Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Dangote aonya sera za uwekezaji za Magufuli

Aliko Dangote, Tajiri namba moja barani Afrika Aliko Dangote, Tajiri namba moja barani Afrika
TAJIRI namba moja barani Afrika Aliko Dangote ambaye pia ni mwekezaji mkubwa nchini Tanzania amemuonya Rais John Pombe Magufuli kuwa sera zake nchini humo zinawaogopesha wawekezaji.

Dangote ambaye amewekeza dola za kimarekani 650 kwenye uzalishaji wa saruji, amesema wakati umefika kwa raisi Dk. Magufuli kuzipitia upya sera zake ama akubali kuingia katika hatari ya kuwapoteza wawekezaji wote nchini humo.

Raisi Magufuli alipoingia madarakani, wawekezaji na wafanyabisahara walifurahishwa kwa jinsi alivyopambana na rushwa lakini miaka miwili baadae, baadhi ya wafanyabiashara wamegubikwa na hofu hasa baada ya kuona mazingira ya kibiashara yamebadilika kutokana na mfumo wake wa utawala.

Mapema mwaka huu rais Magufuli alianzisha uchunguzi wa kina katika sekta ya madini na kubaini uhalifu mkubwa ambao ulisababishwa kuundwa kwa sheria mpya ya madini.

Katika kongamano lililofanyika mjini London, mfanyabiashara huyo alisema sheria mpya zinazoundwa Tanzania zinaiweka nchi hiyo kwenye hatari ya kuwafukuza wawekezaji wote na kushindwa kuwarejesha tena.

Serikali nchini humo ina amini kwamba sheria hizo zitawanufaisha wananchi kutokana na rasilimali za taifa lao licha ya kwamba makampuni ya kigeni yamekuwa yakipinga mabadiliko hayo ya sheria kwa madai hazitekelezeki.
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget