Wakazi wa Kata ya Kipunguni wametakiwa kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo ili serikali iweze kuwaunga mkono kwa kumalizia miradi hiyo kama Rais alivyowataka kufanya hivyo.
Hayo yamesemwa na Mgeni Rasmi ambaye pia ni Diwani wa kata ya Kipunguni Mh. Mohamed Msofe alipoudhuria katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yaliyofanyika katika kata hiyo.Mh. Msofe aliwataka wa watu wa Sauti ya Jamii na Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kipunguni kutoa elimu kwa wakazi wa kata hiyo ili waweze kufahamu umuhimu wa kuchangia miradi ya maendeleo.
lakini pia diwani huyo aliwataka wakazi wa kata ya Kipunguni kuacha vitendo ya ukeketaji na kuelimisha wenzao kuhusu madhara ya ukeketaji kwa watoto wa kike kwani takwimu za mkoa zinaonyesha kuwa wilaya yao ndio inaongoza kwa vitendo hivyo.
Aidha diwani huyo aliwataka wakazi wa kata hiyo kuwapeleka watoto shule na kuacha kuwafanyisha kazi za majumbani na biashara kama kulima na kuwapa mabeseni ya kwenda kuuza mboga wakati wa masomo.
Na jambo lingine Diwani aliwataka wakazi wa kata hiyo kuwa na tabia ya kuwatii viongozi wao ili maendeleo yaweze kujengwa kwa pamoja kati ya wananchi na viongozi na sio mpaka washurutishwe katika wajibu wao.
Mwisho kabisa Diwani Msofe alipenda kuyapongeza mashirika likiwemo TGNP Mtandao pamoja na WILDAF kwa kuweza kuwasaidia wakazi wa kata hiyo kwa kuwapa elimu iliyowajenga mpaka sasa wamekuwa wakitoa msaada wa kisheria na huduma nyinginezo za kiharakati.
Wanaharakati wa Kata ya Kipunguni wakiwa wameshikilia mabango yenye jumbe mbalimbali wakati wa kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika kata hiyo mapema leo jijini Dar es salaam. |
Bw. Joven Silvester ambaye ni Mtendaji Kata wa Kipunguni akitoa neno la msisitizo, wakati wa kumkaribisha Diwani wa Kata hiyo katika maadhimisho ya siki 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, |
Diwani wa kata ya Kipungunia Mh. Mohamed Msofe akitoa ufafanuzi wa jambo fulani katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yaliyofanyika mapema leo katika Kata ya Kipunguni. |
Diwani wa Kipunguni Mh. Mohamed Msofe akiongea na wananchi wake wa Kata ya Kipunguni. |
Wanaharakati wanaotoa msaada wa kisheria katika Kata ya Kipunguni wakiwa katika picha ya pamoja |
Post a Comment