Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Jiji la Dar es Salaam lapata tuzo kupitia Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka

Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita wa kwanza kushoto mstari wa mbele akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wengine huko Chicago Nchini Marekani wakiwa wameshika tuzo zao.
JIJI  la Dar es Salaam ni miongoni mwa majiji 10 duniani ambayo yamepata tuzo ya C40 Bloomberg Philantropies 2017   kupitia Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka.
Katika tuzo hiyo  mwaka huu imepokelewa na Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Miwta aliyerejea nchini alfajiri ya Desemba 8 mwaka huu.
 Picha ya tuzo ya C40 Bloomberge Philantropies iliyotolewa kwa jiji la Dar es Salaam Chicago Nchini Marekani.
Jiji la Dar es Salaam limechangia tuzo hiyo  na Jiji la New York  nchini Marekani na .
Mradi wa Mabasi yaendayo haraka unawahudumia abiria 200,000 kila siku kwa kutumia mabasi ya kisasa ambayo yanachangia kupunguza msongamano wa magari barabarani na kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa na hivyo kuwa siri ya mafanikio ya tuzo jijini hapa.
Tuzo ya C40 Bloomberg Philanthropies hutolewa kila mwaka katika miradi inayotekelezwa kwenye maeneo mahususi matano ili kutambua jitihada za majiji wanachama wa Taasisi ya mtandao wa Majiji zaidi ya 90 duniani inayoshughulika na namna bora ya kukabiliana na Athari za mabadiliko ya Tabia ya Nchi Duniani.
Imetolewa leo Desemba 10
Na Christina Mwagala , Afisa Habari Ofisi ya Mstahiki Meya wa jiji.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akitoa neno la shukrani baada ya kukabidhiwa tuzo ya C40 Bloomberge Philantropies .
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget