Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela
(aliyenyoosha mkono), akimfafanulia jambo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Mhe. Mhandisi Atashasta
Nditiye (wa nne kulia) wakiwa kwenye eneo la abiria wanaowasili kutoka nje
ya nchi.
Kaanankira Mbise, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhamiaji
Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), akieleza namna
abiria anavyopata huduma ya viza mbele ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye
(kushoto), huku Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania
(TAA), Bw. Richard Mayongela (kulia) akisikiliza kwa makini
Naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Mhe. Mhandisi
Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) akiwaeleza jambo Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela
(kulia) na Kaimu Mkurugenzi Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius
Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka katika eneo la kuchukua mizigo baada
ya kuwasili.
Na
Mwandishi Wetu
JENGO
la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(JNIA-TBIII) linalotarajiwa kukamilika Desemba 2018, litafungwa mfumo wa huduma
ya viza kwa njia ya mtandao (e-visa), ambao utarahisha na kuharakisha upatikanaji
wake.
Kaimu
Mkuu wa Kitengo cha Uhamiaji cha JNIA, Bw. Kaanankira Mbise amemwambia jana
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na
Mawasiliano), Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye alipotembelea eneo la uombeaji
viza kwa abiria wa kimataifa wanaowasili, kuwa wanatarajia kutumia huduma hiyo
ambayo ni rahisi na haraka.
“Tayari
mkakati umeanza wa kuanzisha huduma hii ya e-visa hivyo tukifanikiwa utafungwa
katika jengo hili jipya, ambapo itasaidia kwa abiria kuipata huduma hiyo kwa
haraka kwani itatumia mtandao,” amesema
Bw. Mbise.
Hata
hivyo, Bw. Mbise amesema kwa sasa wameboresha huduma hiyo kwa wasafiri
wanaowasili katika jengo la pili la abiria (JNIA-TBII) , ambapo tayari
wamepatiwa mashine nne za kisasa zinazosaidia kupunguza msongamano wa abiria
wenye kuhitaji huduma hiyo, hususan kipindi cha mchana chenye ujio wa ndege
nyingi za nje ya nchi.
“Hizi
mashine zimeharakisha upatikanaji wa huduma kwani tumeweza kuhudumia abiria
wengi kwa wakati mmoja, na msongamano umepungua kiasi tofauti na awali mashine
zilikuwa chache.” amesema Mbise.
Naye
Mhe. Mhandisi Nditiye amesema baada ya ziara yake amegundua mashine za viza ni
za muda mrefu na zinahudumia abiria mmoja kwa mrefu, na tayari ameuagiza
uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kuwasilisha kwa
maandishi mapendekezo yao ya namna ya kuharakisha huduma hiyo, ili serikali iyafanyie
kazi kwa kusaidia kuondoa kero hiyo.
“Nimegundua
kuna baadhi ya mashine za viza zimeongezwa lakini pia zilizopo zimechoka kwani
ni za muda mrefu na zinahudumia abiria mmoja kwa muda mrefu na hii inaharibu
sifa ya kiwanja chetu kwa wageni wanaokuja hapa nchini,” amesema Mhandisi
Nditiye.
Hata hivyo,
amesema wanampango wa kuongeza madirisha ya benki yanayolipia viza hizo ili kuharakisha
huduma hiyo, ambapo sasa ni machache kulinganisha na idadi kubwa ya abiria
wanaowasili kwa ndege kubwa. Ndege hizo ni Emirates, Etihad, Oman Air, Qatar,
South Africa Air na Ethiopia, ambazo zimekuwa zikipishana kwa muda mfupi.
Naye
Kaimu Mkurugenzi wa TAA, Richard Mayongela amesema tayari wanampango wa
kuongeza upana wa eneo hilo la wasafiri wanaowasili wa kimataifa, ambapo sasa
kumekuwa na msongamano kutokana na ufinyu wake.
“Hili
jengo linazaidi ya miaka 30 na ukiangalia abiria waliokuwa wamekadiriwa wakati
ule lilikuwa likikidhi mahitaji, lakini sasa abiria wameongezeka na eneo
limekuwa dogo, hivyo tayari tumeanza kwa kuondoa baadhi ya ofisi ili kuongeza
upana wake, ninaimani litapunguza msongamano uliopo sasa,” amesema Bw.
Mayongela.
Lakini
pia Bw. Mayongela amesema sasa wapo katika mazungumzo na Mamlaka ya Usafiri wa
Anga (TCAA), ili kuangalia namna bora ya kuzipangia muda ndege zinazopishana
muda mdogo kwa wakati wa mchana ili ziachiane muda mrefu, ambapo kutasaidia
kupunguza msongamano
Awali
eneo hilo linakumbwa na changamoto kubwa ya msongamano wa abiria wanaohitaji
huduma ya viza baada ya uchache mashine zinazosimamiwa na Idara ya Uhamiaji zilizokuwepo
na kufanya abiria wanaohitaji huduma hiyo kutumia muda mrefu kuipata.
Post a Comment