Muonekano wa jengo la
kiwanja cha ndege cha Shinyanga.
|
Muonekano wa kiwanja
cha Ndege cha Shinyanga ambacho kinatarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami na
Mkandarasi wa Kampuni ya ujenzi ya China ya CHICO.
|
NAIBU Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya Ujenzi), Elius
Kwandikwa, amemtaka Mkandarasi wa kampuni ya ujenzi ya China ya CHICO aliyepewa
zabuni ya ujenzi wa Kiwanja cha ndege cha Shinyanga kuanza ujenzi huo haraka.
Akizungumza mara baada
ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanja hicho katika eneo la Ibadakuli
leo, mkoani Shinyanga, Kwandikwa,
amesema kuwa haoni sababu ya mkandarasi huyo kuchelewa kuleta vifaa vyake
katika eneo la mradi hadi sasa wakati tayari mkataba wa kuanza kazi hiyo
umeshasainiwa.
"Mkandarasi hana
sababu ya kuchelewa kuanza kazi wakati fedha zipo na zimeshatengwa kwa ajili ya
mradi huu na mkataba umeshasainiwa, sasa namwagiza kuleta vifaa vyake na
kuanza kazi mara moja", amesema Mhe. Kwandikwa.
Aidha, Kwandikwa amemtaka Meneja wa kiwanja hicho, Julius Msollow kuhakikisha anakuwa bega kwa bega na kutoa ushirikiano kwa kumsimamia mkandarasi huyo, ili kuhakikisha kiwanja hicho kinakamilika mapema na kwa viwango vinavyotakiwa.

"Naamini
tukimsimamia vizuri mkandarasi huyu tutapata kiwanja kizuri na imara hapa
Shinyanga na tutafungua fursa mbalimbali za kiuchumi katika mkoa huu",
amesisitiza Mhe. Kwandikwa.
Kwa upande wake,
Meneja wa kiwanja cha ndege cha Shinyanga, Msollow, amemhakikishia na kuahidi kuwa atatoa
ushirikiano kwa mkandarasi huyo atakapowasili eneo la mradi.
Msollow amesema kuwa mradi huo utahusisha
ujenzi wa barabara ya kuruka na kutua ndege, jengo la abiria, maeneo ya
maegesho ya ndege na mnara wa kuongozea ndege.
Amesema barabara ya kutua na kupaa kwa ndege inarefushwa kwa urefu wa Kilometa mbili na itakuwa kwa kiwango cha lami, ikigharimu zaidi ya shilingi Bilioni 49.
Amesema barabara ya kutua na kupaa kwa ndege inarefushwa kwa urefu wa Kilometa mbili na itakuwa kwa kiwango cha lami, ikigharimu zaidi ya shilingi Bilioni 49.
Wakati huohuo, Naibu
Waziri Kwandikwa, amekagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Mwigumbi - Maswa
(KM 50.3), mkoani Simiyu na kumsisitiza mkandarasi anayejenga barabara hiyo
kuikamilisha kwa wakati na kwa viwango.
Amesisitiza kuwa kukamilika kwa barabara hiyo ambayo ni kiungo kwa wananchi wa Maswa, Bariadi, Lamadi na Mwanza, kutarahisisha huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo katika maeneo hayo.
Amesisitiza kuwa kukamilika kwa barabara hiyo ambayo ni kiungo kwa wananchi wa Maswa, Bariadi, Lamadi na Mwanza, kutarahisisha huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo katika maeneo hayo.
Naye, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoani Simiyu, Mhandisi Albert Kent, amesema kuwa mradi upo katika hatua nzuri na unatarajiwa kukamilika ndani ya miaka miwili kutoka sasa.
Naibu Waziri Kwandikwa
amefanya ziara ya kikazi katika mkoa wa Shinyanga na Simiyu ambapo amekagua
miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wizara yake.
Post a Comment