Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi
akisaini kitabu cha wageni alipotembelea katika viwanja vya Maonyesho ya
Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi
akiwaeleza viongozi mbalimbali waliotembelea viwanja vya maonyesho ya
Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jinsi Taasisi
yake inavyofanya kazi za kutibu magonjwa ya Moyo na umuhimu wa kupima
afya mara kwa mara japo mara moja kwa mwaka.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi
akiongea jambo na Mkurugenzi wa Huduma za Biashara wa Tan Trade Fidelis
Mugenyi wakati alipotembelea maonyesho ya Kimataifa ya biashara
yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini
Dar es Salaam.
Daktari
Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Aika Nnkya akimsikiliza Haubert Makoke ambaye alimuuliza swali
kuhusu magonjwa ya Moyo wakati alitembelea banda la Taasisi hiyo
lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho
ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ajili
ya kupima magonjwa ya Moyo bure, kupata ushauri na kuona huduma
mbalimbali za matibabu ya moyo wanazozitoa.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi
akimpa ushauri kuhusu afya ya Moyo Mzee John Lihame aliyembelea banda la
Taasisi hiyo lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja
vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere kwa ajili ya kupima magonjwa ya Moyo bure, kupata ushauri na
kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo wanazozitoa.
Daktari
Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Bashir Nyangasa akiwaonyesha wananchi waliotembelea
banda la Taasisi hiyo lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi
katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere jinsi upasuaji wa Moyo unavyofanyika.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi
akijibu maswali mbalimbali kuhusu magonjwa ya moyo aliyoulizwa na
wananchi waliotembelea banda la Taasisi hiyo lililopo ndani ya Hema la
Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara
vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Wananchi hao walifika katika banda
hilo kwa ajili ya kupima magonjwa ya Moyo bure, kupata ushauri na
kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa.
Afisa
Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Fatuma Mkomwa akimpima
mapigo ya moyo (BP) Mzee Mwanga ambaye alifika katika banda la Taasisi
hiyo lililopo ndani ya Hema la Ally Hassan Mwinyi katika viwanja vya
Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
kwa ajili ya kupima magonjwa ya Moyo bure, kupata ushauri na kuona
huduma mbalimbali wanazozitoa.
Neema
Juma akimsikiliza kwa makini Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Pedro Pallangyo wakati akimweleza
namna anavyoweza kuishi na kuepukana na magonjwa ya moyo. Neema
alitembelea banda la Taasisi hiyo lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan
Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya kupima magonjwa ya Moyo bure,
kupata ushauri na kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo
wanazozitoa.
Wananchi
wakiwa katika mstari wa kupima magonjwa ya Moyo bure na kupata
ushauri katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya
Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi (kushoto)
akibadilishana mawazo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tan trade Edwin
Rutageruka (kulia) na Mkurugenzi wa Huduma za Biashara wa Tan Trade
Fidelis Mugenyi (katikati) alipotembelea maonyesho ya Kimataifa ya
biashara yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere jijini Dar es Salaam.
Picha na JKCI
Post a Comment