama kuna matatizo yanayowakwamisha waweze kuwasaidia.

Alisema kuwa sanjari kuwa karibu na wakulima Maafisa hao ni lazima kuanzia msimu ujao wa kilimo wapite kwa kila mkulima ili kuhakiki mazao yaliyopo katika mashamba ya wakulima wa tumbaku  (crop survey) ili kujua hali halisi ya matarajio ya uzalishaji wa kila mmoja wao kwa ajili kuepuka udanganyifu.

Bw. Mwanri alisema kuwa hatua hiyo itasaidia kuwabaini watu ambao hawakulima tumbaku lakini inapofika msimu wa mauzo wanaingiza tumbaku katika masoko na kuendelea kuwanyonya wakulima na kuwafanya waendelee kuwa tegemezi.

Naye Mkuu wa Chuo cha Kilimo Tumbi Kasele Steven alisema kuwa Mafunzo hayo ya siku kwa Maafisa Ugani hao ni muhimu sana katika kuhakikisha kuwa wanapata elimu itakayowawezesha kuwa na uelewa wa kutosha juu ya zao hilo kwa sababu baadhi yao wakati wanasoma vyuo hawakupata mafunzo kuhusu zao la tumbaku.

Alisema kuwa baada ya mafunzo hayo Maafisa Ugani wa Serikali watakuwa karibu sana na wakulima kuliko ilivyokuwa hapo awali ambapo ni Maafisa Ugani wa Kampuni za Tumbaku pekee ndio walikuwa wakimhudumia mkulima wa tumbaku na kukosa msaada wa Wataalamu wa Serikali.

Steven aliongeza kuwa Maafisa Ugani wataweza kujifunza juu ya aina na sifa za mbegu bora za tumbaku, uandaaji na utunzaji wa vitalu , maandalizi ya shamba, utunzaji wa shamba, uvunaji wa tumbaku, ukaushaji wa tumbaku ,uchambuzi na upangaji madaraja ya tumbaku na Sheria na Kanuni za kilimo cha tumbaku.

Mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa magizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa aliyoyatoa alipofanya ziara mkoani hapo kwa vipindi tofauti tofauti ya kutaka Maafisa hao wapatiwe mafunzo na waende kuwasaidia wakulima wa tumbaku badala ya kuwaachia wa Kampuni zinazonunua Tumbaku pekee ndio wahudumie mkulima wa tumbaku.

Katika kutekeleza agizo hilo Mkoa wa Tabora umeanza na Maafisa Ugani 114 ambao wanatoka Wilaya za Sikonge, Nzega, Uyui, Manispaa ya Tabora, Urambo , Kaliua na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora.

DSC_2410
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar  Dk.Ali Mohamed Shein  alipokuwa akifungua pazia kuweka jiwe la msingi Tawi  la CCM Kijiji cha Njuguni Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba jana   akiwa katika ziara zake Mkoa wa Kaskazini Pemba,kutembela Miradi mbali mbali ya Maendeleo
DSC_2420
Baadhi ya Wanachama wa Chama cha  Mapinduzi Kijiji cha Njuguni walipokuwa wakimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar  Dk.Ali Mohamed Shein  mara alipowasili katika Kijiji hicho  kuweka jiwe la msingi Tawi la CCM  Njuguni  Wilaya ya Micheweni jana  akiwa katika ziara zake Mkoa wa Kaskazini Pemba,kutembela Miradi mbali mbali ya Maendeleo
DSC_2435
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar  Dk.Ali Mohamed Shein  alipokuwa akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kuweka jiwe  la msingi Tawi la CCM  Njuguni Wilaya ya Micheweni jana akiwa katika ziara zake Mkoa wa Kaskazini Pemba,kutembela Miradi mbali mbali ya Maendeleo
DSC_2442
Risala ya Chama cha Mapinduzi Tawi la CCM Njuguni ikisomwa na Bi.Mkitu Hassan Mwalimu wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar  Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipofika kuweka jiwe la msingi Tawi la CCM Kijijini hapo jana akiwa katika ziara zake Mkoa wa Kaskazini Pembe kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo
DSC_2540
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar  Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto pichani) alipokuwa akizungumza na WanaCCM Tawi la CCM Njuguni mara baada ya kuliweka jiwe la msingi Tawi  hilo jana akiwa katika ziara zake Mkoa wa Kaskazini Pembe kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo,pia alifanyisha Harambee ya kukamilisha Ujenzi wa Tawi hilo,[Picha na Ikulu.]22/08/2017.

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget