Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Latest Post

0V5A0017Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhaniakiwa na kitabu cha wageni kwenye Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Malindi Estate ambayo ipo kwenye nyumba ya mmoja wa wagombea wa Uchaguzi Mdogo wa Madiwani Kata ya Mbweni.Picha na NEC.
Hussein Makame-NEC
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imejiridhisha kuwa uamuzi wa kuvihamisha vituo 21 vya kupigia kura katika Kata ya Mbweni, jimbo la Kawe katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, umezingatia Sheria na Kanuni za Uchaguzi.
NEC imetoa msimamo huo, baada ya kupokea taarifa kutoka kwa baadhi ya wananchi na vyama vya siasa wakilalamika kuwa Tume ya uchaguzi imehamisha vituo vinane (8) vya kupigia kura na kuvipeleka kwenye Kituo cha Polisi, hatua waliyoeleza kuwa ni kuwanyima haki wapiga kura katika kutimiza haki ya msingi.
Malalamiko mengine yaliyoifikia NEC ni kwamba Tume ilivihamisha vituo vingine 15 kutoka maeneo ya awali na kuvipeleka maeneo mengine jambo ambalo baadhi ya vyama havikukubaliana na uamuzi huo.
Kutokana na malalamiko hayo, jana Jumanne Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Kailima Ramadhani akiambatana na watendaji wengine wa Tume, walitembelea maeneo hayo na kujiridhisha kuwa mabadiliiko ya vituo yaliyofanywa na msimamizi wa uchaguzi yamekidhi matakwa ya kisheria.
“Nimefika hapa jimbo la Kawe kata ya Mbweni, baada ya mwananchi mmoja kunitumia ujumbe akiniambia kuwa kuna chama kimoja kinachoshiriki Uchaguzi Mdogo wa Madiwani wa Kata ya Mbweni kinalalamika kwamba Tume imehamisha vituo vya kupigia kura kiholela,” alisema Ramadhani.
Mkurugenzi wa Uchaguzi aliongeza kuwa, chama hicho kimelalamika kuwa vituo hivyo vimepelekwa kwenye eneo la kituo cha Polisi, kwa hiyo huenda wapigakura wakanyimwa haki yao ya kupiga kura.
Alisema alipowauliza watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, majibu yao hayakumridhisha ndipo alipoamua kufika eneo la tukio.
“Kwanza wanalalamika kwamba vituo vilivyohamishwa ni 27, lakini ukweli ni vituo 21, vituo hivyo vimehamishwa kwa mujibu wa Sheria kwa sababu  Novemba mosi 2017, Msimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata aliviita vyama vinne na kufanya mkutano na aliwaambia tunavihamisha vituo hivyo kwa sababu mbalimbali.
“Sababu alizozitoa msimamizi wa uchaguzi ni kwamba vituo vinane  vilikuwa shule ya Sekondari New Era na vituo saba7 vilikuwa jirani na nyumbani kwa mgombea ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa na vituo sita vilikuwa kwenye eneo la Kanisa,” alifafanua Kailima.
Alibainisha kuwa kifungu cha 20 (2) cha Kanuni za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura za Mwaka 2015 na Kifungu cha 21 cha Kanuni za Uchaguzi Mkuu wa 2015, vinabainisha kuwa vituo vya kupigia kura havipaswi kuwa kwenye maeneo ya watu binafsi, kwenye maeneo ya ibada na kwenye kambi za jeshi.
Kutokana na msingi wa kanuni hizo, Kailima alithibitisha kuwa uamuzi wa kuvihamisha vituo hivyo kwenye maeneo hayo ambao umefanywa na  msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Kawe ulikuwa sahihi.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ambaye ndiye  Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kawe ilipo kata ya Mbweni, Aron Kagurumjuri alisema malalamiko kuhusu kuhamishwa kwa vituo hivyo yalitolewa na chama kimoja kati ya vyama vinne ambavyo vitashiriki kwenye uchaguzi mdogo wa diwani wa kata hiyo.
Alisema Uchaguzi mdogo wa kata hiyo unafanyika baada ya mahakama kutengua uchaguzi wa awali kutokana na ukiukwaji wa baadhi ya taratibu za Uchaguzi.
“Tuko hapa kwa sababu chama kimoja kati ya vyama vinne vinavyoshiriki Uchaguzi huu mdogo, kulalamika kwamba tumehamisha vituo na kuvipelekea kwenye maeneo ambayo sio rafiki kwa wapiga kura,” alisema Kagurumjuri.  
Alifafanua kuwa hali halisi inaonesha kwamba kanuni  na taratibu za kupigia kura, haziruhusu kuweka kituo kwenye jengo la mtu binafsi,  na shule hiyo ambayo ilikuwa na vituo kadhaa ni shule ya mtu binafsi.
“Kwa hiyo kwa Uchaguzi huo wa mwakaa 2015 kanuni hizo zilikiukwa sasa kwa uchaguzi huu kwa sababu tunataka tufanye Uchaguzi kwa kufuata kanuni na sheria hatukutaka kuingia kwenye uvunjaji wa kanuni na taratibu,”
 “Baada ya kuhamisha vituo na kuvipeleka eneo hilo, ikazua sintofahamu kwa chama kimoja na vyama vitatu vilivyoridhia ambapo tulikuwa na mashaka inawezekana kilifaidika na vituo kuwepo maeneo hayo,” alisema.
Kagurumjuri alisema vituo vingine vimehamishiwa kwenye eneo la wazi na lenye usalama zaidi kwa wapiga kura pamoja na vitu vingine, na kwamba wanaona halina shida.

DSC_0456
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seuf Ali Idi akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mustafa Abdujumbe mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Halmashairi ya Wilaya ya Kaskazini A Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa ajili ya Kushuhudia utiwaji wa saini ujenzi wa Barabara za Bububu Mahonda Mkokotoni,Pale Kiongele,Matemwe Muyuni na Fuoni Kombeni.
DSC_0487
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mustafa Abdujumbe kulia akitoa taarifa kuhusiana na Uwekaji saini ujenzi wa Barabara za Bububu Mahonda Mkokotoni,Pale Kiongele,Matemwe Muyuni na Fuoni Kombeni hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Halmashairi ya Wilaya ya  Kaskazini A Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja.
DSC_0509
Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Balozi Ali Karume akitoa hotuba kuhusiana na Ujenzi wa Barabara katika hafla ya Uwekaji saini ujenzi wa Barabara za Bububu Mahonda Mkokotoni,Pale Kiongele,Matemwe Muyuni na Fuoni Kombeni, iliofanyika katika Ukumbi wa Halmashairi ya Wilaya ya  Kaskazini A Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja.
DSC_0522
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mustafa Abdujumbe kushoto akitiliana saini na Mkurugenzi Muendeshaji wa Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation(CCECC)Jiang Yigao kuhusiana na ujenzi wa Barabara za Bububu Mahonda Mkokotoni,Pale Kiongele,Matemwe Muyuni na Fuoni Kombeni,hafla  iliofanyika katika Ukumbi wa Halmashairi ya Wilaya ya  Kaskazini A Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja.
DSC_0530
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mustafa Abdujumbe kushoto akikabidhiana vitabu vya mikataba na Mkurugenzi Muendeshaji wa Kampuni ya China  Civil Engineering Construction Corporation(CCECC)Jiang Yigao Baada ya kutiliana saini  kuhusiana na ujenzi wa Barabara za Bububu Mahonda Mkokotoni,Pale Kiongele,Matemwe Muyuni na Fuoni Kombeni,hafla  iliofanyika katika Ukumbi wa Halmashairi ya Wilaya ya  Kaskazini A Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja.
DSC_0571
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seuf Ali Idi akitoa hotuba katika hafla ya utiaji saini ujenzi wa Barabara za Bububu Mahonda Mkokotoni,Pale Kiongele,Matemwe Muyuni na Fuoni Kombeni,hafla  iliofanyika katika Ukumbi wa Halmashairi ya Wilaya ya  Kaskazini A Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja.
DSC_0580
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria katika hafla ya uwekaji saini ujenzi wa Barabara za Bububu Mahonda Mkokotoni,Pale Kiongele,Matemwe Muyuni na Fuoni Kombeni,  iliofanyika katika Ukumbi wa Halmashairi ya Wilaya ya  Kaskazini A Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja.
DSC_0592
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seuf Ali Idi akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali waliohudhuria katika  hafla ya uwekaji saini ujenzi wa Barabara za Bububu Mahonda Mkokotoni,Pale Kiongele,Matemwe Muyuni na Fuoni Kombeni,  iliofanyika katika Ukumbi wa Halmashairi ya Wilaya ya  Kaskazini A Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

Twitter logoHaki miliki ya pichaREUTERS
MTANDAO wa kijamii wa Twitter imetangaza kwamba imeanza kuwafungulia watu wanaoutumia mtandao huo   uwezo wa kuandika ujumbe kwa kutumia tarakimu 280 badala ya 140.
Kampuni hiyo ilikuwa imewawezesha baadhi ya watu kutumia tarakimu hizo lakini kwa majaribio tangu Septemba lakini sasa wamesema watu wengi wataruhusiwa kuandika ujumbe mrefu.
Watakaozuiwa pekee ni wale wanaoandika ujumbe kwa Kijapani, Kichina na Kikorea ambao wanaweza kuwasilisha maelezo zaidi kwa kutumia tarakimu chache.
Ufupi wa ujumbe
Wakati wa majaribio, ni ujumbe 5% ambao ulikuwa na urefu wa zaidi ya tarakimu 140 na ni 2% uliokuwa na zaidi ya tarakimu 190, wamesema.
Lakini walioandika ujumbe mrefu walipata wafuasi zaidi, walihusiana na watu zaidi na walitumia muda zaidi katika mtandao huo.
"Tuliona kwamba watu walipohitaji zaidi ya tarakimu 140, waliandika ujumbe kwa urahisi na mara nyingi. Muhimu zaidi, watu waliandika ujumbe wa chini ya tarakimu 140 mara nyingi zaidi na ufupi wa ujumbe wa Twitter ulisalia," meneja wa bidhaa na huduma wa Twitter Aliza Rosen ameandika
Mabadiliko hayo yalipotangazwa mara ya kwanza, wengi waliyakosoa na kusema badala yake wangelipenda kuona taarifa za chuki pamoja na mashine zinazoandika ujumbe zikidhibitiwa zaidi.
Aidha, wengi walitaka ujumbe urudi kufuata historia tena, ujumbe wa karibuni zaidi ukionekana mwanzo na pia waweze kuhariri ujumbe.
Mtandao huo kwa sasa una watu 330 milioni, idadi ambayo ni ya chini ukilinganisha na 800 milioni wa Instagram na zaidi ya 2 bilioni wa Facebook.

OdingaHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
KIONGOZI  wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amependekeza serikali ya muda iundwe nchi humo na kutawala kwa muda wa miezi sita kama sehemu ya kutatua mzozo wa kisiasa nchini humo.
 Odinga, ambaye alisusia uchaguzi wa marudio uliofanyika mwezi uliopita, amesema katika kipindi hicho kunafaa kufanyika marekebisho ya katiba kuchunguza upya mamlaka ya rais.
Kiongozi huyo ambaye ameanza ziara nchini Marekani alisema yuko tayari kufanya mazungumzo na Rais Uhuru Kenyatta kuhusu marekebisho ya kikatiba ambayo anasema yanahitajika kupunguza hatari ya kuzuka kwa fujo kutoka kwa makundi ya jamii za wachache ambao wanajiona kwamba wametengwa.
 Kenyatta alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo wa marudio uliofanyika tarehe 26 Oktoba akiwa na kura 7.5 milioni ambazo ni sawa na asilimia 98 ya kura zilizopigwa.
Waliojitokeza kushiriki uchaguzi huo ni asilimia 39 ya waliojiandikisha kuwa wapiga kura nchini humo.
Uchaguzi huo ulitokana na hatua ya Mahakama ya Juu, kufuatia kesi iliyowasilishwa na Bw Odinga, kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa tarehe 8 Agosti ambapo Bw Kenyatta alikuwa ametangazwa mshindi akiwa na asilimia 54 ya kura.
Mahakama ya Juu ilisema uchaguzi huo wa mwanzo ulikumbwa na kasoro nyingi ambapo  Odinga alisusia uchaguzi wa marudio akisisitiza lazima mageuzi yafanywe katika Tume ya Uchaguzi (IEBC).
Alisema hakuna na imani kwamba uchaguzi huo wa marudio ungekuwa huru na wa haki.
Wafuasi wa  Odinga wamekuwa wakiandamana mara kwa mara tangu kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa kwanza.
Watu zaidi ya 50 wameuawa katika makabiliano kati ya polisi na wafuasi wa upinzani.
"Mfumo halisi wa utawala wa urais unaendeleza ukabila kwa sababu kila kabila linahisi kwamba haliko salama ikiwa mtu kutoka kabila hilo si kiongozi," aliambia Reuters kwenye mahojiano.
Wafuasi wa upinzaniHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
Image captionWafuasi wa upinzani wamekuwa wakiandamana mara kwa mara kushinikiza mageuzi katika tume ya uchaguzi
Katiba mpya iliyoanza kutekelezwa mwaka 2010 iligatua baadhi ya mamlaka ya serikali kuu kwa kuunda serikali za majimbo 47 zinazoongozwa na magavana.
Serikali hizo huwa na uwezo wa kujiendeshea shughuli nyingi lakini bw Odinga anasema mamlaka mengi bado yamebaki kwenye serikali kuu na hilo linafaa kubadilika.
"Tulipata katiba mpya mwaka 2010; Tunafikiri kwamba wakati umefika tuiangalie upya," amesema.
Alieleza kuwa marekebisho ya Katiba hiyo yanafaa kuimarisha taasisi huru za serikali mfano tume ya uchaguzi na kupunguza mamlaka ya rais.
"Tunafikiri kwamba pengine miezi sita itatosha kufanikisha marekebisho haya ambayo tunayahitaji katika taifa hili," alisema.
Bw Kenyatta, baada ya kutangazwa mshindi, alisema hatafanya mazungumzo na upinzani hadi umalize njia zote za kisheria za kupinga matokeo ya uchaguzi.
Matokeo kamili ya wagombea wote kama yalivyotangazwa na IEBC
MgombeaChamaKuraAsilimia
Uhuru KenyattaJubilee7,483,89598.28
Raila Odinga (Alisusia)ODM73,2280.96
Mohamed Abduba DidaARK14,1070.19
Japheth Kavinga KaluyuMgombea wa kujitegemea8,2610.11
Michael Wainaina MwauraMgombea wa kujitegemea6,0070.08
Joseph Nthiga NyagahMgombea wa kujitegemea5,5540.07
John Ekuru AukotThirdway Alliance21,3330.28
Cyrus JirongoUDP3,8320.05
 Odinga, siku moja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi alitangaza kwamba atageuza muungano wake wa National Super Alliance (Nasa) kuwa vuguvugu la kupinga serikali.
Majuzi, muungano wake uliwahimiza wafuasi wake kususia bidhaa na huduma za kampuni tatu kuu ambazo alisema zimekuwa zikiisaidia serikali ya Rais Kenyatta.
Kesi mbili ziliwasilishwa kupinga ushindi wa Bw Kenyatta Jumatatu katika Mahakama ya Juu.
Mahakama hiyo ina siku 14 kusikiliza na kutoa uamuzi kuhusu kesi hizo.
Upinzani ulipinga matokeo ya uchaguzi wa marudio na badala yake kusema uchaguzi mpya unafaa kufanyika katika kipindi cha siku 90.
Nasa hata hivyo hawajawasilisha kesi ya kupinga matokeo hayo mahakamani.
CHANZO BBC NEWS

US President Donald Trump speaks at the National Assembly on 8 November 2017 in Seoul, South KoreaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMr Trump also addressed Mr Kim directly in his speech
RAIS  wa Marekani Donald Trump ametoa onyo kali kwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong un katika hotuba ndani ya bunge la Korea Kusini.
''Usitudharau, usitujaribu," alisema, huku akishutumu hali ilivyo nchini Korea Kaskazini.
Rais  Trump alimzungumzia moja kwa moja rais Kim akisema kuwa ''silaha unazojilimbikia hazikufanyi wewe kuwa salama lakini zinakuweka katika hali hatari''.
Kiongozi huyo wa Marekani yuko katika ziara ya siku mbili nchini Korea Kusini katika ziara ya bara Asia.
Kwengineko katika hotuba yake amesema kuwa huku Korea Kaskazini ikiona uvumilivu kuwa udhaifu sasa kuna utawala mpya nchini Marekani.
Trump pia ameutaka ulimwengu hususan China na Urusi kuiwekea shinikizo kali Pyongyang kusitisha utengenezaji wake wa silaha za kinyuklia.
Dunia haiwezi kuvumilia hatari inayosababishwa na taifa linaloongozwa na utawala usioaminika ambao unaitishia na silaha za kinyuklia.
Mataifa yote yaliowajibika yanafaa kuungana kuangamiza utawala wa kikatili wa Korea Kaskazini kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayeuunga mkono, kupata usaidizi wowote ama hata kukubalika, alisema.
CHANZO BBC NEWS

Hamisa Mobeto

MWANAMITINDO kutoka Tanzania,  Hamisa Mobetto amefanikiwa kunyakuwa tuzo ya Starqt Awards katika msimu wake wa nne kupitia kipengele  cha ‘People Choice Awards’.

Mrembo huyo aliyekuwa ana wakilisha Tanzania na Afrika Mashariki alikuwa akiwania vingengere viwili ambavyo ni ‘People Choice Awards’ na ‘Super Mum’ ila amefanikiwa kuibuka kidedea katika kipengele kimoja tu.

Starqt Awards ni tuzo zinazohusisha biashara, mitindo, burudani na vitu vingine. Na zoezi la ugawaji tuzo hizo lilifanyika Novemba 4 mwaka huu katika ukumbi wa Bedford View City Hall, mjini Johannesburg nchini South Afrika.

WAZIRI  Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Mawaziri kuacha kutoa matamko yasiyotekelezeka ili kuepusha mkanganyiko serikalini.

Waziri ametoa tamko hilo jana jioni kwenye kikao cha baraza la mawaziri kilichofanyika Dodoma, ambapo amewaasa mawaziri kujidhirisha na bajeti pamoja na sera za serikali kabla ya kutoa tamko ili kuepusha athari zinazoweza kujitokeza endapo tamko halitatekelezeka.

Mbali na hilo waziri mkuu amewataka viongozi hao wafanye kazi kwa kuzingatia maadili ya uongozi ili kuithibitishia jamii kuwa Rais Dkt. John Magufuli aliwateua kutokana na uadilifu na uwezo wao kiutendaji.

“Tunao wajibu mkubwa kuhakikisha kwamba kila mmoja wetu anafanya kazi kwa nguvu na bidii ili kutimiza matarajio ya Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli na wananchi wote kwa ujumla,” amesema waziri mkuu.

Aidha waziri mkuu amewataka mawaziri wafanye ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo inayohusu sekta zao kwa kuwa wao ni wasimamizi wa utekelezaji wa majukumu ya Serikali.

MTU mmoja ambaye jina lake halijatambulika na maeneo ambayo anaishi amekutwa amekufa na mwili wake kutelekezwa katika Barabara ya Mwanza eneo la Kiwanda cha Nyuzi Tabora kilichopo Kata ya Tambukareli Manispaa ya Tabora.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kutokea kwa tukio mauaji jana mjini Taboea na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari hasa watembea majira ya usiku.

