Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

NECTA YATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI,DARASA LA NNE


BARAZA la mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mitihani ya upimaji wa darasa nne na kidato cha pili iliyofanyika Novemba mwaka jana, huku idadi kubwa ya wanafunzi wakifaulu vizuri katika mitihani hiyo.
Akitangaza matokeo hayo leo Jumatatu, Januari 8, Katibu Mtendaji wa baraza hilo,  Dk Charles Msonde amesema jumla ya wanafunzi 1,086,156 waliofanya mtihani wa darasa la nne wamefaulu  kati ya 1,158,444 waliofanya upimaji huo.
Amesema  wanafunzi hao wamefaulu kwa kupata alama zenye madaraja ya A,B,C na D wakati wanafunzi 72,288 sawa na asilimilia 6.24 wamepata alama za daraja E, ambao ni ufaulu usioridhisha.
Kuhusu matokea ya upimaji wa kidato cha pili, Dk Msonde  amesema jumla ya wanafunzi 433,453 sawa na asilimia 82.32 kati ya 486,742 waliosajiliwa  kufanya mtihani huo wamepata ujuzi wa maarifa ya kuwawezesha kuendelea  na kidato cha tatu.
Dk Msonde alisema wanafunzi wa kidato cha pili  51,807 sawa na asilimia 10.68 wameshindwa kupata alama za kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu.

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget