Mwita atoa neno kwa wenyeviti wa Serikali za mitaa kuhusu uuzwaji wa maeneo yaliyopo mabondeni, yasiyopimwa.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita
NA CHRISTINA MWAGALA,OFISI YA MEYA WA JIJI
MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya
Mwita amewataka wenyeviti wa serikali za mitaa kuepuka kujihusisha kwenye suala
la uuzwaji wa maeneo yaliyopo mabondeni, yasiyopimwa na yenye migogoro.
Aidha Mwita amewaomba waandishi wa habari
kuongoza wananchi katika suala la upandaji wa miti kwenye maeneo wanayoishi.
Mwita amesema kuwa wenyeviti ndio wasimamia
wa maeneo hayo na kwamba wanapaswa kujiepusha na mambo hayo kwani kufanya hivyo
ni kujiingiza kwenye migogoro isiyokuwa
ya lazima na kuwasababishia wananchi kupata usumbufu wa mafuriko nyakati za
mvua.
Kauli ya Meya Mwita imekuja ikiwa ni baada ya
kurejea Jijini hapa akitokea Ujerumani
alipokuwa kwenye mkutano wa Mabadiliko ya Tabia ya nchini uliohusisha Mameya wote
Duniani, na wataalamu wa masuala ya mabadiliko hayo.
Meya Mwita amefafanua kuwa wenyeviti wa
serikali za mitaa ndio wanaosimamia makazi ya wananchi ikiwemo kushugulikia
suala la upimaji na kwamba wanalojukumu kubwa la kuhakikisha kuwa wanaepuka kushiriki
katika suala hilo la uuzwaji wa maeneo ambayo yana asili ya mikondo ya maji.
“ Nikweli kumekuwa na migogoro ya namna hii,
sasa ni jukumu la kila kiongozi kwenye mtaa wake asikubali kujihusisha kwenye uuzwaji
wa maeneo ambayo hayajapimwa, yaliyopo mabondeni, kufanya hivi nikujiletea matatizo
kwao na kwa wananchi pia” amesema Meya Mwita.
Akizungumzia suala la upandaji miti, Meya
Mwita amesema kuwa kila mwananchi anapaswa kupanda miti kwenye maeneo
wanayoishi na akasisitiza kuwa waandishi wa habari wanatakiwa kuwa mfano kwenye
maeneo yao.
“ Suala la upandaji miti ni jukumu la kila
mmoja, lakini katika jiji langu, niwaombe waandishi wa habari muwe mfano kwenye
hili ,kwakuwa nyie ndio kikoo cha jamii, iwe upanga, ama umejenga unapaswa
kupanda mti kwenye eneo lako” amesisitiza Meya Mwita.
Mwita aliongeza kuwa” hata mimi Meya wenu nimepanda
miti kwenye eneo lango, lakini pia nitaendelea kupanda, lakini mtakapounga
mkono jambo hili wananchi pia watapata hamasa kubwa kutoka kwenu.
Post a Comment