Alisema kuwa Polisi wanaendelea na uchunguzi ili kuweza kubaini chanzo cha mauaji hayo ili wahusika weweze kuchukuliwa hatua na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Kitete.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kijiweni  katika Manispaa ya Tabora Mohamed Mayunga amelaani kitendo hicho na kusema ni cha kinyama na kuomba Polisi kuhakikisha wanafuatilia kitendo hicho ili kukomesha mauaji zaidi.

Alisema kuwa pamoja marehemu haijafahamika alikuwa anafanyakazi gani ni vema wakazi wa Tabora hasa madereva wa boda boda wakachukua tahadhari wanapokodishwa nyakati za usiku kwa wapo watu wasio na nia njema kwao.

Mtu huyo anasadikiwa kuwawa kwa kupigwa kwa kitu chenye ncha kali katika sehemu za  kichwa.

 


 

Rais Dk. Magufuli

AGIZO  la Rais Dk. John Magufuli kuhusu wananchi wanaofanya shughuli za kibinadamu ndani ya mita 60 kutoka vyanzo vya maji wasibughudhiwe limeibua maswali bungeni ikielezwa kuwa kauli hiyo ya Rais amevunja sheria.

Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini (Chadema), Peter Msigwa katika swali la nyongeza bungeni amesema, “Kwanza niipongeze wizara mara nyingi imejitahidi kuelimisha jamii itunze mazingira, lakini sisi kama wawakilishi wa wananchi tumsikilize Rais au waziri? mara nyingi tumeambiwa akisema Rais ni sheria jana amewaambia wananchi  waingie kwenye mabonde walime mpaka mvua itakapowatoa,  lakini waziri unazuia.”

Akijibu swali hilo , Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Kangi Lugola amesema Rais Magufuli hajavunja sheria kuagiza mamlaka zinazohusika na mazingira kuacha kuwabughudhi wananchi wanaolima pembezoni mwa mito.

Pia, ameonya viongozi wanaochochea wananchi kuvunja sheria na wananchi waliozoea kuzivunja akisema Serikali itapambana nao.

Lugola pamoja na waziri wa wizara hiyo, January Makamba leo Jumatano Novemba 8,2017 wamesema sheria inatoa mamlaka kwa waziri kutoa kibali kwa shughuli kufanyika katika maeneo hayo.

Waziri January amesema kutokana na maelekezo ya Rais Magufuli ya jana Jumanne Novemba 7,2017 kwa eneo mahsusi kwa mujibu wa sheria wataweka mwongozo wa matumizi.

Rais Magufuli alisema busara itumike wakati wa utekelezaji wa  sheria ya mazingira inayozuia shughuli za kibinadamu ndani ya mita 60 kutoka kwenye chanzo cha maji ili kuwaondolea  kero wakulima wanaojitafutia chakula na kipato cha kawaida kwa ajili ya familia zao.

“Ni vyema utekelezaji wa sheria ya mazingira ya mita 60 ilenge zaidi kubana wanaotumia maeneo ya maziwa na bahari na si wananchi wanaolima mazao ya  chakula ya muda mfupi kando mwa mito,” aliagiza.

Rais Magufuli alitoa kauli hiyo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa mwananchi aliyejitambulisha kwa jina moja la Roshi, mkazi wa Kyaka wilayani Missenyi aliyedai kuwa mazao ya  chakula yaliyokuwa kwenye shamba lake lililopo kando mwa  mto yalifyekwa na watu wa mazingira kwa madai kuwa yalilimwa ndani ya mita 60.

Rais Magufuli alisisitiza agizo hilo wilayani Karagwe na hata mjini  Bukoba akiagiza wananchi hao kuendelea na shughuli za kujiongezea kipato na wasiondolewe katika maeneo hayo.

Kuhusu wananchi wanaodaiwa kuvamia vyanzo vya maji, Rais aliagiza watu zaidi ya 200 wanaodaiwa kuvamia vyanzo vya maji watafutiwe maeneo mengine kwa sababu ni kosa la viongozi na mamlaka husika zilizozembea kuwazuia mapema kuingilia maeneo hayo.

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget