Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

WENGER AMTETEA SANCHEZ


  MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amemtetea mchezaji wa zaman wa klabu 
aliyehamia Manchester United baada yake kukosa kipimo muhimu kuhusu matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mwilini.

Aidha, amesema klabu hiyo haifichi habari zozote kuhusu tukio hilo.

Raia huyo wa Chile mwenye miaka 29 anadaiwa kukosa kipimo muhimu Jumatatu siku ambapo alikamilisha uhamisho wake kwenda Manchester United.

"Nafikiri lilikuwa tukio la kipekee, kwake kukosa kipimo siku hiyo kwa sababu alikuwa kwingine," amesema Wenger.

Mfaransa huyo ameongeza pia kwamba klabu yake haijaombwa ufafanuzi wowote na Chama cha Soka cha England au Shirika la kupambana na matumizi ya dawa zilizoharamishwa michezoni Uingereza.

Sanchez alihamia Gunners kutoka Barcelona mwaka 2014, lakini alielekea Old Trafford kwa kubadilishana na mchezaji wa Armenia Henrikh Mkhitaryan.

Baada ya taarifa za awali Uhispania, magazeti ya Uingereza Alhamisi yaliripoti kwamba Sanchez alikiuka kanuni FA ya kupatikana wakati wowote ule anapotakiwa kupimwa.

Sanchez na Mkhitaryan walipigwa picha wakiwa afisi za uhamiaji Liverpool wakitafuta vibali vya kufanya kazi kabla ya kukamilisha uhamisho wake.

Wenger amesema: "Jumatatu kulikuwa na mengi sana yaliyokuwa yanatokea, ni siku ya kipekee sana kwa Alexis Sanchez - kujaza stakabadhi muhimu, vibali vya kazi na usafiri. Alikuwa bado ni mchezaji wetu Jumatatu au la? Huwezi kujua.

"Ni siku mbaya tu kwako kutafutwa ukapimwe. Kusema kweli, ukiangalia upande wa usimamizi, huenda ikawa bado ilikuwa ni wajibu wetu kwa kuwa hakuwa amehama. Sijui nini hasa kilitokea.

"Sina wasiwasi kwa sababu hatuna chochote cha kuficha, huwa tunajaribu sana kadiri ya uwezo wetu kushirikiana na maafisa wa kupambana na matumizi ya dawa zilizoharamishwa michezoni Uingereza.

"Nia ya Alexis haikuwa kujificha na sisi hatuna jambo la kuficha."

Sheria zinasemaje?

Klabu zinatakiwa kutoa maelezo sahihi ya kina kuhusu vipindi vya mazoezi na walipo wachezaji ili waweze kupimwa wakati wowote ule.

Klabu ikikosa kufanya hivyo - au maafisa wa kupima wachezaji washindwe kumpata mchezaji wanayemtafuta - mara tatu kipindi cha miezi 12, basi huchukuliwa kwamba amekiuka sheria za FA.

Manchester City na Bournemouth mwaka jana walitozwa faini ya £35,000 kila mmoja na kutahadharishwa baada ya kukiuka kanuni hizo.

Arsenal wamemnunua yeyote?

Wenger amesema hawapo karibu kumnunua mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang. Ofa yao ya pili ya euro 50m (£43.64m) ilikataliwa wiki hii.

Borussia wanaaminika kutaka walipwe zaidi ya £50m kwa mchezaji huyo wa Gabon wa miaka 28.

Wenger pia amesema hataki kumpoteza Olivier Giroud.

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget