Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Kidato cha pili kuanza kufanya Mitihani yao kesho.



 

Image result for dk msonde 

NA MWANDISHI WETU, DAR

BARAZA la Mitihani la Tanzania limetangaza kuanza kufanyika kwa mitihani ya kitado cha pili na Darasa la Nne Novemba mwaka huu.

Mitahi hiyo itaanza kwa awamu mbili ambapo ,kesho jumla ya wanafunzi  521,855 wa kidato cha pili wataanza kufanya mitihani hiyo huku wavulana wakiwa 251, 570 sawa na asilimia 48.21 na wasichana wakiwa 270, 285 sawa na asilimia 51.79.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa leo, Katibu Mtendaji wa baraza hilo Dk. Charles Msonde amesema kuwa mitihani ya kidato cha pili itaanza kufanyika kesho Novemba 13 na kumalizika Novemba 24 katika jumla ya shule za Sekondari 4,705.

Amefafanua kuwa katika wanafunzi hao wa kidato cha pili , wapo wenye uoni hafifu ambao alitaja idadi yake kuwa 330.

Akizungumzia mtihani wa  upimaji  wa kitaifa wa darasa la nne, Dk Msonde amesema jumla ya wanafunzi 1,195,970 wamesajiliwa kufanya mtihani huo mwaka huu.

Ameongeza kuwa kati ya wanafunzi hao waliosajiliwa ,wavulana ni 592,005 sawa na asilimia 49.50 na wasichana ni 603,965 sawa na asilimia 50.50.

Aidha Dk. Msonde amefafanua kuwa mitihani hiyo itaanza kufanyika Novemba 22 hadi 23 mwaka huu ambapo utafanyika Tanzania bara katika jumla ya shule za msingi 17,224.

Amefafanua “kuwa dhana ya upimaji wa kitaifa hutofautiana na ile ya mitihani ya Taifa kwakuwa upimaji wake hufanywa katikati ya mafunzo wakati mitihani ya kitaifa hufanyika mwishoni mwa mafunzo.

Akizungumzia kuhusu maandalizi ya mitihani hiyo, Dk. Msonde amesema yamekamilika ikiwa ni pamoja na kusambazwa kwa karatasi za maswali yatakayotumika katika upimaji huosambamba na nyaraka zote muhimu zinazohusu upimaji huo katika mikoa, halmashauri zote Tanzania Bara.



Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget