Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Odinga apendekeza serikali ya muda iundwe Kenya

OdingaHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
KIONGOZI  wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amependekeza serikali ya muda iundwe nchi humo na kutawala kwa muda wa miezi sita kama sehemu ya kutatua mzozo wa kisiasa nchini humo.
 Odinga, ambaye alisusia uchaguzi wa marudio uliofanyika mwezi uliopita, amesema katika kipindi hicho kunafaa kufanyika marekebisho ya katiba kuchunguza upya mamlaka ya rais.
Kiongozi huyo ambaye ameanza ziara nchini Marekani alisema yuko tayari kufanya mazungumzo na Rais Uhuru Kenyatta kuhusu marekebisho ya kikatiba ambayo anasema yanahitajika kupunguza hatari ya kuzuka kwa fujo kutoka kwa makundi ya jamii za wachache ambao wanajiona kwamba wametengwa.
 Kenyatta alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo wa marudio uliofanyika tarehe 26 Oktoba akiwa na kura 7.5 milioni ambazo ni sawa na asilimia 98 ya kura zilizopigwa.
Waliojitokeza kushiriki uchaguzi huo ni asilimia 39 ya waliojiandikisha kuwa wapiga kura nchini humo.
Uchaguzi huo ulitokana na hatua ya Mahakama ya Juu, kufuatia kesi iliyowasilishwa na Bw Odinga, kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa tarehe 8 Agosti ambapo Bw Kenyatta alikuwa ametangazwa mshindi akiwa na asilimia 54 ya kura.
Mahakama ya Juu ilisema uchaguzi huo wa mwanzo ulikumbwa na kasoro nyingi ambapo  Odinga alisusia uchaguzi wa marudio akisisitiza lazima mageuzi yafanywe katika Tume ya Uchaguzi (IEBC).
Alisema hakuna na imani kwamba uchaguzi huo wa marudio ungekuwa huru na wa haki.
Wafuasi wa  Odinga wamekuwa wakiandamana mara kwa mara tangu kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa kwanza.
Watu zaidi ya 50 wameuawa katika makabiliano kati ya polisi na wafuasi wa upinzani.
"Mfumo halisi wa utawala wa urais unaendeleza ukabila kwa sababu kila kabila linahisi kwamba haliko salama ikiwa mtu kutoka kabila hilo si kiongozi," aliambia Reuters kwenye mahojiano.
Wafuasi wa upinzaniHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
Image captionWafuasi wa upinzani wamekuwa wakiandamana mara kwa mara kushinikiza mageuzi katika tume ya uchaguzi
Katiba mpya iliyoanza kutekelezwa mwaka 2010 iligatua baadhi ya mamlaka ya serikali kuu kwa kuunda serikali za majimbo 47 zinazoongozwa na magavana.
Serikali hizo huwa na uwezo wa kujiendeshea shughuli nyingi lakini bw Odinga anasema mamlaka mengi bado yamebaki kwenye serikali kuu na hilo linafaa kubadilika.
"Tulipata katiba mpya mwaka 2010; Tunafikiri kwamba wakati umefika tuiangalie upya," amesema.
Alieleza kuwa marekebisho ya Katiba hiyo yanafaa kuimarisha taasisi huru za serikali mfano tume ya uchaguzi na kupunguza mamlaka ya rais.
"Tunafikiri kwamba pengine miezi sita itatosha kufanikisha marekebisho haya ambayo tunayahitaji katika taifa hili," alisema.
Bw Kenyatta, baada ya kutangazwa mshindi, alisema hatafanya mazungumzo na upinzani hadi umalize njia zote za kisheria za kupinga matokeo ya uchaguzi.
Matokeo kamili ya wagombea wote kama yalivyotangazwa na IEBC
MgombeaChamaKuraAsilimia
Uhuru KenyattaJubilee7,483,89598.28
Raila Odinga (Alisusia)ODM73,2280.96
Mohamed Abduba DidaARK14,1070.19
Japheth Kavinga KaluyuMgombea wa kujitegemea8,2610.11
Michael Wainaina MwauraMgombea wa kujitegemea6,0070.08
Joseph Nthiga NyagahMgombea wa kujitegemea5,5540.07
John Ekuru AukotThirdway Alliance21,3330.28
Cyrus JirongoUDP3,8320.05
 Odinga, siku moja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi alitangaza kwamba atageuza muungano wake wa National Super Alliance (Nasa) kuwa vuguvugu la kupinga serikali.
Majuzi, muungano wake uliwahimiza wafuasi wake kususia bidhaa na huduma za kampuni tatu kuu ambazo alisema zimekuwa zikiisaidia serikali ya Rais Kenyatta.
Kesi mbili ziliwasilishwa kupinga ushindi wa Bw Kenyatta Jumatatu katika Mahakama ya Juu.
Mahakama hiyo ina siku 14 kusikiliza na kutoa uamuzi kuhusu kesi hizo.
Upinzani ulipinga matokeo ya uchaguzi wa marudio na badala yake kusema uchaguzi mpya unafaa kufanyika katika kipindi cha siku 90.
Nasa hata hivyo hawajawasilisha kesi ya kupinga matokeo hayo mahakamani.
CHANZO BBC NEWS
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget