NA
MWANDISHI WETU,
IGP Sirro akizungumza na polisi
wa Rwanda. Picha na mtandao.
|
TANZANIA na Rwanda Zimeunganisha nguvu kupitia Majeshi yao ya
Polisi chini ya wakuu wake IGP Simon Sirro wa Tanzania na RNP Emmanuel Gassana
wa Rwanda ili kupambana na uhalifu, ujangili na kuangalia namna ya kutatua
matatizo ambayo inazikumba nchi hizo.
Akizungumza na Waandishi wa habari Gassana
amesema kuwa lengo ni kushirikiana kutokana na changamoto ambazo zinatokea
katika nchi ikiwemo kuongeza nguvu, teknolojia, vifaa na kuongeza uzoefu wa
matumizi ya vifaa.
Kwa upande wake, IGP Sirro amesema kuwa kwa
ushirikiano huo ambao unafanyika kwa kuangalia nini ambacho kinatakiwa kufanya
na maarifa ambayo yatatumiwa ili Jeshi la Polisi liweze kufanya kazi yake kwa
usahihi na kupunguza uhalifu na endepo mtu akijiingiza kwenye uhalifu anaweza
kupoteza familia yake na kuishia pabaya.
“Wenzetu Rwanda wako mbele katika matumizi ya
teknolojia, hivyo kuna baadhi ya mambo ambayo watatuelekeza na tutapata uzoefu
katika kupambana na wahalifu wa mitandaoni ambao wamekuwa wakiwasumbua raia.
Sisi pia tuna uzoefu wa mambo mengi ambayo wenzetu Rwanda watajifunza kutoka
kwetu,” alisema Sirro.
Post a Comment