NA TIGANYA VINCENTRS-TABORA
SERIKALI imepiga marufuku Halmashauri zote nchini
kuingia makubaliano na Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali(NGO’S) bila kupitia na
kiuhidhinishwa na Ofisi ya Rais , Serikali
za Mitaa na Tawala za Mikoa( TAMISEMI ) kwa kuwa baadhi ya mambo yamekuwa
hayazingatia vipaumbule vya Serikali na kuokuwa na manufaa kwa jamii.
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni mkoani Tabora na
Naibu Katibu Mkuu (ELIMU) Ofisi
ya Rais , Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa( TAMISEMI ) Tixon Nzunda wakati
akizungumza na Watendaji na watumishi wa
Mkoa huo.
Alisema kuwa
mashirika hayapaswi kuanza kazi katika Halmashauri yoyote kabla ya mpango
kazi wao hajaonwa na viongozi wa TAMISEMI ili kujidhirisha kama kweli malengo
yao yanaendana na vipaumbele vya Serikali vya kuboresha maisha ya watanzana
Watanzania ambao maisha yao yako chini.
Nzunda alisema baadhi ya mashirika hayo yamekuwa
yakidai kusaidia Watanzania ,lakini matokeo yake ni kuwanufaisha viongozi wa mashirika hayo na
wachache.
“Kwa mfano Mashirika hayo yanapokuja kutaka fulani kama
vile elimu ni vema yakajua kuwa vipaumbele vya Serikali …….mfano kuboresha
miundo mbinu ya kujifunzia na kufundishia, kuwajengea uwezo walimu, kuwepo na vifaa
vya kufundishia na kuweka mazingira mazuri kwa watoto wenye mahitaji kujifunza
na kusoma katika mazingira rafiki” alisema Nzunda.
Alisema kuwa wanapoaandika taarifa kwenda kwa watu
waliowawezesha fedha wanaonyesha kuwa wamewasaidia Watanzania katika miradi ya
maendeleo ya mabilioni ya fedha kumbe sio kweli fedha nyingi zimeshia mifukoni
kwa wachache na unapoenda katika eneo ambalo wanadai kusaidia hakuna kitu.
Nzunda alisema kuwa Serikali inelenga kuhakikisha
kuwa kama fedha zinatolewa kwa ajili ya walemgwa ziende kusaidia eneo husika na
kama wafadhili wanapokuja waone kuwa fedha waliotoa imefanya kazi inayoonekana
na sio maelezo yasiyo na ushahidi.
Alisema kuwa Serikali inapenda kushirikiana na
wadau mbalimbali lakini ni vema wadau hao watambue kuwa vipo vipaumbele ambavyo
inavikusudia katika kuwaletea maendeleo watu wake.
Katika hatua nyingine Naibu Katibu Mkuu huyo
ameagiza kuwa majengo yote yanayojengwa katika Shule na Taasisi mbalimbali za
elimu yawe rafiki kwa watu wenye mahitaji maalumu na watoto wa kike ili kuondoa
vikwazo vya wao kupata elimu.
Alisema kuwa baadhi ya majengo yamekuwa yakisababu
wanafunzi wenye mahitaji maalumu kushindwa kuhudhiria masomo yao vizuri na
kukwamisha ndoto zao za kuapata elimu.
Nzunda alisema kuwa yapo majengo ambayo yamekuwa
hayana maeneo mazuri kwa ajili ya watoto wa kike na kuwafanya washindwe
kuhudhuria masomo katika kipindi Fulani cha mwezi.
Post a Comment