Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

WAPANGAJI WA URAFIKI WA ONDOLEWA KWA NGUVU

Uongozi wa kiwanda cha Urafiki umeanza kuwaondoa kwa nguvu wadaiwa sugu sambamba na kuchukua mali zao kwaajili ya kufidia malipo ya fedha ya kodi ya pango wanayodaiwa.

Hilo limebainishwa leo na Naibu Meneja mkuu kiwanda cha Urafiki Shadrack Nkelebe, ambaye amesema zoezi hilo linaendeshwa na kampuni ya udalali ya YONO na tayari wameshawaondoa wapangaji 90 kwa awamu ya kwanza.

Nkelebe amesema awali walitoa siku 14 kwaajili ya wadaiwa hao kuhakikisha wanalipa madeni yao lakini zimeisha bila kufanya utekelezaji hivyo kulazimika kutumia nguvu ili kuwaondoa na kupata fedha za kufidia.

Nkelebe ameongeza kuwa fedha zitakazopatikana zitatumika kwaajili ya kuongeza pato la kiwanda sambamba na kuongeza uzalishaji kwa kutengeneza na kununua vitendea kazi vya kisasa.

Kwa upande wake naibu Mhasibu wa kiwanda hicho Levina Kahwa amesema wanadai zaidi ya shilingi milioni 600 kwa wapangaji hao lakini tayari asilimia 60 wameanza kulipa baada ya zoezi hilo kuanza.

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget