Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

January 2018

Baraza la Mitihani la Tanzania limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) leo Januari 30, 2018 ambapo kiwango cha ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 7 ukilinganisha na mwaka jana 2016.

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde ametangaza matokeo hayo leo jijini Dar es Salaam na kusema ufaulu kwa wanafunzi umeongezeka kwa asilimia 7 ukilinganisha na matokeo ya mwaka jana.

"Jumla ya Watahiniwa 287,713 ambao sawa na asilimia 77.09%  kwa shule za kawaida na vituo vya kujitegemea wamefaulu ambao katika ya hao wasichana wapo 143,728 sawa na asilimia 75.21% wakati wavulana wapo 143,985 sawa na asilimia 79.06%. Mwaka jana wanafunzi waliofaulu mitihani ya kidato cha nne walikuwa 277,283 ambao ni asilimia 70.09% hivyo ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 7" alisema Msonde

Mbali na hilo Msonde aliweza kuweka wazi kuwa jumla ya wanafunzi 265 wamebainika kufanya udanganyifu mbalimbali katika mitihani hiyo ambayo ilianza kufanyika Oktoba 30, 2016 mpaka Novemba 17, 2016


 Shule 10 kitaifa ambapo shule iliyoongoza  inatoka Mkoani  Mbeya.shule hizo ni 
TOP 10 YA SHULE BORA.
1. St. Francis Girls ya Mbeya
2. Feza Boys ya Dar es salaam
3. Kemebos ya Kagera 
4. Bethel Sabs Girls ya Iringa 
5. Anwarite Girls ya Kilimanjaro 
6. Marian Girls Pwani 
7. Canossa ya Dar es salaam 
8. Feza Girls ya Dar es salaam 
9. Marian Boys ya Pwani 
10. Shamsiye Boys ya Dar es salaam 
TOP 10 YA SHULE ZA MWISHO KITAIFA
10. Mtule ya Kusini Unguja
9. Nyeburu ya Dar es salaam
8. Chokocho ya Kusini Pemba
7. Kabugaro ya Kagera
6. Mbesa ya Ruvuma
5. Furaha ya Dar es salaam
4. Langoni ya Mjini Magharibi
3. Mwenge S.M.Z ya Mjini Magharibi
2. Pwani Mchangani ya Kaskazini Unguja
1. Kusini ya Kusini Unguja

MAAMUZI YA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI KUHUSU RUFAA MOJA YA MGOMBEA UBUNGE NA RUFAA TANO ZA WAGOMBEA UDIWANI

Kwa kuzingatia masharti ya Kifungu cha 40(6) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, ikisomwa pamoja na Kanuni za 34 na 35 za Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2015, Tume ilipokea Rufaa moja (1) kutoka kwa Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) akipinga maamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo kuhusu pingamizi alilomuwekea Mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Aidha, kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 44 (5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, ikisomwa pamoja na Kanuni za 28 na 29 za Kanuni za Serikali za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani) za mwaka 2015, Tume ilipokea Rufaa tano (5) za Wagombea  Udiwani  kutoka katika Kata ya Isamilo – Halmashauri ya Jiji la Mwanza, wakipinga Maamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo.  Rufaa tatu (3) ni za wagombea walioondolewa kwenye kugombea ili warejeshwe na Rufaa mbili (2) zinaomba Tume itengue uteuzi wa mgombea Udiwani aliyeteuliwa katika Kata hiyo.

Katika kikao chake cha kawaida kilichofanyika tarehe 26 Januari 2018 siku ya Ijumaa, Tume ilipitia Rufaa hizo na kuamua kama ifuatavyo:

Mosi, kuhusu Rufaa ya Mgombea Ubunge, Tume imekubaliana na maamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi na hivyo Mgombea aliyekatiwa Rufaa wa CHADEMA anaendelea kuwa mgombea wa Ubunge Jimbo la Kinondoni.

Pili, kuhusu Rufaa za Wagombea Udiwani Kata ya Isamilo katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza, kupinga kuondolewa kugombea Udiwani katika Kata hiyo, Tume imewarejesha kuwa Wagombea Udiwani wawili wa vyama vya CHADEMA na CUF.

Tatu, Tume imekubaliana na maamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi ya kumuondoa katika orodha ya wagombea Udiwani mgombea wa Chama cha UDP. Hivyo hatakuwa mgombea katika kata hiyo

Nne, Tume imekataa rufaa mbili zilizokuwa zinapinga uteuzi wa mgombea wa CCM aliyeteuliwa katika Kata hiyo na hivyo, mgombea wa CCM anaendelea kugombea Udiwani katika kata husika.

Taarifa rasmi za maamuzi ya Tume zimetumwa kwa Wasimamizi wa Uchaguzi ili wawapatie wahusika maamuzi hayo.

Kailima, R.K
MKURUGENZI WA UCHAGUZ

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Makarani Khamis , akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, juu ya eneo la Tunguu lililoko Mkoa wa Kusini Unguja  ambalo ni mali ya Jeshi la Polisi, hivi sasa likimilikiwa na wananchi kinyume cha sheria.Kushoto ni Mkuu wa mkoa huo, Hassan Khatib Hassan. Naibu Waziri yuko Visiwani Zanzibar kwa ziara ya kikazi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Hassan Khatib Hassan, akizungumza na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni baada ya kukagua makazi ya askari polisi yanayoonekana pichani, yaliyopo eneo la Machui, lililopo Mkoa wa Kusini Unguja.Naibu Waziri yupo Visiwani Zanzibar kwa ziara ya kikazi ya kukagua maeneo yanayotarajiwa kujengwa vituo vya polisi na makazi ya askari.Kulia ni Kiongozi wa Chama cha Mapinduzi mkoani hapo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na viongozi wa Mkoa Kusini Unguja alipowasili leo  mkoani hapo kwa ziara ya kikazi ya kukagua maeneo yanayotarajiwa kujengwa vituo vya polisi na makazi ya askari.Kulia ni Kiongozi wa Chama cha Mapinduzi mkoani hapo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Mbunge wa Ubungo, Said Kubenea ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Kanda ya Pwani amefunguka na kusema mgombea wa Ubunge wa jimbo la Kinondoni kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu kuwa ni mtu makini na ndiye Lissu mdogo ambaye anastaili kwenda Bungeni.
Image result for kubenea
Kubenea amesema hayo leo Januari 27, 2018 kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa marudio ambao unatarajiwa kufanyika Februari 17, 2018 katika majimbo mawili ya Kinondoni na Siha.

Kubenea amesisitiza kuwa mgombea huyo ni kati ya watu makini ambao wanapaswa kufika Bungeni kuwatetea wananchi wa Kinondoni.

"Nina mfahamu Salum Mwalimu ni kati ya waandishi wa habari wachache nchi hii walio jasiri na wasioogopa wanafanya kile wanachokiamini, ameandika stori kubwa na kuripoti matokeo makubwa sana na kutetea hadhi za binadamu, amefanya kazi kubwa kutetea misingi ya uandishi wa habari mkimpeleka Bungeni mtakuwa mmetupeleka chachu nyingine, mtakua mmemleta Lissu mwingine mdogo na kwenda kumpandikiza Bungeni" alisema Kubenea

Mbali na hilo Kubenea aliwataka wananchi kupuuza maneno yanasosambazwa kuwa Salum Mwalimu si Mtanzania na kusema huyo ni raia wa Tanzania na amekulia Tanzania bara hivyo waachane na maneno hayo yanayosambazwa na watu wa Chama Cha Mapinduzi

Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akimweleza mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu namna ambavyo Kituo cha Utafiti Mikocheni kinavyochangia kwenye kuongeza tija na uzalishaji katika Sekta ya Kilimo kushoto kwa Dkt. Mwanjelwa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Dkt. Thomas Kashillilah
Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu katika moja ya maabara ya Kituo cha Utafiti Mikocheni
Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu wakimsikiliza Mkuu wa Idara ya Udhibiti wa Magonjwa ya Mimea Dkt. Deusdeth Mbanzibwa katika moja ya maabara ya Kituo cha Utafiti Mikocheni
Aina za mbegu mbalimbali za mihogo ambazo ni Sehemu ya matokeo ya tafiti zinazoendeshwa na Kituo cha Utafiti Mikocheni ambazo Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu walipata nafasi ya kujionea
Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu wakimsikiliza Mtafiti Mwandamizi wa Kituo cha Mikocheni Dkt Aloyce Kulaya ambaye amewaeleza faida za mbegu za mahindi ziligunduliwa Kituoni hapo kupitia Mradi wa WEMA
Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Dkt. Qu Dongyu wakimsikiliza Dkt. Christopher Materu Mkuu wa Idara ya Udhibiti wa Wadudu na Magonjwa kutoka Kituo cha Utafiti Mikocheni namna nzuri ya kudhiti magonjwa ya mimea kwa kutumia wadudu marafiki

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Dkt Mary Mwanjelwa ameishukuru Serikali ya China kwa kuonyesha nia ya kusaidia eneo la utafiti na maendeleo hususan kwenye kuendeleza zao la minazi na mihogo kupitia Kituo cha Utafiti wa Mazao cha Mikocheni JIJINI Dar es Salaam.

Dkt Mwanjelwa amemshukuru Serikali ya China kupitia Naibu Waziri wa Kilimo wa China Dkt Qu Dongyu mara baada ya kufanya ziara katika Kituo hicho mapema leo.

Katika Wasilisho lake kwa ugeni wa Waziri huyo wa Kilimo kutoka China, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Utafiti Mikocheni Dkt Fred Tairo amesema Kituo kimekuwa kikiendesha tafiti mbalimbali zenye lengo la kuzuia na kukabiliana na magonjwa hatari ya minazi na mihogo lakini kikwazo kikubwa kimekuwa teknolojia hafifu na uzoefu mdogo katika nyanja hiyo.

Mara baada ya wasilisho hilo Naibu Waziri wa Kilimo wa China ambaye anataaluma ya kilimo amesema Serikali ya China ipo tayari kuisaidia Tanzania kwenye maeneo ya utafiti wa kuzuia magonjwa ya mazao kwenye minazi na mihongo na kutoa wito kwa Watafiti wa Tanzania kuongeza juhudi katika kubunia teknolojia mbazo zitakuwa rahisi na rafiki kwa Wakulima wa Tanzania ili iwe rahisi kuziuza na baadae pato lake lisaidie Kituo hicho kujiendesha.

Dkt Qu Dongyu yupo nchini kwa ziara ya Kiserikali pamoja na Mwenyeji wake, Dkt Mary Mwanjelwa ambapo wote kwa pamoja wamepata nafasi ya kuitembelea maabara ya Kituo cha Utafiti Mikocheni na kujionea matokeo ya tafiti mbalimbali.

Akizungumzia kuhusu uwezeshaji wa Serikali ya China kwa Kituo cha Utafiti Mikocheni, Mtafiti Mwandamizi wa Kituo cha Mikocheni Dkt Aloyce Kulaya amesema kwa sehemu kubwa Kituo kimekuwa kikipata uwezeshaji kutoka Serikalini pamoja na Wabia wa Maendeleo kama Mfuko wa Bill and Belinda Gates Foundation na kuongeza kuwa uwezeshaji kama kutoka Serikali ya China utaongeza tija na uzalishaji katika mazao mengine si kwa minazi na mihogo tu.

Dkt Qu Dongyu anataraji kumaliza ziara yake ya Kiserikali hapo kesho kwa kukutana na Wawekezaji wa China waishio Tanzania na baadae atareje nyumbani siku hiyo ya Jumamosi.

 
BODI ya  Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inawataarifu wanafunzi wanaonufaika na mikopo kuwa  wanatakiwa kuendelea kuingiza taarifa zao kwa njia ya mtandao kupitia http://olas.heslb.go.tz  hadi tarehe 31 Januari, 2018.

Wanafunzi wanufaika wanapaswa kufanya yafuatayo:

•    Tembelea mtandao wa http://olas.heslb.go.tz

•  Fungua kiunganishi cha “Click here to start” kwenye maelezo ya mwanzo ya kukaribisha.

•    Weka namba yako ya mtihani ya Kidato cha Nne na mwaka uliofanya mtihani huo, kwa mfano: S0129.0004.2020

•   Weka namba yako ya akaunti ya Benki kama ilivyowasilishwa HESLB au kama inavyoonekana kwenye “signing sheet”

•    Ingiza neno jipya la siri na ulithibitishe.

•   Baada ya kuthibitisha, ukurasa wa kuweka picha yako “passport size photo” utafunguka.

•    Weka picha yako ya rangi katika ukubwa wa 120×150

•    Wanufaika wapya wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2017/2018 hawatahusika kwenye zoezi hili kwa vile taarifa zao ziliwasilishwa wakati wa kuomba mikopo.

Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Tarehe 26/01/2018


  MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amemtetea mchezaji wa zaman wa klabu 
aliyehamia Manchester United baada yake kukosa kipimo muhimu kuhusu matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mwilini.

Aidha, amesema klabu hiyo haifichi habari zozote kuhusu tukio hilo.

Raia huyo wa Chile mwenye miaka 29 anadaiwa kukosa kipimo muhimu Jumatatu siku ambapo alikamilisha uhamisho wake kwenda Manchester United.

"Nafikiri lilikuwa tukio la kipekee, kwake kukosa kipimo siku hiyo kwa sababu alikuwa kwingine," amesema Wenger.

Mfaransa huyo ameongeza pia kwamba klabu yake haijaombwa ufafanuzi wowote na Chama cha Soka cha England au Shirika la kupambana na matumizi ya dawa zilizoharamishwa michezoni Uingereza.

Sanchez alihamia Gunners kutoka Barcelona mwaka 2014, lakini alielekea Old Trafford kwa kubadilishana na mchezaji wa Armenia Henrikh Mkhitaryan.

Baada ya taarifa za awali Uhispania, magazeti ya Uingereza Alhamisi yaliripoti kwamba Sanchez alikiuka kanuni FA ya kupatikana wakati wowote ule anapotakiwa kupimwa.

Sanchez na Mkhitaryan walipigwa picha wakiwa afisi za uhamiaji Liverpool wakitafuta vibali vya kufanya kazi kabla ya kukamilisha uhamisho wake.

Wenger amesema: "Jumatatu kulikuwa na mengi sana yaliyokuwa yanatokea, ni siku ya kipekee sana kwa Alexis Sanchez - kujaza stakabadhi muhimu, vibali vya kazi na usafiri. Alikuwa bado ni mchezaji wetu Jumatatu au la? Huwezi kujua.

"Ni siku mbaya tu kwako kutafutwa ukapimwe. Kusema kweli, ukiangalia upande wa usimamizi, huenda ikawa bado ilikuwa ni wajibu wetu kwa kuwa hakuwa amehama. Sijui nini hasa kilitokea.

"Sina wasiwasi kwa sababu hatuna chochote cha kuficha, huwa tunajaribu sana kadiri ya uwezo wetu kushirikiana na maafisa wa kupambana na matumizi ya dawa zilizoharamishwa michezoni Uingereza.

"Nia ya Alexis haikuwa kujificha na sisi hatuna jambo la kuficha."

Sheria zinasemaje?

Klabu zinatakiwa kutoa maelezo sahihi ya kina kuhusu vipindi vya mazoezi na walipo wachezaji ili waweze kupimwa wakati wowote ule.

Klabu ikikosa kufanya hivyo - au maafisa wa kupima wachezaji washindwe kumpata mchezaji wanayemtafuta - mara tatu kipindi cha miezi 12, basi huchukuliwa kwamba amekiuka sheria za FA.

Manchester City na Bournemouth mwaka jana walitozwa faini ya £35,000 kila mmoja na kutahadharishwa baada ya kukiuka kanuni hizo.

Arsenal wamemnunua yeyote?

Wenger amesema hawapo karibu kumnunua mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang. Ofa yao ya pili ya euro 50m (£43.64m) ilikataliwa wiki hii.

Borussia wanaaminika kutaka walipwe zaidi ya £50m kwa mchezaji huyo wa Gabon wa miaka 28.

Wenger pia amesema hataki kumpoteza Olivier Giroud.

 

MKUU wa Simba Mfaransa, Pierre Lechantre anatarajiwa kukaa kwa mara kwanza kwenye benchi la timu hiyo kesho Jumapili wakati watakapoivaa Majimaji ya Ruvuma, lakini amechimbwa mkwara na straika wa wapinzani wao hao.

Jerry Tegete ambaye ni straika wa Majimaji FC inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya Sokabet, amedai anataka kuvuruga ‘fungate’ la Simba na kocha huyo ambaye ameanza kazi Jumanne wiki hii.

Majimaji itaivaa Simba katika mechi ya Ligi Kuu Bara itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo awali Majimaji ilitoka sare ya bao 1-1 na Yanga mkoani Ruvuma.

Kocha wa Simba alitua nchini wiki iliyopita na kusaini mkataba wa miezi sita wa kuifundisha timu hiyo akiwa pamoja na msaidizi wake raia wa Tunisia, Mohammed Aimen.

Tegete alisema ujio wa kocha huyo mpya hauwafanyi wao waogope na kupata matokeo mabaya, kwani wataingia uwanjani kwa ajili ya ushindi pekee.

“Kama unavyojua ligi inaelekea katika mzunguko wa pili, hivyo ni lazima tushinde michezo yote iliyokuwepo mbele yetu ili tujiweke katika nafasi nzuri katika msimamo,” alisema Tegete.

Alisema walianza na sare mbili kutoka kwa timu kubwa zenye upinzani mkubwa ambazo ni Azam FC na baadaye Singida United, hivyo wanaofuata ni Simba.

 “Tunajua Simba wameleta kocha mpya Mfaransa, lakini hiyo haitufanyi sisi kuwaogopa, kwani tuna timu imara itakayoleta ushindani, tumetoka 

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika Serikali ya Awamu ya Nne, Bernard Membe wamekutaka katika msiba wa mama wa Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.

Membe na Lowassa wamekutana leo Alhamisi Januari 25,2018 nyumbani kwa Askofu Gwajima, Salasala wilayani Kinondoni.

Wawili hao walijitosa katika kura ya maoni ya CCM kuwania kupitishwa na chama hicho tawala kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Katika mchakato huo jina la Lowassa lilikatwa mapema, huku Membe akiwa miongoni mwa wagombea watano waliopitishwa na Kamati Kuu ya CCM. Walishindwa na John Magufuli aliyepeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi huo na kuibuka na ushindi.

Ruth Basondole, mama mzazi wa Askofu Gwajima amefariki dunia akiwa na miaka 84

MBUNGE wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mohammed Razar, amemkabidhi msaada wa chakula kwa Waziri, Kassim Majaliwa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wenye uhaba wa chakula.
Akikabidhi misaada hiyo mapema leo katika ofisi ya waziri mkuu jijini Dar es salaam Bw. Razar alisema kuwa anatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi kwani ndio chama tawala na ndio chenye dhamana ya kuhakikisha wananchi wake wanakuwa katika hali ya usalama.

Mbali na hilo, Razar amempa nafasi Majaliwa amchagulie mikoa mitano ambayo itafanyiwa mashindano na kila mkoa utatoa timu ya taifa ya michezo ya watoto wa shule, ambapo mashindano hayo atayagharamia yeye mwenyewe kuanzia jezi, mazoezi na vitu vingine.

Aidha, Razar ameelezea dhamira yake ya kutaka mashindano hayo yaanzishwe ni kutokana na timu za mpira Tanzania, kuwa na idadi kubwa ya wachezaji kutoka nchi jirani kuliko wale wanaotoka nyumbani, hivyo anachokitaka ni kuzalisha vipaji na kuvikuza vije kuchezea timbu zao hapo baadae.
Lakini pia mbunge Razar alipenda kuwapongeza Marais wote wawili akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dr. Magufuri na Dr, Sheni kwa kazi nzuri wanazozifanya za kutetea maslahi ya watanzania na kuwakomesha mafisadi.

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget