Majaliwa awataka Mawaziri kuacha kutoa matamko yasiyotekelezeka
WAZIRI Mkuu
Kassim Majaliwa amewataka Mawaziri kuacha kutoa matamko yasiyotekelezeka ili
kuepusha mkanganyiko serikalini.
Waziri ametoa tamko hilo jana jioni kwenye kikao cha baraza
la mawaziri kilichofanyika Dodoma, ambapo amewaasa mawaziri kujidhirisha na
bajeti pamoja na sera za serikali kabla ya kutoa tamko ili kuepusha athari
zinazoweza kujitokeza endapo tamko halitatekelezeka.
Mbali na hilo waziri mkuu amewataka viongozi hao wafanye kazi
kwa kuzingatia maadili ya uongozi ili kuithibitishia jamii kuwa Rais Dkt. John
Magufuli aliwateua kutokana na uadilifu na uwezo wao kiutendaji.
“Tunao wajibu mkubwa kuhakikisha kwamba kila mmoja wetu
anafanya kazi kwa nguvu na bidii ili kutimiza matarajio ya Mheshimiwa Rais Dkt.
Magufuli na wananchi wote kwa ujumla,” amesema waziri mkuu.
Aidha waziri mkuu amewataka mawaziri wafanye ufuatiliaji na
tathmini ya utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo inayohusu sekta zao
kwa kuwa wao ni wasimamizi wa utekelezaji wa majukumu ya Serikali.
Post a Comment