Upungufu wa matundu ya vyoo katika shule za msingi limeendelea kuwa ni tatizo kubwa katika shule mbalimbali za jiji la Dar es salaam.
Imebainika kuwa shule nyingi hasa za msingi idadi ya matundu haiendani na idadi ya wanafunzi katika shule zilizopo Dar es salaam hata mikoani pia.
Hayo yamesemwa mapema wiki hii na wanaharakati wa GDSS walipokuwa wanawasilisha ripoti ya zoezi walilopewa la kwenda kuulizia vipaumbele vilivyohainishwa katika serikali zao za mitaa kwa ajili ya bajeti kuu ya taifa ya mwaka 2017/18.
Katika zoezi hilo zilipata nafasi kata tatu kuweza kuwasilisha vipambele vyao walivyoweka katika kata zao, na kata hizo ni Kipunguni, Makumbusho na kata ya Mabibo.
Muwakilishi wa Kata ya Kipunguni Ndugu. Selemani Bishagazi akiwasilisha vipaumbele walivyoviweka katika kata yao ya Kipunguni mapema wiki katika semina ya GDSS. |
Kata ya Kipunguni na Makumbusho zimeonekana kuwa na matatizo yanayofanana kwa kuwa katika vipaumbele vyao wote walidai kuongezewa matundu ya vyoo katika shule zao pamoja na Zahanati ndio vitu wenye uhitaji navyo mkubwa katika maeneo yao.
Na Kipunguni ni kata mpya hivyo bado serikali haikuweka zahanati katika kata hiyo, na kata ya Makumbusho mwanzo walikuwa wakitumia hospitali ya Mwananyamara ambayo kwa sasa imekuwa Hospitali ya Rufaa na inakataa kupokea wagonjwa wa kawaida na kuwataka wapewe rufaa ndipo waende hospitalini hapo.
Kwa upande wa Kipunguni wao pia waliomba Kituo cha Polisi kwa kuwa katika eneo lao hakuna kituo hiyvo inawalazimu kutumia vituo vilivyopo kata nyingine kama Gongo la mboto nk, lakini pia waliomba vitambaa vya kujiifadhia watoto wakike(Pad) wawapo katika siku zao.
Licha ya kudai matundu ya vyoo na Zahanati Makumbusho kipaumbele chao kingine kilikuwa ni ukarabati wa shule ya Mwananyamara na Mianzini kwani mvua ikinyesha inaingia darasani na kufanya watoto kushindwa kusoma mpka wasubiri mvua ziishe.
Lakini pia wakazi wa Makumbusho waliomba kuwekewa ukuta katika shule zao kwani uvamizi wa watu unazidi mpaka katika maeneo ya shule na kufanya wanafunzi kushindwa kusoma akili na mawazo yao yanakuwa nje darasa.
Aidha katika hizi kata zote kata ya Mabibo imeonekana kuwa na changamoto chache sana na nyingi zikiwa tayari zimeshapatiwa ufumbuzi wake, ikiwa waliomba million 15 kwa ajili ya kujenga jingo jipya na ukuta ukuta wa Zahanati ya Mabibo vyote vimeweza kufanikishwa.
Wanaharakati kutoka sehemu mbalimbali za jiji la Dar es salaa wakimsikiliza kwa makini muwasilishaji wa vipumbele vya kata ya Mabibo ndugu. Msafiri Shabani Mapema wiki hii jijini Dar es salaam. |
Na jambo lingine lilikuwa ni vyumba vya kujiifadhia watoto wa kike na wakiume Mwalimu Mkuu wa Jeshini ameahidi kutoa vyumba viwili na Mwalimu wa Umoja ametoa ahadi ya kutoa kimoja, lakini pia walikuwa na mradi wa kujega shule ya Sekondari Kawawa wameshapata mfadhili na ujenzi utaanza hivi karibuni.
Na mwisho kabisa walikuwa na changamoto ya ujenzi wa Kivuko cha TASAF kilichoalibika na mvua, walineda kuwaomba msaada kiwanda cha NIDA Textile
wameambiwa watapewa million 20 kwa ujenzi huo na million 5 zilizobaki waombe Halmashauri.
Ndugu. Innocent Sirriwo akitoa maoni yake kuhusu mawasilisho ya vipaumbele yalikuwa yakifanywa na wanaharakati mbalimbali wa jiji la Dar es salaam. |
Post a Comment