WALIMU wilayani Sikonge wameiomba Serikali kuangalia uwezekano
wa kulipa madai ya muda mrefu kwani yamekuwa yakipunguza ari ya utekelezaji wa
majukumu yao ya kila siku.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Walimu (CWT)
wilayani Sikonge Perez Kuduhula katika mkutano uliowakutanisha walimu hao kwa
lengo la kutathmini utendaji wao wa kazi pamoja na kujadili changamoto
mbalimbali zinazowakabili
Alisema kuwa baadhi ya walimu walishapandishwa madaraja lakini
wamekuwa wakiendelea kupata mshahara ule ule wa kabla hajapandishwa.
Kuduhula aliongeza kuwa wapo wengine wamekuwa wakidai gharama za
masomo , nauli na gharama za matibabu jambo ambalo linawatia hadi sasa
hawajatimiziwa.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Sikonge Simon Ngatunga aliwataka walimu hao kuwa wavumilivu kwani serikali
inafanya jitihada za kulipa madai yao.
Alisema kuwa Halmashauri hiyo itaendelea kulipa madai hayo ya
walimu kadiri itakavyokuwa ikipokea fedha .
Naye Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alisema kuwa pamoja na
changamoto hizo zinazowakabili walimu amewataka walimu kuendelea kujituma ili
kuongeza ufaulu wa wanafunzi.
Alisema kuwa Serikali inaendelea kushughulikia matatizo yao ya
ya wale watumishi wengine ni vema wakawa na subira kwani ilikuwa katika zoezi
zito la kuhakiki wafanyakazi hewa.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora Mwanri ametoa
wiki mbili kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya, Mji na Manispaa pamoja na
Maafisa elimu wilaya kukaa na Wazazi na Walezi kupanga mipango ya kutekeleza
utoaji wachakula kwa wanafunzi kwa shule ambazo hazijaanza kutekeleza mpanga
huo.
Alisema kuwa Kiongozi yoyote mwenye dhamana atakayeshindwa
kutekeleza jukumu hilo hatasita kumwajibisha kwani ukosefu wa chakula shule
hasa kwa wale wanafunzi wanaoishi mbalimbali na shule umekuwa ukisababisha
utoro na ufaulu mbaya.
Mwanri alisema kuwa mwanafunzi hawezi kumsikiliza vizuri mwalimu
kama anasumbuliwa na njaa na wakati mwingine anatoroka shule pindi anapokuwa na
njaa.
Post a Comment