Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
akimjulia hali mtoto Nasib Robert,(kushoto) ni mama wa mtoto Veronica
Chilala,wakati alipo tembelea wodi ya watoto katika hospitali ya Wilaya
Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai
12, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
akizungumza na wananchi wakati alipo tembelea hospitali ya Wilaya
Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai
12, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
akikata utepe wakati alipo kabidhi gari mbili za kisasa za kubebea
wagonjwa,katika hospitali ya Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya
kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
akikagua gari ya kubebea wagonjwa wakati alipokabidhi gari mbili za
kisasa za kubebea wagonjwa,katika hospitali ya Wilaya Ruangwa, akiwa
kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
akikagua vifaa ndani ya gari la kubebea wagonjwa baada ya kukabidhi gari
mbili za kisasa za kubebea wagonjwa,katika hospitali ya Wilaya
Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai
12, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………………..
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amefanya ziara katika hospitali ya wilaya ya Ruangwa na amekabidhi
magari mawili ya kubebea wagonjwa.
Amesema kati ya magari hayo moja
ni kwa ajili ya hospitali hiyo ya wilaya na la pili litapelekwa katika
kituo cha afya cha Mandawa.
Waziri Mkuu amekabidhi magari
hayo leo (Jumatano, Julai 12, 2017), alipotembelea hospitali hiyo, ikiwa
ni siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi Mkoani Lindi.
Amesema magari hayo ni muendelezo wa mkakati wa Serikali ya awamu ya tano wa kuboresha huduma za afya kwa wananchi wake.
“Rais wetu Dkt. John Magufuli
amedhamiria kuwaondolea wananchi kero mbalimbali zinazowakabili zikiwemo
za huduma za afya, hivyo tuendelee kumuunga mkono.”
Waziri Mkuu amesema magari hayo
ya kisasa yatasaidia kurahisisha usafiri kwa wagonjwa wanaohitaji
matibabu ya dharura katika hospitali kubwa.
Kabla ya kukabidhi magari hayo,
Waziri Mkuu alitembelea wodi ya akina mama na ya watoto waliolazwa
katika hospitali hiyo na amesema kwamba ameridhishwa na hali ya utoaji
huduma.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa
Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Mheshimiwa Rashid Nakumbya amesema
magari hayo ni faraja kwao kwa kuwa walikuwa na changamoto ya usafiri
kwa wagonjwa wa dharura.
“Tunatambua na kuthamini jitihada
kubwa zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano katika halmashauri yetu
na Taifa kwa ujumla, nasi tutayatumia magari haya kama ilivyokusudiwa.”
Awali, Mganga Mfawidhi wa
Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa, Dkt. Regan Rajuu amesema hali ya
upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika hospitali hiyo umeongezeka
kutoka asilimia 80 Desemba, 2016 na kufikia asilimia 90 Juni 2017.
Pia Waziri Mkuu alitembelea shule
ya Sekondari ya Kassim Majaliwa iliyoanza kujengwa Desemba, 23, 2016
kwa michango ya Halmashauri, fedha za mfuko wa jimbo pamoja na wadau
mbalimbali wa maendeleo.
Kaimu Mkuu wa shule hiyo, Mwalimu
Emmanuel Sechawe alisema msingi wa kuanzisha shule hiyo ulitokana na
uwepo wa wanafunzi 319 waliofaulu darasa la saba mwaka 2016 kukosa
nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza katika shule zilizopo.
Mbali na kutembelea shule hiyo,
pia Waziri Mkuu alifanya ukaguzi wa maendeleo ya mradi wa ujenzi wa
gereza la wilaya ya Ruangwa, ambalo litakapokamilika litapunguza
msongamano wa wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya
Nachingwea.
Post a Comment