Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla amekabidhi jumla
ya vifaa 831 vyenye thamani ya jumla ya Shilingi milioni 400, kwa kituo
cha Afya Mkoani Kibaha Mjini, vifaa vilivyotolewa na Mbunge wa jimbo
hilo, Mh. Silvestry Koka.
Awali kabla ya kukabidhi vifaa hivyo,
Dk. Kigwangalla alipata wasaha wa kukagua maeneo ya majengo ya Kituo
hicho cha Afya huku akbaini mambo mbalimbali aliyoagiza yafanyiwe kazi
ili kituo hicho kiweze kuwa Hospitali ya Wilaya pindi itakapokamilisha
vigezo
Wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Dk.
Kigwangalla alipongeza juhudi za Mh. Koka kwa kujali wananchi wake kwani
hadi kuweza kupata vifaa hivyo aliweza kutumia maarifa na ukaribu wake
na wananchi wake hivyo kufika kwa vifaa hivyo vitakuwa faraja kubwa kwa
Wanakibaha na wananchi wote wa maeneo jirani.
“Nampongeza Mbunge Koka kwa
kuwaletea vifaa hivi. Kwani ni vizuri na vitakuwa msaada mkubwa kwa
wananchi wa Kibaha na maeneo yake ya jirani. Nakupongeza sana sana” alieleza Dk. Kigwangalla wakati wa tukio hilo la kukabidhi vifaa hivyo.
Aidha, aliwataka wananchi wa Kibaha
mjini waweze kuwa karibu na Mbunge wao na wamwamini kwani anawajali ndio
maana anawatumikia kwa kila njia ikiwemo kuwaletea maendeleo kwa
ujumla.
Kwa upande wake, Mbunge wa Kibaha Mjini
Mh. Silvestry Koka amemshukuru Naibu Waziri Dk. Kigwangalla kwa kuweza
kufika na kujionea Kituo hicho sambamba na kukabidhi vifaa huku
akimuomba kuendelea kufika mara kwa mara kujionea mipango ya Afya
jimboni humo.
“Leo hiii najisikia faraja kwa
vifaa hivi kuweza kufika hapa jimboni kwangu kutoka nchini Marekani.
Nawaomba vitumike kwa uangalifu mkubwa sana na viweze kuwa msaada kwetu” alieleza Mh. Koka.
Awali alieleza kuwa, kiasi cha shilingi
milioni 32 fedha zilizotolewa na Halmshauri ya mji wa Kibaha ziweza
kusaidia usafirishaji wa vifaa hivyo kutoka nchini Marekani huku yeye
kama Mbunge akitumia gharama ya shilingi milioni 12 kwa ajili ya
kuwaleta wataalam kwa ajili ya ukaguzi na kuvifunga vifaa hivyo.
Mbunge huyo ameeleza kuwa, vifaa hivyo
vitagawia katika zahanati na vituo vyote vilivyopo mjini Kibaha na
maeneo mengine yenye uhitaji.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza katika tukio hilo la
kukabidhi vifaa tiba vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini,
Mh. Koka
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla akikabidhia nyaraka zenye vifaa tiba akikabidhiwa na
Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini, Mh. Koka
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla akikabidhi nyaraka yenye idadi ya vitu hivyo vya vifaa tiba
kwa uongozi wa Kituo cha Afya Mkoani Kibaha Mjin wakati wa tukio hilo
la kukabidhi vifaa tiba vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha
Mjini, Mh. Koka
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla akishuhudia vitu hivyo vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la
Kibaha Mjini, Mh. Koka
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi akiwa katika picha wakati wa
tukio hilo
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla kisalimiana na na uongozi wa Mkoa na Wilaya ya Kibaha
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla akisaini kitabu cha wageni kwa ofisi ya Wilaya ya Kibaha
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla akisalimiana na baadhi ya Madiwani wa Jimbo la Kibaha Mjini
Baadhi ya vifaa tiba vilivyokabodhiwa leo
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla akifanya ukaguzi katika maeneo mbalimbali ya kituo cha Afya
Mkoani
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla akikagua eneo la mahabara katika kituo cha Afya Mkoani,
Kibaha Mjini
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla akikagua eneo la Chumba cha Upasuaji katika kituo cha Afya
Mkoani, Kibaha Mjini
Baadhi ya vifaa vilivyotolewa na mbunge wa jimbo hilo
Wakiangalia vifaa hivyo
Mbunge wa Kibaha Mjini Mh. Koka akielezea namna vifaa hivyo
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla akipiga picha ya pamoja na baadhi ya watendahi wa
Hospitali ya Mkoa, Kituo cha Afya Mkoani na Mganga Mkuu wa Mkoa
Post a Comment