Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

HUYU NDIYE KIGOGO ALIYETANGAZWA KUJIUNGA NA CCM LEO

Aliyekuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Bodi ya Udhaminia, na Mshauri wa Mameya wa Dar es Salaam, Muslim Hassanal ametangaza kujivua uanachama wa Chama hicho pamoja na nafasi zake zote za Uongozi na kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Tukio hilo limetokea leo katika ukumbi wa Check Point Pugu Dar es Salaam ambapo Hassanal alirudisha kadi ya Chadema na kukabidhiwa mpya ya CCM na Makamu Mwenyekiti CCM bara, Philip Mangula.

Akizungumzi ya baada ya kula kiapo mbele ya Mangula, Hassanal alisema sababu kubwa ya kujiunga na CtCM ni kuunga utendaji kazi wa Rais Magufuli katika kuleta maendeleo ambayo yeye na wapinzani wamekuwa wakiyapigia kelele kwa muda mrefu.

" Mimi sijanunuliwa kama watu wanavyosema, nimejiunga mwenyewe kwa mapenzi yangu ili kumshauri Rais na kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli katika kuleta maendeleo kwa Nchi yangu.

" Sina sababu ya kubaki upinzani wakati tuliyokuwa tunayapigia kelele kwa muda mrefu sasa yanafanywa na Rais, nitaitumikia CCM kwa nguvu zangu zote na kama nitahitajika katika nafasi za uongozi nitaikubali kwa moyo mkunjufu," Alisema Muslim.

Kwa upande wake Mangula alimkaribisha Muslim ndani ya CCM na kumueleza kuwa yale ambayo upinzani wamekuwa wakiyapigia kelele sasa wao wanayafanya hivyo wapinzani hawana tena hoja na wamebaki kukosoa kila jambo ambalo linafanywa na Serikali ya CCM

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget