Kidato cha pili kuanza kufanya Mitihani yao kesho.
NA MWANDISHI WETU, DAR
BARAZA la Mitihani la Tanzania limetangaza kuanza
kufanyika kwa mitihani ya kitado cha pili na Darasa la Nne Novemba mwaka huu.
Mitahi hiyo itaanza kwa awamu mbili ambapo
,kesho jumla ya wanafunzi 521,855 wa
kidato cha pili wataanza kufanya mitihani hiyo huku wavulana wakiwa 251, 570
sawa na asilimia 48.21 na wasichana wakiwa 270, 285 sawa na asilimia 51.79.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini
hapa leo, Katibu Mtendaji wa baraza hilo Dk. Charles Msonde amesema kuwa mitihani
ya kidato cha pili itaanza kufanyika kesho Novemba 13 na kumalizika Novemba 24
katika jumla ya shule za Sekondari 4,705.
Amefafanua kuwa katika wanafunzi hao wa
kidato cha pili , wapo wenye uoni hafifu ambao alitaja idadi yake kuwa 330.
Akizungumzia mtihani waupimajiwa kitaifa wa darasa la nne, Dk Msonde amesema jumla ya wanafunzi
1,195,970 wamesajiliwa kufanya mtihani huo mwaka huu.
Ameongeza kuwa kati ya wanafunzi hao
waliosajiliwa ,wavulana ni 592,005 sawa na asilimia 49.50 na wasichana ni
603,965 sawa na asilimia 50.50.
Aidha Dk. Msonde amefafanua kuwa mitihani
hiyo itaanza kufanyika Novemba 22 hadi 23 mwaka huu ambapo utafanyika Tanzania bara
katika jumla ya shule za msingi 17,224.
Amefafanua “kuwa dhana ya upimaji wa kitaifa
hutofautiana na ile ya mitihani ya Taifa kwakuwa upimaji wake hufanywa katikati
ya mafunzo wakati mitihani ya kitaifa hufanyika mwishoni mwa mafunzo.
Akizungumzia kuhusu maandalizi ya mitihani
hiyo, Dk. Msonde amesema yamekamilika ikiwa ni pamoja na kusambazwa kwa
karatasi za maswali yatakayotumika katika upimaji huosambamba na nyaraka zote
muhimu zinazohusu upimaji huo katika mikoa, halmashauri zote Tanzania Bara.
Post a Comment