Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA

 JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kukubaliana na vitendo vya uhalifu ili kuhakikisha kuwa wakazi wa Mkoa huu wanaendelea kuwa salama na mali zao.
KUHARIBU MIUNDOMBINU YA KAMPUNI YA MAWASILIANO – TTCL.
Siku za hivi karibuni Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilipata taarifa kuhusu uhalifu wa kuhujumu miundombinu ya Kampuni ya Mawasiliano Tanzania [TTCL]. Katika uhalifu huo, wahalifu wamekuwa wanakata nyaya hizo kutoka kwenye nguzo na zingine kuzichimbua ardhini na kwenda kuuzwa kama vyuma chakavu.
Kutokana na taarifa hizo, Jeshi la Polisi liliunda kikosi kazi kwa kushirikiana na Maafisa wa Kampuni ya Mawasiliano Tanzania [TTCL] ili kubaini wahusika wanaoshiriki kufanya uhalifu huo. Taarifa za kiintelijensia zilipatikana na kuanzia tarehe 31/12/2017 hadi tarehe 05/01/2018 Operesheni ilifanyika katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya na kufanikiwa kuutia mbaroni mtandao wa wahalifu wanaojihusisha kuhujumu miundombinu ya TTCL kwa maana nyaya kwa kuzikata kwenye nguzo na zile zilizochimbuliwa ardhini.
Aidha pamoja na kuwatia mbaroni watuhumiwa, pia nyaya zilizohujumiwa za TTCL pamoja na Makampuni mengine kama TANESCO vilikamatwa katika maeneo ya watuhumiwa hao.
Katika Operesheni hiyo jumla ya watuhumiwa 06 walikamatwa wakiwa na nyaya za TTCL. Watuhumiwa hao ni:-
  1. JACKSON NGALA [28] Mkazi wa Ilemi.
  2. MOSES SINYINZA [22] Mkazi wa Ilomba.
  3. LAURENT JONAS [30] Mkazi wa Forest Mpya.
  4. WILIAM JEREMIA [26] Mkazi wa Makondeko – Mwakibete.
  5. ANDREA JOSEPH [26] Mkazi wa Makondeko – Mwakibete.
  6. DICKSON FREDRICK [18] Mkazi wa Mama John – wote wa Jijini Mbeya.
Aidha imebainika kuwa maeneo yaliyopata athari zaidi katika Mkoa wa Mbeya kutokana na kuharibiwa kwa miundombinu hiyo ni:-
  1. Eneo la Gombe – Itezi ambapo nyaya zenye urefu wa mita 150 zilikatwa.
  2. Eneo la Stendi Kuu ya Mabasi ambapo nyaya zenye urefu wa mita 50 zilikatwa.
  3. Eneo la Kiwanja Ngoma – Sokomatola ambapo nyaya zenye urefu wa mita 200 zilikatwa.
  4. Eneo la Ghana – Mbata nyaya zenye urefu wa mita 100 zilikatwa.
Halikadhali katika Operesheni hiyo, mali mbalimbali ambazo ni nyaya za Kampuni ya Mawasiliano – TTCL zilikamatwa kama ifuatavyo:-
  1. Nyaya zenye uzito wa kilogram 22.5 – Mali ya TTCL Mbeya.
  2. Mita za maji 08 [Reading Meters] Mali ya Idara ya Maji Mbeya.
  3. Nyaya zenye uzito wa kilogram 105 – Mali ya TANESCO Mbeya.
Hata hivyo hadi sasa thamani halisi ya mali zote zilizopatikana bado haijafahamika, tunaendelea kuwasiliana na Idara husika kuweza kujua thamani halisi ya mali hizo.
Watuhumiwa wote mara baada ya kuhojiwa wamekiri kushiriki katika wizi na kuhujumu miundombinu ya Makampuni ya TTCL, TANESCO na Idara ya Maji.
WITO:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi MOHAMMED R. MPINGA anatoa wito kwa jamii kuondokana na tamaa ya kutaka utajiri kwa njia zisizo halali kwa kujihusisha na uhalifu na badala yake watafute shughuli halali kwa ajili ya kujipatia kipato. Aidha anatoa onyo kali kwa wanaonunua vyuma chakavu kuacha mara moja kununua vyuma chakavu vilivyoibiwa katika miundombinu mbalimbali kama hii ya TTCL, Idara ya Maji, TANESCO, Reli n.k. Pia anatoa rai kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuzuia uhalifu. Aidha Kamanda MPINGA anawaasa wananchi kutoharibu miundombinu iliyowekwa na serikali ambayo imegharimu fedha nyingi ili kuleta maendeleo na kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya umeme, maji na mawasiliano kwani kufanya hivyo ni kuhujumu maendeleo ya nchi.  
         Imesainiwa na:           
[MOHAMMED R. MPINGA – DCP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYAshiESHI Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kukubaliana na vitendo vya uhalifu ili kuhakikisha kuwa wakazi wa Mkoa huu wanaendelea kuwa salama na mali zao.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget