Profesa Mbarawa amesema hayo alipokagua ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), inayojengwa usiku na mchana kuanzia Dar es Salaam-Morogoro yenye urefu wa KM 205 na kuzungumzia kuridhishwa na kasi ya ujenzi huo.
“Hii ni fursa
kubwa ambayo mmeipata kujenga mradi mkubwa utakaocha historia katika nchi hii
hivyo fanyeni kazi kwa bidii, weledi na uzalendo”, amesema Waziri Prof.
Mbarawa.
Amewataka viongozi
wa Shirika Hodhi la Rasilimali za Reli (RAHCO), kuwa katika eneo la mradi wakati
wote ili kuhakikisha mkandarasi anapata ushirikiano wa kutosha na hivyo
kuwezesha mradi kukamilika kama ilivopangwa.
Aidha amemuagiza
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO Mhandisi Edward Malima, kuhakikisha wanafunzi wa
uhandisi wanapata nafasi ya kutosha ya kushiriki kwa vitendo katika ujenzi huo
ili kuiwezesha nchi kuwa na wataalamu wa kutosha wenye uzoefu kwenye ujenzi na
usimamizi wa miradi ya reli.
“Ongezeni
wahandisi wanafunzi katika mradi huu, nia yetu ni kupata reli lakini pia na
wataalamu wengi katika ujenzi na uendeshaji wa reli”, amesisitiza Prof.
Mbarawa.
Naye Mhandisi Edward Malima, amempongeza Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa kufanya ziara ya kustukiza usiku ambayo
imechochea hamasa kwa wafanyakazi na mkandarasi na kuahidi kumsimamia mkandarasi kikamilifu ili mradi
huo ukamilike kwa wakati na uwiane na thamani ya fedha.
Takribani
shilingi trilioni 2.8 zinatarajiwa kutumika kujenga reli ya kisasa (SGR), awamu
ya kwaza kati ya Dar es Salaam na Morogoro yenye urefu wa KM 205 itakayowezesha
treni ya umeme yenye kasi ya KM 160 kwa saa kupita na hivyo kuhuisha mfumo wa
usafiri wa reli hapa nchini.
Post a Comment