MBUNGE wa Jimbo la Iringa Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mchungaji Peter Msigwa amefunguka na kusema kuwa katika Bunge ambalo linatarajiwa kuanza Novemba 7, 2017 anakusudia kupeleka hoja ya kumuondoa Spika wa Bunge, Job Ndugai
Msigwa amesema hayo leo kupitia moja ya mtandao wake wa kijamii na kusema kuwa kwa kuzingatia kanuni ya 137 ya kanuni za kudumu za Bunge atapeleka hoja yake hiyo ya kumuondoa Spika wa Bungue.
"Ninakusudia kupeleka hoja ya kumuondoa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Job Ndungai, kwa kuzingatia Kanuni ya 137 ya kanuni za kudumu za bunge ina complement ibara ya 84 (7) (d) ya Katiba" alisema Msigwa
Mbunge Peter Msigwa ni kati ya wabunge ambao wamekuwa wakilalamika kuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai amekuwa akiendesha bunge kwa shinikizo na upendeleo na kudai kuwa hastahili kuendelea kuongoza kiti hicho.
Chanzo .EATV
Post a Comment