Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Auwawa na kutelekezwa barabarani huko Tabora

MTU mmoja ambaye jina lake halijatambulika na maeneo ambayo anaishi amekutwa amekufa na mwili wake kutelekezwa katika Barabara ya Mwanza eneo la Kiwanda cha Nyuzi Tabora kilichopo Kata ya Tambukareli Manispaa ya Tabora.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kutokea kwa tukio mauaji jana mjini Taboea na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari hasa watembea majira ya usiku.

Alisema kuwa Polisi wanaendelea na uchunguzi ili kuweza kubaini chanzo cha mauaji hayo ili wahusika weweze kuchukuliwa hatua na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Kitete.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kijiweni  katika Manispaa ya Tabora Mohamed Mayunga amelaani kitendo hicho na kusema ni cha kinyama na kuomba Polisi kuhakikisha wanafuatilia kitendo hicho ili kukomesha mauaji zaidi.

Alisema kuwa pamoja marehemu haijafahamika alikuwa anafanyakazi gani ni vema wakazi wa Tabora hasa madereva wa boda boda wakachukua tahadhari wanapokodishwa nyakati za usiku kwa wapo watu wasio na nia njema kwao.

Mtu huyo anasadikiwa kuwawa kwa kupigwa kwa kitu chenye ncha kali katika sehemu za  kichwa.

 


 

Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget