
RAIS wa Marekani
Donald Trump na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin wamekubaliana
kuhakikisha kundi la wapiganaji wanaojiita Islamic State (IS)
wanashindwa nchini Syria, maafisa wa rais wa Urusi wamesema.
Kwa jumla, viongozi hao wawili walikutana mara tatu katika kipindi cha saa 24 katika mji wa Da Nang hakuna uthibitisho wowote rasmi kutoka kwa Marekani kuhusu tamko hilo la Urusi.
Mkutano kati ya Rais Trump na Vladimir Putin ulitarajiwa kufanyika wakati wa mkutano huo wa Apec, lakini ni maelezo machache sana ambayo yametolewa.
Wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza Julai katika mkutano wa G20 katika mji wa Hamburg nchini Ujerumani.
Ingawa White House haijasema chochote kuhusu mkutano wa wawili hao, taarifa ya Kremlin iliyotolewa Jumamosi imesema viongozi hao "waliafikiana kwamba mzozo wa Syria hauwezi kutatuliwa kwa njia ya kijeshi".
Kadhalika, walikariri "kujitolea kwao kuwashinda Isis [jina jingine la IS" na kuzitaka pande zote kushiriki mazungumzo ya amani ya Geneva.
Urusi imekuwa ikiunga mkono serikali ya Bashar al-Assad katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu miaka sita sasa.
Marekani nayo huwasaidia waasi wa makundi ya Waarabu wa Syria na Wakurdi ambapo angu 2014, Marekani imeongoza muungano ambao umekuwa ukitekeleza mashambulio ya kutoka angani dhidi ya IS nchini Syria.
CHANZO BBC NEWS
Post a Comment