Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

CDF YAWAPIKA WANAHABARI KUWEZA KURIPOTI HABARI ZA KUTETEA NA KULINDA HAKI ZA MTOTO

Mkurugenzi Mtendaji wa Lecri Consuilt ambaye pia ni muwezeshaji wa semina ya kuwajengea uwezo wanahabari Bi. Edna Kamaleki iliyoandaliwa na Shirika la CDF makao makuu ya shirika hilo mapema leo jijini Dar es salaam.
Afisa habari wa shirika la Utu wa Mtoto(CDF) Michael Sungusia akitoa mchango wake katika semina ya kuwajengea uwezo wanahabari ili kuweza kuripoti habari za kulinda na kutetea haki za mtoto.
Baadhi ya wanahabari wakifuatilia kwa umakini semina iliyoandaliwa na shirika la Utu wa Mtoto(CDF) mapema leo jijini Dar es salaam.

Muwezeshaji wa semina ya kuwajengea uwezo wanahabari kuweza kuripoti habari za kulinda na kutetea haki za watoto Bi. Edna Kamaleki akiongea na wana habari mapema leo jijini Dar es salaam.

NA MUANDISHI WETU

Waandishi wa habari wametakiwa kuwa makini waandikapo habari za kuhusu watoto, hii ikiwa ni pamoja na kufuata misingi na sharia ya mtoto.

Hayo yamesemwa mapema leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Lecri Consult ambaye pia ni mshauri wa maswala ya haki za watoto Bi. Edna Kamaleki alipokuwa akiongoza semina kwa wanahabari kuhusu uvunjwaji wa haki za mtoto na namna ya kuzilinda haki hizo.

Bi Edna amesema kuwa vema wanahabari wanapotaka kutoa taarifa yeyote inayomuhusu mtoto kuzingatia maadili ya uandishi wa habari lakini pia sharia zinazomlinda mtoto huyo.

Sharia imeweka wazi kuwa mtoto aruhusiwi kupigwa picha au kurekodiwa pasipokuwa na ridhaa yake au mzazi/mlezi wake na pia hairuhusiwi kutumia sauti yake, jina kamili wakati akielezea au kufanya kitu chochote kitakacho mtambulisha yeye ni nani.

Mkurugenzi huyo aliendelea kusema kuwa sharia inamuhesabia makosa kwa mtu yoyote aliyeshuhudia au anajua kuwa kuna mtoto amekuwa akifanyiwa vitendo vya ukatili na hakuchukua hatua yeyote kama kutoa taarifa mahali husika, mtu huyo anapigwa faini ya shilingi 50 elfu au kifungo jela au mda mwingine vyote viwili.

Baada ya kusema hayo Bi. Edna alipenda kuwashauri watunga sera na viongozi walio katika ngazi ya maamuzi kujaribu kurekebisha baadhi ya sharia zinazokinzana pamoja na kurekebisha sharia zinazolalamikiwa kuwa zimepitwa na wakati na zinazowanyonya watoto hasa wa kike.

                   ANGALIA VIDEO HII KUJUA MENGI ZAIDI..
                     
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget