Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

June 2017

unnamed
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia)akizungumza pale ugeni kutoka Umoja wa Wanamichezo wa Mpira wa Miguu kutoka FC GRACE UNITED STATES ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. wa pili kulia ni Mwenyeji na kiongozi wa Msafara Bishop Oscar John.
1
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akimsikiliza Mheshimiwa William Ngeleja akizungumza wakati Umoja wa Wanamichezo wa Mpira wa Miguu kutoka FC GRACE UNITED STATES ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
3
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia)akimsikiliza Bishop Oscar John (aliesimama) akizungumza, pale ugeni kutoka Umoja wa Wanamichezo wa Mpira wa Miguu kutoka FC GRACE UNITED STATES ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
6
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kulia) akizungumza na ugeni kutoka Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania ulioongozwa na Rais wa Chama hicho Ndg. Mwadini Jecha (katikati) na Mratibu wa Mawasiliano Ndg. Anne kilimo (kushoto) uliomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
3
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Washindi wa Medali za Dhahabu katika Mashindano ya kimataifa ya Mazingira na Sayansi yaliyofanyika hivi karibuni nchini Marekani. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Shule ya Wavulana ya Feza Ndg. Ibrahim Rashid, anaefuata ni Ndg. Rashid Kikwete, kulia ni Mhe. Hawa Ghasia, wa pili kulia ni Ndg. Kassi Nkamia na watatu kulia ni Ndg. Abdallah Rubeya, waliotembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
4
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na ugeni kutoka Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania ulioongozwa na Rais wa Chama hicho Ndg. Mwadini Jecha (kushoto waliokaa) baada ya kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
5
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kulia) akimsikiliza Rais wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania  Ndg. Mwadini Jecha (katikati) pale ugeni kutoka Chama  hicho ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma, kushoto ni Mratibu wa Mawasiliano Ndg. Anne kilimo.

1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Borge Brende aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
2 3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha  na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Borge Brende wanne kutoka (kushoto), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga wanne kutoka (kulia)pamoja na vingozi wengine wa Tanzania na Norway mara baada ya mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.
4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Borge Brende mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwatazama Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Borge Brende wakati akizungumza jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

unnamed
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akifuatilia mjadala katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Pamoja iliyokuwa ikijadili miswada miwili ya sheria  kuhusiana na usimamizi wa maliasili za Nchi.kikao hicho kilifanyika Mjini Dodoma jana Katika Ukumbi wa Msekwa.
1 2
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akifuatilia mjadala katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Pamoja iliyokuwa ikijadili miswada miwili ya sheria  kuhusiana na usimamizi wa maliasili za Nchi.kikao hicho kilifanyika Mjini Dodoma jana Katika Ukumbi wa Msekwa.


1
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakijadili kwa umakini na katibu mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wakiongea na waandishi wa habari(Hawapo kwenye picha) juu ya taarifa ya kuibiwa kwa mtoto mmoja wa Bi. Hasma Juma katika hospitali ya Temeke jijini Dar Es salaam.




Na Jonas Kamaleki-MAELEZO
Mkazi wa Mkoa wa Iringa, Thomas Lubinza ametembea zaidi ya kilometa 502 kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada zote anazozifanya katika kulinda na kusimamia raslimali za watanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari, Lubinza amasema kuwa Rais Magufuli kwa kipindi kifupi cha uongozi wake ameweza kufanya mambo makubwa ikiwemo kudhibiti na kupambana na vitendo vya rushwa, kurudisha nidhamu serikalini na kuboresha miundombinu.
Licha ya juhudi hizi zinazofanywa na Mhe. Magufuli,wapo ambao wanabeza jitihada hizi na wengine kukejeli, alisema Lubinza na kuongeza kuwa yeye ameona ni vyema ajitokeze kumpongeza.

  mail.google.com
                                                               
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema msimamo wa Serikali wa kuzuia usafirishaji wa chakula kwenda nje ya nchi uko pale pale.

Pia amesema mahindi iliyokamatwa mkoani Kilimanjaro yakisafirishwa kwenda nje ya nchi yataingizwa kwenye Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) na magari yatabaki polisi.

NA BASHIR NKOROMO
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kinaridhishwa sana na kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli kwa kuwa serikali hiyo imejikita ipaswavyo katika kutekeleza ilani ya Chama ikiwemo kuipeleka Tanzania katika nchi ya Uchumi wa Viwanda.


Akizungumza na Waandishi wa habari katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole, amesema, CCM imefikia hatua ya kutoa tamko rasmi la kuridhishwa kwake na utendaji kazi wa Serikali hiyo, baada ya Chama kufanya ziara ya uhakiki wa hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa viwanda vikubwa, vya kati na vidogo katika mkoa wa Pwani.

NIS1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohanmed Shein (kushoto) akimtunuku Nishani ya Mapinduzi kwa Viongozi na Wananchi wenye Sifa Maalum Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Pamdu Ameir Kificho katika hafla ya Sherehe Maalum ya Kutunuku nishani mbali mbali iliyofanyika leo katika Viwanja vya Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 29/06/2017.
NIS2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohanmed Shein (katikati) akitunuku Nishani ya Mapinduzi kwa Viongozi na Wananchi wenye Sifa Maalum (pichani) Bw.Aboud Talib Aboud akitukiwa nishani  katika hafla ya Sherehe Maalum ya Kutunuku nishani mbali mbali iliyofanyika leo katika Viwanja vya Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 29/06/2017.
NIS3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohanmed Shein (kulia) akitunuku Nishani ya Mapinduzi kwa Viongozi na Wananchi wenye Sifa Maalum (pichani) Dk.Msimu Abdulrahman  Hassan akitunukiwa Nishani  katika hafla ya Sherehe Maalum ya Kutunuku nishani mbali mbali iliyofanyika leo katika Viwanja vya Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 29/06/2017.

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget